Waziri Mbarawa atoa mwezi mmoja Data Centre ianze kufanya kazi

Queen V

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
775
1,332
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ametoa mwezi mmoja kwa Katibu Mkuu wa Wizara anayeshughulikia Sekta ya Mawasiliano na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu nchini (TTCL), kuhakikisha kituo cha kutunzia taarifa (Data Centre) kilichopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam kinaanza kufanya kazi.

Prof. Mbarawa ametoa agizo hilo kufuatia kukamilika kwa Data Centre hiyo miezi kadhaa iliyopita na mahitaji ya wadau wa huduma ya kutunza kumbukumbu za taasisi zao katika kituo hicho kuongezeka.

“Katibu Mkuu wa Sekta ya Mawasiliano na Mtendaji mkuu wa TTCL hakikisheni kituo hiki kilichojengwa kwa gharama kubwa kinaanza kutumika na kuwezesha mashirika na taasisi mbalimbali kutunza kumbukumbu zao na kuiletea Serikali mapato”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa amesema huduma ya mtandao katika kituo cha Data Centre imeimarishwa kutokana na kuunganishwa na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano hivyo itawarahisishia wateja wake kuweka na kuchukua taarifa zao kwa haraka.

Akizungumza mara baada ya kukagua maeneo mbalimbali unapopita Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano Prof. Mbarawa amemtaka Mkurugenzi wa TTCL kanda ya Kaskazini Bw. Peter Lusama kuhakikisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano unapitishwa juu ya nyaya katika maeneo yenye changamoto za mafuriko ili kuepuka uharibifu wa mara kwa mara na usumbufu kwa watumiaji.

Aidha amezitaka taasisi za Serikali na binafsi kukitumia kituo cha kisasa cha kuhifadhi taarifa DATA CENTRE kutunza taarifa zao ili kuzihakikishia usalama na uhakika wa kuzitumia wakati wote, ambapo asilimia 75 imetengwa kwa ajili ya kutunza taarifa kutoka sekta binafsi na 25 itatunza taarifa za Serikali.

Kituo hicho ambacho ni cha kwanza kujengwa katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ni fursa mpya kwa wafanyabiashara na wadau mbalimbali wenye taarifa nyingi kuzihifadhi na kuzitumia wanapozihitaji kinamilikiwa na Serikali na ujenzi wake umegharimu takribani dola za kimarekani milioni 93.

Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa amekagua uwanja wa ndege wa Singida na mahali utakapojengwa uwanja mpya na kusisitiza umuhimu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini kusimamia kikamilifu ujenzi wa uwanja wa ndege wa sasa ambao upembuzi yakinifu wake umekamilika.

Amesema tayari Serikali imebainisha viwanja 11 vya ndege nchini kote na kuvifanyia upembuzi yakinifu kabla ya kuanza kuvijenga ili viweze kukidhi mahitaji ya soko.

Amevitaja viwanja hivyo kuwa ni Lake Manyara, Musoma, Iringa, Tanga, Songea, Kilwa Masoko, Lindi, Moshi, Njombe, Simiyu na Singida ambavyo vitapanuliwa na kujengwa kwa kiwango cha lami.

sin8.jpg
 
Wasambaze mkonga wa taifa hadi majumbani.

Tuunganishe kama umeme, tunalipia kwa luku.
 
Sijaelewa please wataalam iyo data centre ina umuhimu gani kwa mustakabali wa Tanzania?
 
Sijaelewa please wataalam iyo data centre ina umuhimu gani kwa mustakabali wa Tanzania?
Ni chanzo cha mapato kwa serikali (TTCL) ma ukienda kuweka pale servers zako unalipia kwa mwezi! Mfano rack 1 ni 1,000$ kwa mwezi....sasa kama banks wanakuwag nazo hadi rack 10 kwenda juu....pale inakuw kama back up au distater recovery ya HQ servers! Ni clean money haina ubishi.....! Business nzuri san hiyo! Ila waliopewa wamelala!!
 
Ni chanzo cha mapato kwa serikali (TTCL) ma ukienda kuweka pale servers zako unalipia kwa mwezi! Mfano rack 1 ni 1,000$ kwa mwezi....sasa kama banks wanakuwag nazo hadi rack 10 kwenda juu....pale inakuw kama back up au distater recovery ya HQ servers! Ni clean money haina ubishi.....! Business nzuri san hiyo! Ila waliopewa wamelala!!
Ok nimekuelewa ila wametengeneza kwa pesa nyingi sana,return yake itarudi kweli kwa mfumo wa kifisadi?
 
Ok nimekuelewa ila wametengeneza kwa pesa nyingi sana,return yake itarudi kweli kwa mfumo wa kifisadi?
Msaada wa serikali ya china! Watarudisha mi 15 hivi ila itakaa sana zaidi ya miaka 50 huko!! Zinarudi faster tu......inabidi waijaze tu banks zote zikiweka hapo mbona hela 5yrs imerudi mkuu!!!
 
Back
Top Bottom