Waziri Mkuu Majaliwa: Tunaangalia utaratibu utakaofaa uhifadhi eneo Loliondo

PendoLyimo

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
879
956
Wakuu Kuna blog moja ya Dar ili-tweet leo kwamba suala la Ngorongoro limeisha kumbe PM alikuwa Loliondo na sio Ngorongoro Ila ukweli ndio huo hapo na sio kama walivyo-ripoti.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MAJALIWA: TUNAANGALIA UTARATIBU UTAKAOFAA UHIFADHI ENEO LA LOLIONDO

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali inaangalia utaratibu utakaofaa kuhusu suala la uhifadhi katika eneo la Loliondo lililopo kwenye wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha.

"Katika mjadala wetu wa leo, mmetoa maoni nasi tumeyapokea. Bado Serikali inayaangalia maslahi mapana ya umma. Tutawashirikisha pia ni lipi lina maslahi mapana kwa Watanzania."

Ametoa kauli hiyo leo (Jumatatu, Februari 14, 2022) wakati akizungumza na wadau wa uhifadhi kwenye kikao kilichofanyika Wasso-Loliondo. Amesema Serikali imepokea maoni waliyoyatoa, yatayojumuishwa na kuyawasilishwa kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Pia, Mheshimiwa Majaliwa amesema alichoenda kufanya leo ni utekelezaji wa ushauri uliotolewa na wabunge kwa Serikali kupitia Mwenyekiti wa Kamati wa Maliasili na Utalii iliyoielekeza Serikali iende katika maeneo ya Loliondo, Ngorongoro na Sale na kuzungumza na wananchi.

“Kama ambavyo Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza lazima tuimarishe utalii na kuhakikisha wananchi wanashirikishwa, Waheshimiwa wabunge ambao ndio wawakilishi wametoa maoni yao ikiwemo kushauri suala la ushirikishwaji na ndio maana leo nimekuja hapa kuwasikiliza”.

Waziri Mkuu amesema wote tunatambua kuwa idadi ya watu na mifugo imeongezeka ndani ya hifadhi ambapo tusipotafuta suluhisho la kudumu hifadhi zetu zitaathirika. “Sisi sote tunatambua eneo hili ni la utalii, lazima tufike mahali tuamue kama tunataka utalii au la," amesema.

Waziri Mkuu amesema amefarijika kusikia kwamba wachangiaji wote waliozungumza hakuna aliyesema ardhi ni yao. "Kati ya mambo yamenifariji, sijasikia mtu akisema ardhi yetu, ardhi yetu. Sote tunatambua kuwa ardhi iliyo ndani ya mipaka ya nchi hii ni ya umma lakini tumeikasimu kwa Mheshimiwa Rais kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania."

Katika kikao hicho, wananchi wa makundi mbalimbali walipewa nafasi kutoa maoni yao wakiwemo mbunge, madiwani, malaigwanan, wanamije (batemi) na wenyeviti wa vijiji. Katika maoni yao, wengi wao walisema wako tayari kushirikiana na Serikali kuendelea kutunza rasilimali za Taifa.

Waliomba wapatiwe elimu ya uzazi wa mpango, wapimiwe ardhi za vijiji ili kupunguza migogoro inayojitokeza mara kwa mara. Wilaya ya Ngorongoro ina tarafa tatu za Loliondo, Sale na Ngorongoro.

IMETOLEWA:

OFISI YA WAZIRI MKUU

JUMATATU, FEBRUARI 14, 2022.
 
Hili jambo dogo sana, Bi Mkubwa atalimaliza kiulaini kabisa, maana watu waliokosa sera wanalidandia tu kama majuha fulani. Watanzania ni nambari wani. Wanyama, nyayo za mtu wa kwanza, caldera na upuuzi kama huo haviwezi kuwa na thamani kuliko watanzania wanaoishi kwa sasa. Tusubiri na tuone
 
Wewe naona limewashuka baada ya wamasai kukabaa!!, Acheni kupotosha watu, Kila jamii ikae kwenye asili zao.

Mwambie na huyo Balile wamasai tumekaa kikao tutamtoa BHUSHER sio muda mrefu.
 
Hili jambo dogo sana, Bi Mkubwa atalimaliza kiulaini kabisa, maana watu waliokosa sera wanalidandia tu kama majuha fulani. Watanzania ni nambari wani. Wanyama, nyayo za mtu wa kwanza, caldera na upuuzi kama huo haviwezi kuwa na thamani kuliko watanzania wanaoishi kwa sasa. Tusubiri na tuone
Wamasai wanaondoka......mark my words
 
Wewe naona limewashuka baada ya wamasai kukabaa!!, Acheni kupotosha watu, Kila jamii ikae kwenye asili zao.

Mwambie na huyo Balile wamasai tumekaa kikao tutamtoa BHUSHER sio muda mrefu.
Balile na kitenge wasubili kukojoa dagaa
 
Back
Top Bottom