Waziri Mkuu aweka jiwe la msingi mradi wa barabara ya Kagwira – Karema

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
260
Reaction score
199
WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA BARABARA YA KAGWIRA – KAREMA

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa barabara ya Kagwira – Karema (kilometa 112) katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi.

Mradi huo unatekelezwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kwa gharama ya takribani shilingi bilioni 219.09, ukiwa na lengo la kuboresha miundombinu ya usafiri na kuchochea shughuli za kiuchumi katika ukanda wa Ziwa Tanganyika.

Kwa mujibu wa taarifa ya mradi iliyosomwa na Kaimu Meneja wa Udhibiti wa Miradi TANROADS, Mhandisi Malima Musema Mongo, ujenzi wa barabara hiyo umegawanyika katika vipande viwili ambavyo ni Kagwira – Kasekese (kilometa 54.144) na Kasekese – Ikola – Karema (kilometa 56.911).

Alisema ujenzi wa kipande cha Kagwira – Kasekese unagharimu takribani shilingi bilioni 106.95 na umefikia asilimia 8.2 ya utekelezaji, huku kipande cha Kasekese – Ikola – Karema kikigharimu takribani shilingi bilioni 112.14 na kufikia asilimia 33.4 ya utekelezaji.

Mradi huo ni wa kimkakati kwa kuwa utarahisisha usafirishaji wa mizigo kupitia Bandari ya Karema kwenda nchi jirani ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, pamoja na kupunguza msongamano wa malori ya mizigo katika eneo la Tunduma.

Aidha, barabara hiyo itarahisisha usafirishaji wa mazao kutoka mashambani na kuwaunganisha wananchi na huduma mbalimbali za kijamii kama vile huduma za afya na biashara katika maeneo ya ukanda huo.

Mradi huo unatekelezwa kwa mfumo wa kimkataba na unatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi 26. Hadi sasa utekelezaji wa jumla wa mradi umefikia asilimia 21, ambapo kiasi cha shilingi bilioni 32.37 kimeshapokelewa na kutumika katika hatua mbalimbali za ujenzi.

Kukamilika kwa mradi wa barabara ya Kagwira – Karema kunatarajiwa kuwa kichocheo muhimu cha maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika Mkoa wa Katavi na maeneo jirani kwa kuimarisha usafiri, biashara na mawasiliano katika ukanda wa Ziwa Tanganyika.

IMG-20260313-WA0225.jpg
IMG-20260313-WA0228.jpg
IMG-20260313-WA0226.jpg
IMG-20260313-WA0224.jpg
 
View attachment 3557644View attachment 3557645View attachment 3557646View attachment 3557647
Nikiona Karena nakumbuka mbali sana,miaka hiyo ndio maeneo niliyokuwa nafanyia kazi.Namkumbuka marehemu askifu msakili wa karema,nikienda kirando palikuwa na waarabu wengi akina msafiri morimoro,kulikuwa na kijana mmoja baba yake alikuwa ana basi na lori.Ali mabodi nyie mnamjua kama alinkessy,marehemu ricky mwanamyote.Na stori nyingi mno za huko,kirando,kalya,karema,kasanga port,mpulungu,mvuna,kirando mtakuja
 
Back
Top Bottom