Waziri Mkullo afanya kufuru

Good job mwandishi na mchunguzi wa habari hii, haya ndo mambo yanatakiwa wengine igeni kutafuta habari za namna hii.

Keep it up mwandishi.
 
Hizo zipo sana bongo wala hajaanza yeye, kuna mwingine alienda Bukoba kwa ndege hivyo hivyo halafu dereva na mlinzi akafuata kwa gari!
 
Huyo mdee aliliona la waziri wa ccm kuwa ni ubadhirifu, lakini sijamsikia akiongelea ya zitto kabwe aliye kodiwa ndege na mfuko wa pension wa ppf kama shukrani kwa kuzima soo la ufisadi. Bunge hutoa fedha za usafiri kwa kamati zake, ppf wanakodi ndege kumpeleka zitto kabwe bukoba kama nani? Wanachezea fedha zetu wachangiaji huku tukiishia kupewa pension ya shs. 21,000 kwa kwa mwezi. Wizi mtupu.


 
Habari za "kuchakachua" kura zishaanza kuwa boring kwa hiyo zinatafutwa habari zingine kinguvu. Kwani huko Dodoma alienda kwenye kitchen party ya mwanae hata mpige kelele kama wendawazimu?

PUMBAFU!
 
Nauliza. Nikipewa posho. Sehemu ya posho nikalipia tiketi ya ndege au nikiwa nimepewa complimentary ticket ni kufuru kwa dereva wangu kwenda kunisubiri huko ninakoenda? Nauliza tu?
 
Mkullo: Maisha yangu yako hatarini



na Joseph Malembeka, Morogoro




WAZIRI wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, amewashukia watendaji wa ofisi yake kwamba wanahatarisha maisha yake kwa kuvujisha siri za wizara hiyo.

Mkulo alitoa kauli hiyo baada ya gazeti hili hivi karibuni kuripoti kuwa alikodi ndege kwenda Dodoma na kumuagiza dereva wake amfuate kwa shangingi lake aina ya G8.

Waziri huyo alisema hayo jana wakati akifungua mkutano wa baraza la wafanyakazi katika wizara hiyo kwenye ukumbi wa BZ, ulioko nje kidogo ya mji wa Morogoro.

Bila kutaja majina, waziri huyo mwenye dhamana ya fedha, alisema utafiti wake umeonyesha kuwa wavujishaji wakuu wa siri katika wizara yake ni wakurugenzi, makamishina na watendaji wa kati.

Akitoa mfano na kulihusisha gazeti hili, Mkulo alisema umeibuka mtindo wa baadhi ya watumishi hususan makao makuu ya wizara hiyo kutoa siri za ofisi na wizara kwenye vyombo vya habari, kuwachafua mawaziri waonekane wafujaji fedha za umma ili wawajibishwe.

"Hivi karibuni gazeti moja (Tanzania Daima Jumatano), likaamua kufuatilia safari ya waziri na dereva wake toka Dar es Salaam kwenda Dodoma baada ya kukodiwa ndege kwa gharama ya dola 5,000 bila kufanya uchunguzi kwa sababu gani ilifanyika hivyo...lakini ilikuwa imesukwa na baadhi ya watendaji wetu, tena wamo humu ili wamchafue Mkulo," alisema.

Katika hotuba hiyo iliyokuwa fupi lakini iliyorefushwa na ufafanuzi wa taarifa hiyo iliyoonyesha kumkera sana Waziri Mkulo hivyo kumlazimu kutumia zaidi ya dakika 30 kutoa ufafanuzi juu ya mazingira ya kukodiwa ndege hiyo, Mkulo alisema hana mamlaka ya kujiamulia kukodi ndege na kuongeza kuwa tangu awe waziri, amekodiwa ndege mara nane tu.

Mkulo ambaye alionyesha kukerwa sana na taarifa hiyo, alisema wizara iliamua kumkodia ndege hiyo yeye na dereva wake kwenda Dodoma kutokana na majukumu yaliyokuwa yakimkabili likiwemo la kulazimika kukutana na baadhi ya mabalozi na mawaziri wa fedha toka nje ya nchi ambao walikuwa wanaliingizia taifa takriban dola za Kimarekani milioni 100.

"Akaandaliwa mwandishi uwanja wa ndege Dar es Salaam apige picha ndege anayopanda waziri na kule Dodoma akaandaliwa mwandishi kupiga picha ndege atakayoshuka waziri...ni hatari sana; hebu fikiria kama wangekuwa maharamia mimi si nigeuawa kwa dola 5,000 zinazodaiwa nimefuja!?" aliongeza.

Akitahadharisha juu ya kutokuwa na siri katika utumishi hususan serikalini katika wizara nyeti kama hazina ambayo ni roho ya nchi, Mkulo alisema kama hakuna usiri wa nyaraka katika serikali yoyote waelewe kuwa hakutakuwa na utawala.

Alisema nyaraka za serikali sasa zimezagaa mitaani hususan kwenye masoko likiwemo la Kariakoo jijini Dar es Salaam zikitumika katika matumizi yasiyo sahihi kwa wafanyabiashara ndogondogo wakiwemo wauza vitumbua na karanga.

