Waziri Mkuu Majaliwa, akutana na wawekezaji wa Umeme na Gesi toka Japan

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,575



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata ufafanuzi wa mikakati ya uwekezaji kwenye miundombinu ya umeme wa gesi asilia na jua kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya KOYO ya Japan, Bw. Norio Shoji wakati alipokutana na ujembe wa kampuni hiyo ofisini kwake jijini Dar es salaam . (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Viongozi wa Kampuni ya Japan ya KOYO na kampuni ya Kitanzania ya SSF Limited ambazo kwa pamoja zimekusudia kushirikiana ili kuwekeza kwenye miundombinu ya umeme wa gesi asilia na jua nchini. Mazungumzo hayo yalifanyika ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya KOYO ya Japan, Bw. Norio Shoji baada ya kukutana na Mtendaji huyo na ujumbe wake ofisini kwake jijini Dar es salaam May 9, 2016. Kampuni hiyo ikishirikiana na Kampuni ya Kitanzania ya SSF Limited inakusudia kuwekeza kwenye miundombinu ya umeme wa gesi asilia na jua nchini. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kampuni ya Japan ya KOYO na kampuni ya Kitanzania ya SSF Limited ambazo kwa pamoja zimekusudia kushirikiana ili kuwekeza kwenye miundombinu ya umeme wa gesi asilia na jua nchini. Waziri Mkuu alifanya mazungumzo na viongozi hao ofisini kwake jijini Dar es salaam
 
wajapan wana nyukilia ila wanavuna sana umeme wa jua licha ya kuwa na uhapa wa Jua

safi sana watafutwe na wataalam wa umeme wa upepo pia
 
wajapan wana nyukilia ila wanavuna sana umeme wa jua licha ya kuwa na uhapa wa Jua

safi sana watafutwe na wataalam wa umeme wa upepo pia


Unajua tunaweza kuvuna upepo na kutengeneza umeme kutoka baadhi ya mikoa kama iringa,cha muhimu tupate vifaa na wataalamu
 
Safi sana habari ya kuzungumzia umeme kama tatizo tangu nchi ipate uhuru ni aibu, wakae na huyo jamaa wayapange vyema kwani jua lipo la kutosha, gass imebaki historia ya kila uchao.
 
Back
Top Bottom