Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 757
- 1,822
Zaidi ya wafanyakazi 85 wa chuo kikuu cha Mount Meru kilichopo Mkoani Arusha,wakiwemo wakufunzi wa chuo hicho wameandamana wakiwa na mabango kwa waziri wa nchi ofisi ya waziri Mkuu,Sera bunge afya na ulemavu,Jenister Mhagama wakilalamikia malimbikizo ya mishahara yao ya zaidi ya Miezi 10 yenye thamani ya sh, Bilioni 1.
Wakizungumza mbele ya waziri Mhagama aliyekuwa ziarani jijini Arusha katika ufunguzi wa kongamano la maendeleo ya jamii wametoa kilio chao kwa kudai kuwa suala lao limeshindwa kutatuliwa katika ngazi mbalimbali walizopitia.
Wamedai kuwa wamewasilisha malalamiko katika ngazi mbalimbali za serikali lakini mpaka sasa hawajapata ufumbuzi wa staiki zao kwa kuwa hata mwajiri wao hawamfahamu .
Waliongeza kuwa mpaka kufikia Siku ya Jana waliamuriwa kuondoka chuoni hapo baada ya kuletewa askari wa kutuliza ghasia na kulazimishwa kwenda likizo ya miezi sita bila malipo jambo ambalo walilipinga huku wakiwa na hofu ya kupoteza staiki zao
Akiongea kwa niaba ya wafanyakazi hao mbele ya waziri Mhagama,mwenyekiti wa wafanyakazi hao,Michael Sambu alisema kuwa wamefikia hatua ya kuandamana kwa waziri kama sehemu ya kusaka msaada wa kutatua kero hiyo baada ya ngazi mbalimbali za wilaya pamoja na mkoa kushindwa kutatua huku wakishindwa kutatua majukumu ya kifamilia kutokana na ukata wa fedha.
Amemuomba waziri Mhagama kutatua mgogoro wao na chuo kwa kuwa mpaka sasa hawajui mwajiri wao halisi ili waweze kupata staiki zao wanazostaili kuzipata kama wafanyakazi wa chuo hicho.
"Suala la umiliki wa hiki chuo bado linamkanganyiko mkubwa hatujui ila sisi tunachokitaka kwa sasa ni haki yetu watoto wetu huko majumbani wanateseka sana" aliongeza
Kwa upande wake waziri Mhagama akiongea na wafanyakazi hao aliagiza tume kutoka katika wizara yake ije kesho (Jumatano) kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Arumeru ili kuja kutatua changamoto hiyo na kisha wafanyakazi hao kupata haki zao
Waziri Mhagama alilazimika kupiga simu kwa Kamishina wa kazi toka makao makuu na kumpa maagizo ya kuleta tume chuoni hapo haraka itakayoshirikiana na uongozi wa chuo hicho na ofisi ya Mkuu wa wilaya ili kutafuta ufumbuzi wa masuala ya staiki za wafanyakazi hao.
Mgogoro huo umeanza Mara baada ya chuo hicho kikuu cha mt Meru kusitishiwa udahili wa wanafunzi jambo ambalo lililopelekea kuibuka kwa mgogoro mingi kwani hadi sasa wafanyakazi 87 hawajalipwa staiki zao kwa miezi 10.
Ends.....
[https://lh3]