Waziri mkuu wa India Narendra Modi anakuja Tanzania: Vitu 7 huenda hukuvijua kuhusu mtu huyu

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,763
5,591
Mods naomba uzi huu usiunganishwe unalengo la kujifunza kutoka kwa maisha binafsi ya jamaa Huyu.

Huyu ni miongoni mwa viongozi waliowahi kuheshimika na wanaoheshimika sana India na duniani. Tuna mengi ya kujifunza kutoka kwake kama taifa.

1:
620-Elec.jpg
Akiwa kiongozi wa jimbo la GUJARAT alifanikiwa kusambaza umeme vijiji vyote. Pili alitenga umeme katika makundi mawili, Umeme wa nyumbani na Umeme wa Kilimo wazo lililoleta mapinduzi ya kilimo jimboni hapo.
2:
48957838.cms

Alifanya mapinduzi ya Kibiashara na kuondoa Urasimu Gujarat na kuifanya Gujarat Kushika namba moja katika WORD BANK EASY TO DO BUSINESS PLACE kwa miaka miwili mfurulizo.

3:
can-modi-change-india.jpg

Akiwa waziri mkuu alibadili sheria Fyongo na zilizopitwa na wakati 1159 ndani ya miaka miwili, wakati serikali zilizkopita zilitumia miaka 64 kubadili sheria 1301 tu. hii imeifanya india kuendelea kwa spidi ya haraka sana.

4:
13mii2.jpg

Aliweka sera za kuvutia uwekezaji wa makampuni kutoka nje, na kukuza kwa 61% . Ndani ya muda mfupi India ikawa ya KWanza Duniani Ikiwapiku US na CHINA kwa kuwa sehemu ambapo wawekezaji wa nje wangependa kuwekeza mitaji.Miezi michache baada ya kuchaguliwa alianzisha kauli mbiu MAKE IT IN INDIA ili india kuwa kitovu cha mapinduzi ya viwanda duniani.

5:
PM_Modi_participates_in_Shramdaan_as_part_of_Swachhta_Abhiyan_at_Assi_Ghat%2C_Varanasi.jpg

Alianzisha mpango wa bima ya afya nchi nzima, na kutoa madawa bure kwa wale wagonjwa waliozidiwa na wasiojiweza kwa gharama za serikali, Lakini alianzisha pia "CLEAN INDIA" program ya usafi nchi nzima.Alianzisha mradi wa kujenga vyoo vijijini na kuhamasisha wahindi kuvitumia.

6:
131.png

Alianzisha DIGITAL INDIA PROGRAM, hii lengo mahususi nikuhakikisha technogia inarahisisha huduma kwa wananchi na kupunguza urasimu mwingi wa paperwork.Akaanzisha Digital India week, Akasafiri hadi SILICON VALLEY marekani na kukutana na wakina Mark Zugerberg, Sundar Pichai etc kuboresha zaidi wazo lake, Leo kila kituo cha treni kunatakiwa kuwa na free wireless internet access.

7: MUONEKANO NA MVUTO DUNAINI
sunday-et-lok-sabha-elections-2014-how-political-parties-like-congress-bjp-aap-and-their-candidates-are-using-and-abusing-social-media-to-woo-voters.jpg

Huyu jamaa ni kiongozi wa pili duniani kuwa followed na watu wengi duniani katika mitandao ya kijamii nyuma ya Obama, Kupitia mitandao ya kijamii anakutana na raia wake wengi na aliwahi kufanya live chat katika Google hangout na raia wa chini kabisa. Mwaka wa kwanza madarakani katika kura za mitandaoni alikuwa approved kwa asilimia 93. 2015 mtandao wa forbies ulimtambua kama mtu wa 9 dunani mwennye Nguvu. Ni Vegetarian na workaholic anayependa kujituma kupita kiasi.

Hapa unaweza kujua Tanzania inatembelewa na kiongozi wa aina gani.
Hapa Rais anafursa ya kujifunza mengi kwa maana ya Maendeleo Halisi.
 
