Waziri Makamba acha kuhadaa watu

Waziri Makamba acha kuhadaa watu

13 Januari 2021
Itipula, Makete
Njombe Tanzania

TAZAMA MRADI WA BWAWA LA UMEME LITAKALOJENGWA MTO RUHUJI NJOMBE.



Timu ya Watalaamu wa Serikali inayoongozwa na naibu katibu mkuu wizara ya Nishati injinia Leonard Masanja imefika na kufanya ukaguzi wa kwanza katika maporomoko ya mto Ruhuji katika kijiji cha Itipula mkoani Njombe ambao unatarajiwa kujengwa mradi mkubwa wa umeme utakaogharimu dola mil 500 za kimarekani ukiwa na uwezo wa kuzalisha megawats 358 za umeme.

Mradi huo ambao utajengwa katika kipindi cha miezi 36 unaotarajiwa kuanza mwezi juni au julai mwaka huu ulifanyiwa utafiti kwa mara ya kwanza 1998 na kisha kusimama kwa muda mrefu jambo ambalo lilisababisha wananchi kupoteza matumaini na kuanza kurudi kwenye maeneo waliotakiwa kupisha.

Source : Kayuni Online TV
 
Mungu akubariki sana ndugu bagamoyo .
Sijui kwa nini JF hawakupi tuzo.
Sijui kwa nini serikali ya JMT haikupi tuzo.
Umekuwa msaada mkubwa sana kwa wana JF kwa kuweka taarifa sahihi kutoka vyanzo sahihi.
Hakika wewe ni mzalendo.
Kongole sana kwako.
 
Unakufahamu Makete kwanza au unaropoka tuu?
Ni halali 6.9tr izidi kwenye gharama za ujenzi wa bwawa kuubwa kabisa La JKHP?

Ili kulingana Mw zinazopatikana katk bwawa la JKHP na bwawa La mumeo, mabwawa 9 zaidi ya aina hiyo yanapaswa kujengwa, na ikiwa ni hivyo, gharama za vijibwawa hivyo vya mumeo, vitagharimu kodi za watanzania 13+tr, hiyo ni sawa!?
 
Mradi wa kawaida sana kuliko wa Rufiji, swali langu kwa nini mleta mada Kala ban?
 
Kelele zetu za chura(mitandoni) haziwazuii tembo(mafisadi) kunywa maji (kutuibia)
 
Ni halali 6.9tr izidi kwenye gharama za ujenzi wa bwawa kuubwa kabisa La JKHP?

Ili kulingana Mw zinazopatikana katk bwawa la JKHP na bwawa La mumeo, mabwawa 9 zaidi ya aina hiyo yanapaswa kujengwa, na ikiwa ni hivyo, gharama za vijibwawa hivyo vya mumeo, vitagharimu kodi za watanzania 13+tr, hiyo ni sawa!?
Hujajibu swali langu..

Swali jingine kwani Makamba ndio anatengeneza estimates?

Mwisho niletee bajeti za Wizara ya Nishati na madini za 2018 hadi 2020 kabla ya Makamba kuwa Waziri uone gharama za mradi maana msijifanye ni mradi mpya..
 
13 Januari 2021
Itipula, Makete
Njombe Tanzania

TAZAMA MRADI WA BWAWA LA UMEME LITAKALOJENGWA MTO RUHUJI NJOMBE.



Timu ya Watalaamu wa Serikali inayoongozwa na naibu katibu mkuu wizara ya Nishati injinia Leonard Masanja imefika na kufanya ukaguzi wa kwanza katika maporomoko ya mto Ruhuji katika kijiji cha Itipula mkoani Njombe ambao unatarajiwa kujengwa mradi mkubwa wa umeme utakaogharimu dola mil 500 za kimarekani ukiwa na uwezo wa kuzalisha megawats 358 za umeme.

Mradi huo ambao utajengwa katika kipindi cha miezi 36 unaotarajiwa kuanza mwezi juni au julai mwaka huu ulifanyiwa utafiti kwa mara ya kwanza 1998 na kisha kusimama kwa muda mrefu jambo ambalo lilisababisha wananchi kupoteza matumaini na kuanza kurudi kwenye maeneo waliotakiwa kupisha.

