Waziri Makamba acha kuhadaa watu

13 Januari 2021
Itipula, Makete
Njombe Tanzania

TAZAMA MRADI WA BWAWA LA UMEME LITAKALOJENGWA MTO RUHUJI NJOMBE.


Timu ya Watalaamu wa Serikali inayoongozwa na naibu katibu mkuu wizara ya Nishati injinia Leonard Masanja imefika na kufanya ukaguzi wa kwanza katika maporomoko ya mto Ruhuji katika kijiji cha Itipula mkoani Njombe ambao unatarajiwa kujengwa mradi mkubwa wa umeme utakaogharimu dola mil 500 za kimarekani ukiwa na uwezo wa kuzalisha megawats 358 za umeme.

Mradi huo ambao utajengwa katika kipindi cha miezi 36 unaotarajiwa kuanza mwezi juni au julai mwaka huu ulifanyiwa utafiti kwa mara ya kwanza 1998 na kisha kusimama kwa muda mrefu jambo ambalo lilisababisha wananchi kupoteza matumaini na kuanza kurudi kwenye maeneo waliotakiwa kupisha.

Source : Kayuni Online TV
 
Mungu akubariki sana ndugu bagamoyo .
Sijui kwa nini JF hawakupi tuzo.
Sijui kwa nini serikali ya JMT haikupi tuzo.
Umekuwa msaada mkubwa sana kwa wana JF kwa kuweka taarifa sahihi kutoka vyanzo sahihi.
Hakika wewe ni mzalendo.
Kongole sana kwako.
 
Unakufahamu Makete kwanza au unaropoka tuu?
Ni halali 6.9tr izidi kwenye gharama za ujenzi wa bwawa kuubwa kabisa La JKHP?

Ili kulingana Mw zinazopatikana katk bwawa la JKHP na bwawa La mumeo, mabwawa 9 zaidi ya aina hiyo yanapaswa kujengwa, na ikiwa ni hivyo, gharama za vijibwawa hivyo vya mumeo, vitagharimu kodi za watanzania 13+tr, hiyo ni sawa!?
 
Mradi wa kawaida sana kuliko wa Rufiji, swali langu kwa nini mleta mada Kala ban?
 
Kelele zetu za chura(mitandoni) haziwazuii tembo(mafisadi) kunywa maji (kutuibia)
 
Hujajibu swali langu..

Swali jingine kwani Makamba ndio anatengeneza estimates?

Mwisho niletee bajeti za Wizara ya Nishati na madini za 2018 hadi 2020 kabla ya Makamba kuwa Waziri uone gharama za mradi maana msijifanye ni mradi mpya..
 
Hili litajengwa hapo Pembezoni mwa Mji wa Njombe,linalozungumzwa ni Rumakali ambako ni Makete ndani huko milimani.
 
Yaani hakuna hata 100 iliwahi tolewa Wala fidia iliyowahi kulipwa..

Serikali ya waongo ilikuwa ina upuuzi mwingi sana..

Ndio kwaanza fidia zinaanza kulipwa mwaka huu.
 
Kama kawaida Magu.
 
Doto Biteko ameanza kukuumbua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…