Awali Naibu Waziri wa Fedha, Gregory Teu, akiwasalimia wafanyakazi katika mkutano huo jana alisema mbali na kulitumikia taifa kama mkaguzi na mdhibiti wa mali za serikali amebaini kuwa wizara hiyo inakabiliwa na tatizo la matumizi makubwa kuliko mapato jambo linalosababisha kushindwa kufikia malengo.

Hivi karibuni gazeti hili liliripoti kuwa Waziri Mkulo alikodi ndege kwa fedha za serikali kwenda kuhudhuria mahafari ya Chuo cha Mipango mjini Dodoma, lakini bado aliliagiza gari lake la uwaziri limfuate kutoka jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kulitumia katika mji huo wakati Wizara ya Fedha na Uchumi ina ofisi na magari mjini Dodoma.

Waziri Mkulo mwenye dhamana ya fedha nchini, alikodi ndege ya Shirika la Tanzania Air, yenye namba za usajili 5HTZC na kuwasili katika uwanja wa ndege wa mjini Dodoma, majira ya saa nane mchana.

Wakati Waziri Mkulo akipasua anga la Dodoma kwa ndege ya kukodi, siku hiyo hiyo, dereva wake alilazimika kujaza mafuta shangingi la waziri huyo na kuweka kibindoni posho yake kumfuata bosi wake mjini Dodoma.

Taarifa hiyo ambayo ilimkera sana Waziri Mkulo, ilidai kuwa ndege hiyo ilikodishwa kwa dola za Kimarekani 5,000, sawa na sh milioni 7.5.

MY TAKE
Hapo kwenye nyekundu, sijui mheshimwa Mkulo alitaka kuwaambia nini Watanzania. Sikujua Wizara ya Fedha kuna biashara ya kullingizia taifa mabilioni, Mkulo anataka kusema kuwa kama asingekuwepo nchi isingepata hizo fedha. Na je hiyo inakuwaje excuse ya kukodiwa ndege? kwani alikuwa hajui kuhusu hiyo mikutano na wafadhili, kwani asingeweza kuwakilishwa huko Dodoma? Au Dodoma nako alikuwa anaenda kuliingizia taifa mabilioni? Ningemuelewa kama angekodiwa ndege kuwahi mikutano na wafadhili, but not other way round!!! Nimekuwa confused na the whole episode na sijui Mkulo anataka kusema nini, loh
 
 
hii kali...watoto wanakaa chini in classes yeye anasema dola 5000 tu kama vile it is same as nothing....
 
Huo uharaka pekee unaonyesha jinsi gani watu wa serikali wasivyoweza kujipanga kutokana na priority zilizopo. Kila mtu anatumia fedha bila kujua athari zake kesho na bado wanasema eti nao wamesoma.Huko ndio kusomea nini? Kuubomoa uchumi?
 
Yaani Mbaha, hizo fedha ni sawa na Mishahara ya Walimu 30 kwa hesabu za haraka haraka. Shule ngapi zina mwalimu mmoja na hata hakuna madawati na mwalimu mwenyewe huyo mmoja hana motisha wowote?.Tunajenga Taifa au tunaandaa "Time Bomb" litakalolipuka huko mbeleni. Ninavyofahamu Mabalozi wa nje na other Diplomats huwa wana ratiba zao tena very systematic. There is no way kwamba Waziri alikurupushwa na hakuja hicho kikao. This is not an excuse Mhishimiwa Waziri.Awajibke :kev: :A S-fire1:
 
Huo uharaka pekee unaonyesha jinsi gani watu wa serikali wasivyoweza kujipanga kutokana na priority zilizopo. Kila mtu anatumia fedha bila kujua athari zake kesho na bado wanasema eti nao wamesoma.Huko ndio kusomea nini? Kuubomoa uchumi?
Kazi ipo , yawezekana mhe. hakujua kilichokuwa kinaendelea , RA aliconclude deal ikatakiwa sahihi ya waziri akaitishwa mara moja kwa misingi ya kutopoteza USD Mil 100 , hapa sijui kama yeye na wataalam wake walisoma Masharti yanayoambatana na hiyo USD Mil. 100 ; baada ya muda ni maumivu kwa walipa kodi.
 
mkulo ni mpumbafffffff kabisa,yeye anaona kwa vile alikuwa anaenda kuliingizia taifa dola mil 100 basi dola 5000 is nothing, shame on u mkulo!!!!!! na uyo dereva kukufata huko dodoma ni ni si wiziii huo??????????
 
watu wa Mlingotini huwa hawakosi vijisababu! si bure akaenda Mlingotini kumtafuta mbaya wake! Hivi si niliskia Precisionair inaenda Dodoma au mawaziri hawaruhusiwi kutembelea public flights?
 
huyu Mkullo ni ****...si mnakumbuka ishu yake ya bajeti mbili na kutaka kusawazisha ishu kimya kimya!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…