Waziri Mkuu: Watanzania 578 wamefungwa nje ya nchi kwa makosa yanayohusiana na madawa ya kulevya.

MLAU

JF-Expert Member
Aug 23, 2007
4,726
3,358
Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa aliyasema hayo 11/2/2017 wakati akihairisha Mkutano wa Bunge mkoani Dodoma

Na katika hotuba yake aliunga jitihada za vita dhidi ya madawa ya kulevya na kuomba kila mtanzania kushiriki kwa namna moja au nyingine.

Waziri Mkuu alitoa takwimu za jumla kama ifuatavyo:

China watanzania wamefungwa 200,Brazili 12,Iran 63,Ethiopia 7 na Afrika ya kusini wamefungwa watanzania 296.Jumla ni 578

Hizo ni takwimu katika hizo nchi lakini huenda ni zaidi ya hapo na labda hata na wengine labda wamenyongwa kabisa.
 
Walikamatwa na ushahidi.

Na hapa kwetu tukitaka kuwatia hatiani na kupunguza hao punda hatuna budi kuwakamata na ushahidi.

Tusiitumie vita ya kupambana na madawa ya kulevya kupatia kiki za kisiasa au kwa visasi.
 
Kuna ile nchi tuliyotiliana saini mkataba wa kubadilishana wafungwa. Siioni Thailand hapo.
 
Kama wanazo hizo taarifa, na baadhi ya hizo nchi wa uwakilishi wa kibalozi ni kwanini hawaombi nchi zinazo washikilia zikawaruhusu wawahoji ili kujua walikuwa punda wa nani?
Kuliko hivi sasa kuharibu heshima za watu ambao labda hawajui unga mwingine zaidi ya sembe na dona.
Tuwe wabunifu na watii wa sheria na katiba na sio kuongoza kimabavu..
 
Walikamatwa na ushahidi.

Na hapa kwetu tukitaka kuwatia hatiani na kupunguza hao punda hatuna budi kuwakamata na ushahidi.

Tusiitumie vita ya kupambana na madawa ya kulevya kupatia kiki za kisiasa au kwa visasi.
Acha kuropoka. Dj ni juuza sembe. Aende polisi akajisalimishe
 
Wenzetu kama China ukikamatwa na ushahidi hawarembi, ila kwetu mkuu wa nchi anashangaa kesi kuchelewa wakati watuhumiwa wamekatwa na ushahidi na mashuhuda wapo tunasema abavunja katiba.

Bila kukunjiana sura binadam sisi wa ajabu sana, hakuna kitakachofanyika na sisi tunaotetea wahalifu ndiyo tunaongoza kwa kulalamika.
 
Mbowe, Manji, idd azan na askofu mnatumalizia vijana wetu. Rais magufuli kama unaiona hii comment yangu Nakuomba msaidie makonda kikosi cha jeshi kabisa ili Hawa wafanya biashara wa ngada hasa wale WA kati wapigwe kabisa Hawa wakubwa na hela zao tumewajua Sasa watatueleza vizuri
 
Hili swala waachiwe wazazi na walezi wenyewe tu watajua wenyewe namna ya ku-deal na watoto wao.
 
Back
Top Bottom