Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Mgao wa umeme bado ni tatizo. Suala la line moja ya umeme kukatiwa umeme kwa zaidi ya saa tano ni jambo la kawaida kwenye baadhi ya maeneo. Tunatumia nguzo katika kusafirisha umeme, nguzo ambazo wakati wa upepo mkali husababisha umeme kukatika wakati miti mikubwa inaziangukia. Mvua ya nusu saa ambayo inaambatana na upepo mkali inatosha kabisa kuufanya umeme ukatike katika baadhi ya sehemu za miji yetu.
Siku za karibuni waziri Muhongo ameonekana sana akiongea na wadau wa sekta za umeme kutoka Ulaya na kwingineko. Wanaovutiwa ni wenye uwezo wa kusaidia uboreshaji wa upatikanaji wa umeme. Na ndani ya wakati huo huo wanaovutiwa kuwekeza ni wafanyabiashara wenye lengo la kuanzisha viwanda. Ushauri wangu kwa wizara hii nyeti, ni kwamba waangalie ni namna gani tunaweza kuondoka na utegemezi wa umeme wa nguzo.
Tunaingia kwenye nchi ya viwanda, nchi ambayo umeme unapokatika wanaopata hasara ni wengi ambao wapo tayari kuishtaki TANESCO kila watakapopata hasara kwa sababu ya upatikanaji duni wa umeme.
Wizara ya Mheshimiwa Muhongo ijipange kweli, ili serikali isije ikaingia kwenye mtego wa kuanza kulipa fidia yale makampuni makubwa yenye kumiliki viwanda vikubwa.
Serikali ijipange ili nchi inapoingia kwenye pilikapilika za viwanda, tuwe tumeshaachana na hizi habari za mikoa mitano ya kanda ya kati kukosa umeme ndani ya jumamosi na jumapili kwa sababu ya matengenezo ya mtambo fulani mkubwa.
Wenye viwanda vyao hawatakuwa tayari kupokea habari za matengenezo ya mitambo yetu kama kisingizio cha hasara walizozipata kwenye viwanda vyao.
Waziri Sospeter Muhongo tunapokwenda kunahitaji zaidi ya umakini, kunahitaji kujipanga kwelikweli.