Modi ni kiongozi mwenye maono. Lakini hii haisemi India imeshinda yote. Bado yupo na kazi kubwa kuondoa umaskini uliotapakaa kwa watu wakada ya chini. Nimeona yeye pia ni Vegetarian. Basi naweza sema yeye ni mtu mwenye uelewa mkubwa spiritually. Kuwa vegan/vegetarian inakukumbusha kuthamini maisha, kupenda amani zaidi, kifupi idadi kubwa ya vegan/vegetarian wanaongoza maisha positive sana. Look around you will see. Namwona Prime Minister Modi akifikisha India next level. Viongozi wetu pia wajifunze maisha ya kila siku wanayoishi yanataswiri namana ya siasa wanazofanya. Unakita kiongozi anaongoza maisha ya hovyohovyo kabisa lakini anashangiliwa kisa anajulikana sana au ana dough ndefu.....hatari sana. Modi ameweza kwasababu maisha yake, kazi zake zinaonyesha kweli huyu ni kiongozi sio blah blah na siasa uchwara.
 
Uko sawa, Huyu ni kiongozi ambaye Unajifunza sio tu uongozi bali hata maisha binafsi.
Vegetarian ni uamuzi mkubwa sana katika self control and mastery.
Pia ukipewa jimbo kuwa mfano.
Kama alivyofanya Gujarat, Zhao zhiyang alipopewa jimbo la Sichuan china,
Mapinduzi aliyoyafanya akapewa uwaziri mkuu ili alichokifanya SICHUAN hadi wananchi waliokuwa wanakaribia kuteketea kwa njaa wakawa na msemo "Ukitaka Kula Muangalie Zhiyang" kisambazwe nchi nzima. Japo alifia katika kifungo cha ndani lakni. Histora ya China/Modern china imejificha kwa huyu mtu.
Tuna mengi ya kujifuza kwa watu kama hawa
 
Naona kitendo cha Mh. Raisi wetu kutopenda kusafiri nje ya nchi sasa kinakuwa baraka kwa kupata wageni mara kwa mara.

Ahsante Mh. Raisi wanaotutaka kibiashara wao waje na siyo sisi kwenda kujikomba kwao
Hatuwezi kua na kiongozi wa aina hii chini ya CCM, mtoa mada amesema kua viongozi wote walishindwa kuijenga India mpya chini ya cha cha kihafidhina lakini huyu mzee chini ya upinzani kafanya makubwa sana.
 
Nadhani utendaji kazi wa magufuli umemvutia na kumshawishi aje kutembelea nchini. Kutokana na jitihada za rais magufuli za kupambana na mafisadi, atakuwa amevutiwa na kuja kuwekeza nchini ili kuimarisha mahusiano ya kibiashara baina ya nchi hizi
 
Modi ni kiongozi mwenye maono. Lakini hii haisemi India imeshinda yote. Bado yupo na kazi kubwa kuondoa umaskini uliotapakaa kwa watu wakada ya chini. Nimeona yeye pia ni Vegetarian. Basi naweza sema yeye ni mtu mwenye uelewa mkubwa spiritually. Kuwa vegan/vegetarian inakukumbusha kuthamini maisha, kupenda amani zaidi, kifupi idadi kubwa ya vegan/vegetarian wanaongoza maisha positive sana. Look around you will see. Namwona Prime Minister Modi akifikisha India next level. Viongozi wetu pia wajifunze maisha ya kila siku wanayoishi yanataswiri namana ya siasa wanazofanya. Unakita kiongozi anaongoza maisha ya hovyohovyo kabisa lakini anashangiliwa kisa anajulikana sana au ana dough ndefu.....hatari sana. Modi ameweza kwasababu maisha yake, kazi zake zinaonyesha kweli huyu ni kiongozi sio blah blah na siasa uchwara.
Tatizo la kuchagua kiongozi ambaye hajawahi kuleta mageuzi ktk jmii yake ndio haya yanayo tukuta.
 
Nadhani utendaji kazi wa magufuli umemvutia na kumshawishi aje kutembelea nchini. Kutokana na jitihada za rais magufuli za kupambana na mafisadi, atakuwa amevutiwa na kuja kuwekeza nchini ili kuimarisha mahusiano ya kibiashara baina ya nchi hizi
Sijui itendaji wa mtu hupimwaje, wewe umempima kwa Lipi maana nijuavyo mimi utendaji hupimwa kwa matokeo. Naomba angalao matokeo ya utumbuaji majibu ndugu yangu.
 
Back
Top Bottom