Source : Kayuni Online TV

Hili litajengwa hapo Pembezoni mwa Mji wa Njombe,linalozungumzwa ni Rumakali ambako ni Makete ndani huko milimani.
 
TOKA MAKTABA:

31 January 2021

Utekelezaji miradi ya umeme mto Rumakali na Ruhudji, umefika patamu waziri wa nishati afika eneo la mradi

,JANUARY 31, 2021

Na Amiri Kilagalila,Njombe
Katika kutekeleza azma ya serikali ya kuhakikisha upatikanaji umeme nchini unakuwa wa uhakika na kuwapunguzia wananchi mzigo wa ghalama za umeme pamoja na kukuza uchumi wa viwanda, serikali imeendelea kutenga fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbali ya kuzalisha umeme.

Miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na mradi wa Rumakali uliopo wilayani makete utakaozalisha megawati 222 pamoja na mradi wa Ruhudji uliopo mjini Njombe utakaozalisha megawati 358 na kufanya onezeko kubwa la nishati ya umeme huku mkoa wa Njombe ukiwa ni wa kimkakati huku ukiwa ni mkoa wa pili kwa uzalishaji mkubwa wa nishati ya umeme.

Waziri wa nishati Dkt. Medard Kalemani amebainisha hayo januari 30, 2021 alipofika mkoani Njombe pamoja na kutembelea eneo la maporomoka yam to Rumakali uliopo kata ya Kipagalo wilayani Makete na kubainisha kuwa mradi huo utakaozalisha 222 MW ,tayari utekelezaji umeanza na serikali imeshatoa shilingi bilioni 899 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi.

Dr. Medard Kalemani amefafanua kuwa msukumo wanaoweke katika utekelezaji wa miradi ya kuzalisha umeme ni kwasababu uzalishaji wake ni wa ghalama nafuu na kupelekea wananchi kupata bila changamoto kubwa ukilinganisha na aina nyingine ya umeme.

“Uzalishaji wa umeme kwa maji ni ghalama nafuu kulinganisha na vyanzo vingine, kuzalisha umeme kwa maji Unit moja inaghalimu kiasi cha sh.36 tu huku vyanzo vingine ni zaidi ya sh.103 na kuendelea.

Mradi wa Mwl. Julius Nyerere utakapokamilika utawapunguzia wananchi mzigo wa bei za umeme na bei zitashuka sana”alisema Kalemani
Aliongeza “Utekelezaji wa mradi wa Rumakali na Ruhudji umekwishaanza,timu ya kutekeleza mradi huu imeshaundwa na kimsingi timu hiyo imenza na shughuli za matayarisho ya kuanza miradi tajwa na kufika Julai 02, 2021 ujenzi rasmi wa miaradi ya Rumakali na Ruhudji utaanza” aliongeza Dr. Medard Kalemani
Mbali na hayo amesema katika mradi wa Rumakali kitajengwa kituo cha kupokea umeme na utasafirishwa hadi Mwakibeta jijini Mbeya umbali wa kilomita 150 na vijiji vyote vitakavyopitiwa na njia ya kusafirisha umeme vitapatiwa nishati hiyo.

Aidha amesema bado mikakati ya ukamilishwaji wa kazi ya kupeleka umeme vijijini unaendelea na taratibu zote za kufikisha umeme vilivyosalia nchini zimekamilika ambapo februari 05 mwaka huu 2021 wakandarasi wataanza kuingia kazini ili kukamilisha vijiji vilivyosalia ndani ya miezi 18 kwa kuwa tayari serikali imeshatoa shilingi bilioni 851 kwa ajili ya kazi hiyo huku akiwataka wananchi ambao ambao bado vijiji vyao havijapatiwa huduma kuwa wavumilivu.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa Rumakali, meneja uendelezaji wa vyanzo vya umeme kutoka shirika la umeme Tanzania (TANESCO) mhandisi Toto Zedekia amesema, wamejiridhisha baada ya kufanya utafiti na tathmini ya kina kuwa maporomoko ya mto Rumakali una maji mengi na yakutosha kuzalisha umeme.
“Tumejiridhisha vya kutosha mto huu una maji mengi na kutosha kwa kuwa una mita za ujazo 13 kwa sekunde” na kuongeza kuwa
“Litajengwa bwawa lenye urefu wa mita 870 kutoka kingo moja kwenda nyingine na urefu wa kwenda juu utakuwa ni mita 70 na litakapokamilika litakuwa na uwezo wa kuhifadhi maji ya kutosha”

Awali akitoa taarifa ya hali ya upatikanaji wa umeme mkoani Njombe, kaimu meneja wa kanda ya Nyanda za juu kusini Maghalib Mhandisi Yusuph Salim amesema, hali ya umeme mkoani humo imeimarika zaidi tofauti na miaka ya nyuma na hali hiyo imechangiwa na kukamiilika kwa mradi wa Makambako hadi Songea.

