Waziri Mpango pitia upya suala hili la Kodi

mdetichia

JF-Expert Member
Feb 13, 2015
5,292
2,169
Ndugu wana body kumekuwa na kilio cha miaka miingi, kuhusu mfumo wa kodi jinsi ulivyo hapa
nchini kwetu Tanzania na kwa uhalisia ndivyo ulivyo,

Na kuwafanya wafanyabiashara wengi kukwepa kulipa kodi kutokana na kupata kafaida kiduchu tofauti na mataifa mengine,
kitendo kinachowafanya baadhi wafanya biashara kumbizana na serikali katika ulipaji wa kodi kama paka na panya,

Ipo hivi ni rahisi sana mfanyabiashara wa Tanzania kwenda Kenya kununua mzigo unaotoka china na kulipia vibali vyoote stahiki na kuja kuuza hapa Tanzania na kupata faida nzuri na serikali kupata mapato yake,

Na inakuwa ni ngumu mfanyabiashara wa hapa Tanzania kuagiza mzigo uleule kutoka China gharama yake inakuwa kubwa na pia faida yake inakuwa ndogo sana, hembu fikiria umeagiza mzigo china ukiwa bandarini unaulipia kodi, ukiuza mzigo huo huo unaulipia kodi,
Swali linakuja ni kwa nini mzigo ule ule wa china ukiununulia nchi jirani ya Kenya una faida tofauti na ukiuagiza mzigo uleule wa china kupitia hapa kwetu faida yake haionekani?

Waziri husika unaonaje ukatuma wachumi hata wawili wakaenda kwenye nchi kuangalia nini wenzetu wanachofanya ili tuweze kuwa na tija na kulipa kodi bila kuumizana na kuwa rafiki
Kama wenzetu wamarekani?

Mimi naamini utitiri wa kodi ukiondolewa na ile asilimia 18 ya vat ikaondolewa na kufikia mpaka asilimia 8 tutainuka kama Tai na hakuna atakae kuwa na moyo mgumu na lawama za kulipa kodi bila shurti

Kuna vyanzo vingi vya mapato mfano madini, bahari,mlima , mbuga za wanyama (utalii) Bandari gesi nina imani tukisimamia huko na kuwa na mipango thabiti wallah hii nchi itapiga hatua kama nchi nyingine,

Tupende kuiga vizuri vya wenzetu na tuwe na wivu wa maendeleo sio maneno matupu utitiri wa kodi unaturudisha watanzania hatua tano nyuma badala ya kusonga mbele

Nina imani kwa pamoja tunaweza.
 
Back
Top Bottom