Waziri Mansour ataka Serikali 3, asema 2 ni butu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Mansour ataka Serikali 3, asema 2 ni butu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by abdulahsaf, Jul 12, 2011.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [h=1][/h]Written by zenjiboy // 12/07/2011 // Habari // 3 Comments

  Na Juma Mohammed,
  MAELEZO Zanzibar
  Waziri wa Kilimo na Maliasili wa Zanzibar, Mh. Mansoor Yussuf Himid amesema mfumo wa muundo wa Serikali mbili kwa sasa ni butu. Amependekeza kuwepo kwa muundo wa Serikali tatu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  Akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ardhi, Makaazi Maji na Nishati leo katika Baraza la Wawakilishi, Waziri Mansoor alisema umefika wakati kufikiria Serikali tatu kwa maslahi ya Wananchi wote.
  “Mheshimiwa Spika, mfumo wa Serikali mbili ni butu na haufai…sasa basi twende katika Serikali tatu” Alisema Waziri Mansoor.
  Alisema katika dunia ya leo ni ile yenye kusikiliza maoni ya umma, hivyo tabia ya vitisho dhidi ya watu wanaotoa maoni haina nafasi kabisa, matamshi hayo yanaonekana kama kujibu maelezo yaliyotolewa na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta Bungeni aliyesema kwamba hoja ya Serikali tatu ni kutaka kuua Muungano.
  Akichangia mjadala huo Sitta alisema siku ambayo Watanzania wataamua kuwa na serikali tatu za muungano, itakuwa ndiyo tiketi ya kuuvunja muungano huo.
  “Kuunda tena Tanganyika ni kutengeneza mbia mwingine atakayekuwa anashindana na Zanzibar,” alisema Sitta.
  Alifafanua kuwa hali hiyo itajenga mazingira ya mvutano kwa serikali ya Tanganyika na Zanzibar wa kila mmoja kupigania maslahi yake na Serikali ya Muungano haitakuwa na nguvu kwa sababu uwepo wake utategemea pande hizo mbili.
  “Mimi simtaji mtu,lakini inaonekana fikra zao ni za zamani kutisha tisha watu, yale maneno ni ya kupotosha zipo sheria za kimataifa kuhusu Territory Water na matumizi ya rasilimali, mambo ya mipaka yameelezwa sana” Alisema Waziri Mansoor.
  Alisema marekebisho ya Katiba ya Muungano kwa Wazanzibari maana yake ni kujadili Articles of Union na ni vyema tuwaelimishe wananchi wetu wakati ukifika waweze kuitumia vyema fursa hiyo.
  Waziri huyo alisisitza msimamo wake kwamba mafuta na gesi asilia sio suala la Muungano na ni lazima yakabakia kwa maslahi ya Wazanzibari.
  “Makubaliano yetu ni kuyatoa mafuta na gesi asilia katika orodha ya mambo ya Muungano” Alisisitiza Waziri huyo na kuongeza kwamba kuzungumzia mafuta na gesi kuwa ya Muungano ni dhambi kubwa.
  Kauli ya Waziri huyo inakubaliana na hoja iliyowahi kutolewa na kundi la Wabunge 55 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania maarufu kwa jina la “G 55” lilipotaka kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika mwaka 1993.
  Hoja hiyo ilizimwa na marehemu Mwalimu Julius Nyerere ambaye mbali ya kuwatuhumu Waziri Mkuu na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi kwa wakati ule, Holice Kolimba na John Samwel Malecela kwa kumshauri vibaya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi.
  Kutokana na suala hilo, Rais Mwinyi alivunja Baraza la Mawaziri na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Kolimba alihojiwa na Chama chake.
  Hadi sasa msimamo wa CCM katika muundo wa Muungano ni kuwa na Serikali mbili ambazo mara kadhaa zimekuwa ikitetea msimamo huo katika mijadala mbalimbali.
  Chanzo: Blogu ya Jamii (Issa Michuzi)
   

  Attached Files:

 2. J

  JokaKuu Platinum Member

  #2
  Jul 12, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,152
  Trophy Points: 280
  ..maana yake nini?

  ..baada ya kufurumusha matusi wakati ule sasa anabembeleza muungano uendelee??!!

  ..what if wa-Tanganyika hatutaki hizo serikali 3?
   
 3. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Msimamo wa Waziri Mansour haujabadilika na hajawahi kubembeleza kitu.

  Hio ndio option iliobaki ukiondoa kuvunja kabisa.

  So Tanganyikans take the Minister's proposal or let the "union" die.
   
 4. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #4
  Jul 12, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Waziri ana mawazo kama ya Wzbar wengi, yaani umimi zaidi hoja na data haba. Maongezi ya maskani.
  Makaimati na Takashi tunajadiliana hili jambo kila siku. Inapofika mahali mnaulizwa maswali huwa mnakimbia kama thread ya jana.

