singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (Pichani) anatarajia kuanza ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Ruvuma, ambapo atawasili mkoani hapo leo saa tisa alasiri.
Baada ya Waziri Mkuu kuwasili Uwanja wa Ndege wa Songea, atapokelewa na viongozi wa Chama na Serikali, pia atakwenda Ikulu kupokea taarifa ya maendeleo ya mkoa wa Ruvuma.
Aidha, siku ya jumatatu atakuwa na shughuli za kufungua tawi la Benki ya Posta mjini Songea, kukagua maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula (NFRA) kanda ya Songea na kukagua makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Siku inafuata atatembelea na kukagua Hospitali ya Rufaa ya mkoa, na baadaye kuzungumza na watumishi wa hospitali hiyo.
Siku ya nne ya ziara yaani jumatano, Waziri Mkuu atafanya majumuisho ya ziara mkoani humo, kabla ya kuagana na viongozi wa Chama na Serikali na kurejea Dar es
Salaam.
mjengwablog