Aidha mhandisi Yusuph amesema upatikanaji wa umeme mijini na vijijini ni wa uhakika na kupitia miradi ya umeme vijijini (REA),takribani vijiji 293 vya mkoa wa Njombe vimefikiwa na huduma ya nishati huku vikisalia 88 ambavyo vyote vimeingizwa katika mradi wa REA awamu ya tatu mzunguko wa pili huku 90% ya miradi ya REA ikiwa imekamilika.

Baadhi ya wananchi wa kata ya kipagalo wamefurahishwa kuona mwanga wa kuanza kwa mradi wa umeme katika mto Rumakali kwa kuwa wamekuwa wakisubiri tangu miaka 40 iliyopita huku wakiamini kupta fursa za kiuchumi mradi huo utakapoanza rasmi.

Katika ziara hiyo waziri wa nishati Dkt. Medard Kalemani ameongozana na maafisa waandamizi kutoka wizara ya nishati na shirika la umeme Tanzania (TANESCO).

Waziri Kalemani akielekea eneo la mradi wa umeme unaozalishwa katika mto Rumakali uliopo wilayani Makete kata ya Kipagalo.

Waziri wa nishati Dkt,Kalemani akizungumza na baadhi ya wataalmu alipopokelewa katika ofisi ya mkoa wa Njombe iliyopo mjini mjini humo alipofika kwa ajili ya kukagua mradi.

Mhandisi Yusuph Salim akitoa taarifa ya upatikanaji umeme kwa mkoa wa Njombe pamoja na utekelezaji wa miradi ya REA mkoani humo.
Source : Utekelezaji miradi ya umeme mto Rumakali na Ruhudji,umefika patamu waziri wa nishati afika eneo la mradi
Yaani hakuna hata 100 iliwahi tolewa Wala fidia iliyowahi kulipwa..

Serikali ya waongo ilikuwa ina upuuzi mwingi sana..

Ndio kwaanza fidia zinaanza kulipwa mwaka huu.
 

TOKA MAKTABA:​

12 January 2021


Mradi wa Umeme Ruhudji, Maandalizi ya Miundombinu Wezeshi Yaanza​







Maandalizi ya Miundombinu wezeshi kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Ruhudji Mw 358 yameanza rasmi.

Akiwa katika ziara ya kukagua mahitaji ya ujenzi wa miundombinu wezeshi, leo Januari 12, 2021, Kaimu Katibu Mkuu Nishati, Mhandisi Leonard Masanja amesema mradi huo ni muhimu katika kuendeleza sekta ya Nishati ya umeme Nchini.

Ziara hiyo imefuatia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuanza kutekelezwa kwa miradi ya Ruhudji na Rumakali iliyopo Mkoani Njombe.

Mhandisi Masanja amesema, ujenzi wa miradi ya kufua umeme kawaida inaanza na maandalizi ya awali ambayo ni ujenzi wa miundombinu wezeshi.

"Mradi huu ni kati ya miradi muhimu, tumekuja kuanza maandalizi ya mahita ya ujenzi wa miundombinu wezeshi kama maji, umeme, barabara, na kadhalika", amesema Mhandisi Masanja.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka amesema TANESCO imejipanga kutekeleza mradi wa Ruhudji hadi kukamilika kwake.

Kazi ya ujenzi wa mradi wa kufua umeme kwa maji wa Ruhudji inatarajiwa kuanza mwaka huu 2021 baada ya taratibu za manunuzi kukamilika.






Source : Mradi wa Umeme Ruhudji, Maandalizi ya Miundombinu Wezeshi Yaanza
Kama kawaida Magu.
 
Doto Biteko ameanza kukuumbua
 
Back
Top Bottom