  Sasa tuambieni, hiyo serikali 3 nani tagharamia seriklai ya shirikisho? na Fees zitalipwaje? Serikali itaendeshwajwe.
  hakuna kubebana wekeni data hapa. Kiwango cha elimu cha huyu waziri kinatisha, halafu ni waziri!! Zbar for Zbaris

  Hakuna option kwa bara! option ipo kwa Zbar! bara ana lose nini?
   
 5. J

  JokaKuu Platinum Member

  #5
  Jul 12, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,152
  Trophy Points: 280
  Makaimati,

  ..hebu mtueleze basi mipaka ya mamlaka ya hizo serikali 3 zinazokuwa proposed.

  ..serikali 3 ili Zanzibar iendelee kupata umeme wa bure na wabunge wao waendelee kula posho Dodoma wakati hawachangii kitu.
   
 6. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #6
  Jul 12, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Kwamtazamo wangu jamaa yuko sahihi kuhusu serikali3.kama itashindikana hili la serikali tatu basi ije moja ya ukweli na si ya kisanii,yaani serikali ya tanzania then katiba ya zanzibar ibadilishwe pamoja na ya muungano tupate katiba moja ya tanzania na mikoa ifutwe tuweke mfumo wa majimbo na pemba na unguja yawe miongoni mwa hayo majimbo.tukianza na majimbo 30 yanatosha then nafasi za umbea kama ukuu wa mikoa na wilaya zifutwe pesa zitumike kuijenga tanzania ya kweli mpya.mawazo yangu tu.
   
 7. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #7
  Jul 14, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Mkuu Joka kuu, ukishaulizi kitu chenye lojiki wanakimbia halafu baada ya wiki 2 wanarudi na madai yale yale.
  Siku zote huwa nasema Wzbar wanafundishwa vitu vya kusema, ukweli hawajui undani wa kile wanachokisema na wakibanwa huwa hawana majibu. Ni mara 4 nimeuliza serikali 3 wanazotaka zitagharamiwa je na zitaendeshwaje? Wanakimbia.

  Wamefundishwa mambo ya muungano ni 11 na yameongezwa hadi 22 na Bara, wasichokijua ni kuwa yapo waliyoomba kama elimu ya juu ambayo hayakuwa katika mambo 11. Na katika mambo 11 yaliyoongezwa ni pamoja na yale yaliyotokana na kuvunjika kwa EA 1977. Hawakuwa na shirika la posta kwa mfano na mzigo huo ulibebwa na Mtanganyika.

  Umimi na ubinafsi ni mambo yanayowatawala wenzetu, hawaongelei gharama za elimu ya juu, au umeme wa bure, au gharama za ujenzi wa umeme baharini ni deni linalolipwa na mtu wa mpwapwa asiyejua hiyo Zbar ipo wapi. Wao wanachojua ni mafuata yasiwe ya muungano(umimi) bila kujiuliza ajira na elimu ya juu mbona hawaongelei?

  Wzbar wanadai eti idadi ya mawaziri iwe sawa!! ukiwauliza wanachangia nini katika hilo baraza na serikali hawajibu wanakimbia.
  Sasa wanafundishwa kuwa pwani ya Afrika mashariki ni sehemu yao kwasababu sultan aliitwala na kuna watu wenye nywele za kiarabu.myth!

  Wamefikia mahali pa kuwakana akina Jumbe, Mwinyi kwasababu wana nywele za kipilipili, Jamani!!!
  Wanasema mapinduzi ni fitna za Nyerere, lakini tarehe 12 kila mwaka wapo mitaani wanasherehekea mapinduzi!!! wimbo wasioujua lakini wanauimba kwasababu wamefundishwa na mzee mmoja wanayemwamini hata kama hajui kuandika jina lake.

  Jibuni hoja, serikali 3 ziendeshweje na zihudumiwe na nani? Kwanini hamuachi biashara na ajira mkarudi kuijenga Zbar yenye neema?
  Umiliki wa ardhi ni mambo ya muungano? Elimu ya juu ni mambo ya muungano? Mnachangia nini katika muungano? Mnashindwa nini kuondoka na kuvunja muungano! Mnataka mawaziri, yupi wa bara aliyeko baraza la mawaziri? Wabunge wenu walioko Dodoma wanalipwa na kodi ya nani? n.k Acheni kupewa tution za maskani bila kuuliza maswali, mnajidhalilisha!!!!

  Wakati mataifa duniani yanaungana, wenzetu wanafikiria kuwa sehemu ya sultan na kuwa nywele nzuri.
   
Loading...