Waziri Mkuu atoa agizo zito kwa wakuu wa mikoa wote nchini

mamayoyo1

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
1,011
1,019


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Disemba 29 amewaagiza wakuu wa mikoa wote nchini wahakikishe wanasimamia ipasavyo ujenzi wa vyumba vya madarasa vikamilike kwa wakati ili wanafunzi wote waliochagulia kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2020 waanze masomo kwa pamoja.


Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha wanafunzi wote wanaanza kusoma kwa pamoja kwa sababu wakipishana muda wa kuanza masomo baadhi yao wanashindwa kufanya vizuri jambo ambalo si sahihi.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2015/2020 kwenye mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Ruangwa.

Jumla ya watahiniwa 933,369 sawa na asilimia 98.55 ya waliosajiliwa walifanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2019 na kati yao watahiniwa 759,737 wamefaulu ambao ni sawa na asilimia 81.50.

Kati yao wasichana ni 395,738 ambao ni sawa na asilimia 80.87 na wavulana ni 363,999 sawa na asilimia 82.20. Mwaka 2018 watahiniwa waliofaulu walikuwa asilimia 77.72, hivyo kuna ongezeko la ufaulu kwa asilimia 3.78.

“Wakuu wa Mikoa hakikisheni vyumba vya madarasa vinakamilika ili wanafunzi wote waliofaulu waanze masomo kwa pamoja. Kitendo cha wanafunzi kupishana kuanza masomo kinawafanya waliochelewa kutofanya vizuri katika mitihani yao.”

Kadhalika, Waziri Mkuu amewasisitiza viongozi hao wahakikishe wanasimamia vizuri elimu kwa watoto wa kike na kuwachukulia hatua watu wote watakaobainika kuwakatisha masomo iwe kwa kuwaoa, kuwaozoesha au kuwapa ujauzito.

Amesema Serikaliimeweka sheria kali ya kumlinda mtoto wa kike lengo ni kumuwezesha amalize masomo yake ili aweze kujikwamua kiuchumi na aondokane na utegemezi, hivyo ni marufuku kuwakatisha masomo.

“Watoto wa kike wanatakiwa kuheshimiwa katika jamii na Serikali itatoa adhabu kali ya kifungo cha miaka 30 jela kwa mtu atakayekatisha elimu ya mtoto wa kike iwe kwa kumuoa au kumpa ujauzito.”

Waziri Mkuu amesema Serikali inataka kuona idadi kubwa ya watoto wa kike wanatimiza malengo yao kielimu, hivyo ni lazima wakaondolewa vishawishi kwa kuboresha mazingira yao ya kujifunzia ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya mabweni.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini ikiwemo na wilaya ya Ruangwa ambayo imepewa sh. bilioni 38 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuupongeza uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Ruangwa kwa kubuni mradi wa kimkakati wa ujenzi wa ghala la kuhifadhia mazao na pembejeo linalojengwa katika kijiji cha Lipande. Ujenzi huo unaogharimu sh bilioni 5.45.

Ghala hilo ambalo limeanza kutumika lina uwezo wa kuhifadhi tani 20,000 litaiwezesha halmashauri kujiongezea mapato ya ndani na kusaidia kupunguza utegemezi kutoka Serikali Kuu na wafadhili. Pia litapunguza gharama za usafirishaji wa korosho walizokuwa wanatozwa wakulima wakati wa kusafirisha mazao.

Amesema katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano miradi mingi ya kimkakati imetekelezwa nchini ambayo ni pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), upanuzi wa bandari za Mtwara, Dar es Salaam na Tanga, uboreshwaji wa viwanja vya ndege, ununuzi wa rada na ununuzi wa ndege mpya.

Waziri Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Tano tangu ilipoingia madarakani mwaka 2015, kipaumbele chake kilikuwa ni kukuza kiwango cha uchumi kutoka cha chini kwenda cha kati ifikapo mwaka 2025 kupitia sekta ya viwanda.
 
Ina maana viongozi hawajui haya mambo? Kila halmashauri ina afisa mipango hawa wanafanya kazi gani kama kila wakati tunafanya mambo kwa mtindo wa zimamoto? Kama taifa tuna tatizo la vipaumbele.
Screenshot_2019-12-29-20-42-45~2.jpeg
Screenshot_2019-12-29-20-43-02~2.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazee wa kuzima moto kama kawaida yetu.

Kana kwamba hatukujua idadi ya wanafunzi wanaotarajia kumaliza mwaka huu ni wangapi, na kati yao wangapi wataendelea na shule.

Namba tunazipenda ila.......

Hapo bado kuna madawati, achilia mbali mambo mengine yahusianayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ina maana viongozi hawajui haya mambo? Kila halmashauri ina afisa mipango hawa wanafanya kazi gani kama kila wakati tunafanya mambo kwa mtindo wa zimamoto? Kama taifa tuna tatizo la vipaumbele. View attachment 1306718View attachment 1306720

Sent using Jamii Forums mobile app

Hili ni tatizo la kukosa vipaumbele kama taifa....

Leo ni tarehe 29/12/2019, shule zinafunguliwa tarehe 06/01/2020....

Utajenga madarasa gani na kwa namna gani hasa katika wiki moja hii?

Inavyoelekea hakuna mipango ya muda mfupi na muda mrefu...!

Na kama ipo, kuna uwezekano hakuna pesa za kutekeleza....

Kuna possibility kubwa kuwa kinachokwenda kufanyika ili haya madarasa yajengwe ni kwenda kutumia mgambo ili kuwaminya wananchi hawa wanaoitwa "wanyonge" kuchangia kwa nguvu....!!
 
Wanawajaza hao watoto huko sekondari kwani wamewaongeza mishahara walimu? Vipi kuhusu kupanda madaraja na madai yao ta nyuma?Kweli hawa ni stupid teachers at the hill.


Walimu endeleeni na mgomo baridi mlio nao,Maana wanaagiza tu hao waliokuwa walimu na Sasa wapo juu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini hapo utashangaa Kuna wakuu wa mikoa Baadhi Wataanza kuwapiga viboko wazazi na walimu Kupitia Hilo agizo.
Nanukuu;
"Uzuri Sisi mkoa wa mbeya tumeanza kutumia bakola kwa kila jambo. Tukikukuta hujaoa na umetimiza umri wa kuoa tutakuchapa bakola au Kama hujaolewa tutakupiga bakola" Rc Chalamila- mbeya.

Kwahiyo wazazi na walimu wa mikoa husika ya wanaotumia bakola kwa kila jambo kuweni makini sana juu ya Hilo agizo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom