Waziri mkuu kalidanganya taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri mkuu kalidanganya taifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mundali, Feb 13, 2011.

 1. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #1
  Feb 13, 2011
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Wakati akitoa majibu kuhusu kauli ya serikali juu ya mauaji ya Arusha na uchaguzi wa umeya wa halmashauri ya jiji la Arusha, waziri mkuu hakuwa mkweli juu ya masuala yafuatayo: -

  1. Mauaji hayakufanyika mita hamsini kutoka kituo kikuu cha polisi kama alivyosema, bali mauaji yalitokea katika maeneo matatu tofauti na ilikuwa zaidi ya mita 500 toka kituo kikuu cha polisi.

  2. Uhalali wa uchaguzi haujengwi na idadi ya wafuasi wa wagombea, bali hutokana na taratibu zilizokubaliwa kuendesha uchaguzi huo. Kwamba CCM ilikuwa na wapiga kura 16 hakuhalalishi uchaguzi kufanywa na wanaccm pekee. Pengine pinda kachukulia ushindi wake wa kupigiwa kura na wanaccm pekee na kufanikiwa kuwa mbunge ndio msingi, lakini kimsingi hata yeye sio mbunge wa kuchaguliwa kwa mujibu wa katiba. Anabaki kuwa mbunge wa kuteuliwa na chama chake. Wananchi wa jimbo lake hawakupewa fursa ya kufanya uchaguzi. Kadhalika madiwani wa Arusha hawakupewa fursa ya kuchagua meya wao. Hakukuwa na tofauti ya kikao kilichomteua mgombea wa umeya kwa tiketi ya ccm na kikao kilichomidhinisha. Kikao hicho ni halali tu iwapo waliohudhuria na kupiga kura nitheluthi mbili ya wajumbe au zaidi.

  3. Uhalali wa Mary Chatanda, waziri mkuu kaonyesha udhaifu usiomithilika wa kutetea hata ufunjifu wa katiba wa wazi kabisa. Mary Chatanda ni halali kuingia katika baraza la madiwani Arusha kwa sababu chama chake kimempangia kazi Arusha? Ni Ibara ya ngapi ya katiba inayompa uhalali mbunge wa jimbo A la uchaguzi A kwenda kuwa mwakilishi wa wananchi katika counsel V?
  Kama hiyo ndiyo best practise, anatuambia nini kuhusu mbunge wa Mbulu ambaye mwajiri wake kampangia kituo cha kazi Arusha? Je, mawaziri akiwamo yeye, wanapaswa kuhudhuria vikao vya counsel ilala?

  Pinda, ni kweli kwamba watanzania tumeongoza kwa division 0, lakini si mbumbumbu kiasi hicho. HUJASEMA UKWELI, UMETUDANGANYA.
   
 2. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #2
  Feb 13, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,273
  Trophy Points: 280
  Tangu lini CCM waliwahi kusema ukweli katika chaguzi zote zilizopita??Hivyo pinda kusema uongoyupo katika mazoea yake!
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Feb 13, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  pinda ameripoti kama alivyoambiwa, btw... did you expect him to side with CDM?
   
 4. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #4
  Feb 13, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Pinda ni kondoo wa kafara tu, kuna mengi/wengi nyuma yake. Hata bwana Lema naye ni chambo tu, kuna mengi yataibuka wasipokaa vizuri CCM ya Tunisia na Egypt yataanzia kwa Lema. Kama watamtia hatiani Lema kizembe, yaliyowahi kutokea huko nyuma kama ya Zitto yatakuwa mara kumi. Natamani wamfungie ili tuingie barabarani.
   
 5. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #5
  Feb 13, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  sishangai kwa uongo wa shockupsorber wa mafisadi(pinda)..................
   
Loading...