Waziri Makamba acha kuhadaa watu

Waziri Makamba acha kuhadaa watu

Etwege

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2018
Posts
7,345
Reaction score
18,109
Megati 222 = trilion 1.4?( bwawa la makamba)
Vs

Megawat 2225 =trilion 6( bwawa la magufuli)

Hata mwenye akili ndogo ameelewa huu upigaji


Waziri wa Nishati, January Makamba amefika kwenye Wilaya ya Makete Mkoa wa Njombe na kufika kwenye mradi wa kufua umeme kwa Njia ya Maji wa Rumakali (MW 222) wenye thamani ya Shilingi 1.4 Trilioni uliosanifiwa tangu mwaka 1998.

Mbele ya Waziri Makamba, Wananchi wamesema walishakata tamaa ya kuendelezwa mradi huo, Lakini kwa sasa matumaini hayo yamerudi na wanaamini utatekelezwa sababu wananchi hao toka mwaka 1998 walikua tu wakisikia kwamba kuna mradi wa kufua umeme lakini hakukua na mwendelezo au utekelezaji wowote kuhusu mradi huo.

Waziri Makamba amesema >>'Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imeamua kutekeleza mradi wa Umeme wa Maji ya Rumakali uliopo Wilayani Makete Mkoa wa Njombe ili kuwezesha nchi kuwa na Umeme wa kutosha kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vya Nishati, kuanzia Agosti 1 2022 Wathamini wanakuja kuzungumza na nyinyi kuhusu maeneo tutakayoyachukua juu ya fidia zenu kwenye eneo hili la Kilometa za Mraba 13.2 zitakazochukuliwa na huo mradi' - Waziri Makamba.

Tunaona jinsi serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ilivyo na uchu wa maendeleo
 
Mbona huyu February atapata shida ..

Anakula lakini havifiki kwenye utumbo.
Lambda kama anatafuta kwa ajili ya wajukuu.
Vipi kama ikawa vinapitiliza kama ilivyo ada Kwa wanachukua chako mapema 🙄
 
Sisi ndio walipakodi na tuko barida tu wewe hio buku saba ya Lumumba kweni huwa inakatwa hata senti.
Kwanza Kwa kuwa wanachua chakomapema ,wanajichikulia,hawakatwi ila wanajua kusema Kwa wavuja jasho walipa Kodi(kaataaaa)🏃🏃
 
Kwanza Kwa kuwa wanachua chakomapema ,wanajichikulia,hawakatwi ila wanajua kusema Kwa wavuja jasho walipa Kodi(kaataaaa)🏃🏃
Iko namna hawa Matagaling wanavyombebea Bango Waziri Januwari Makamba Mgosi wa zeze ni kwasababu kuna mtu wao alilambwa mutwe na Maza.

Maza keshasema kazi na Bata au Kazi na Kamba.
 
Iko namna hawa Matagaling wanavyombebea Bango Waziri Januwari Makamba Mgosi wa zeze ni kwasababu kuna mtu wao alilambwa mutwe na Maza.
Ndio kawaida ya Sgang,na majungu wanayaweza🏃🏃
 
2115MW kwa 7 trilioni
222MW kwa 1.4 trilioni

Maana yake ni kuwa, anajenga kwa gharama mara mbili ya ile ya bwawa la Julius.

Si ajabu ongezeko la jinsia ya tatu ni la kasi sana!
 
23 February 2021

Tanzania Plans Mega Hydropower Projects to Match Demand​

23 Feb 2021 by powerinfotoday.com
Tanzania has begun preparations for the construction of two large hydropower projects totaling 580 megawatts the minister of energy has announced. Dr. Medard Kalemani said that the Ruhudji Project and Rumakali Project will be located in Njombe Region.

20210223105145685.jpg


He explained that the Ruhudji Project will generate 358 megawatts and the Ruamakali Project will generate 222 megawatts where preparations for the construction of the two major projects have begun its implementation at the same time including the preparation of enabling infrastructure for the official construction of the projects.

“The implementation of these projects started with the design of projects in December 2020 and is nearing completion. We are now looking forward to entering the second stage of announcing tenders to get contractors from March so that by July the contractors will be available and we will officially hand over the construction site so that they can continue construction, “said Minister Kalemani.

Minister Kalemani added that, both projects are expected to be completed within three years and thus add 580 megawatts to the National Grid to increase capacity where currently the National Grid has a capacity of only 1602 megawatts.

“For current needs, the whole country has the capacity to use up to 1400 Megawatts, but the more we add electricity to the Grid, the more we encourage and attract more foreign and domestic investment, so the Government has decided to increase electricity production through these two projects. Ruhudji and Ruamakali ”said Minister Kalemani.

Njombe Regional Commissioner, Engineer Marwa Rubirya thanked the leadership of the Fifth Phase Government, the Ministry of Energy and TANESCO for starting to implement these important projects for the Nation whose research was conducted many years ago but did not reach the stage of implementation.

Ms. Rubirya added that apart from the projects will be of great benefit to the nation but it is the expectation of the people of Njombe that, the projects will open up opportunities for major investment in Njombe Region and surrounding areas.

I assure the Government, the Ministry of Energy and TANESCO that, Njombe Region will continue to implement all the instructions given to take care of the environment that will enable access to water first for the Julius Nyerere Project but also for the Ruhudji and Ruamakali Projects ”said Hon. Rubirya

On behalf of TANESCO, the Deputy Director of Electricity Production, Engineer Pakaya Mtamakaya said in parallel with the power generation projects will be built two ways to transport the electricity of 400 Kilovolti Pressure.

“The first route will be built from Ruamakali to the Mwakibete Mbeya Station and the second from the Ruhudji area to the Iringa Regional Cooling Station to enable the transmission of the electricity to the National Grid and to be used in various regions in the country,” said Engineer Pakaya.

Concluding his visit to Njombe Region, Minister Kalemani appealed to the people of Njombe Region to prepare to receive both projects as well as to seize all opportunities to earn income from the construction of the projects while urging the people of Njombe Region to protect water sources, take care of the environment and all electrical infrastructure.

Source : Tanzania Plans Mega Hydropower Projects to Match Demand - World-Energy
 
TOKA MAKTABA:
Habari za miradi ya umeme wa Rumakali na Ruhuji

01 August 2021

MIRADI YA UMEME RUHUDJI NA RUMAKALI KUKAMILIKA NDANI YA MIAKA MITATU, MSIMAMIZI WA MIRADI ANENA MBELE YA BODI YA WAKURUGENZI WA TANESCO



Jumla ya Megawati 222 za Umeme wa Maji Zinatarajiwa Kuzalishwa Katika Mto Rumakali Uliopo Bulongwa Wilayani Makete Mkoani Njombe ambao Utajengwa Katika Kipindi Cha Miezi 36 Baada ya Hatua za Awali Kukamilika.

Katika Ziara ya Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania Tanesco Ya Kutembelea Miradi ya Ruhuji Wilayani Njombe na Rumakali Wilayani Makete.

Msimamizi wa Muda wa Miradi Hiyo Mhandisi Toto Zedekia amesema Endapo Mradi wa Rumakali Utafanikiwa Kujengwa na Kukamilika Basi Umeme Wake Utaingizwa Kwenye Gridio ya Taifa Kwa Manufaa ya Watanzaia Wote.

Alexender Kyaruzi ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TANESCO Ambaye baada ya Kuzulu Katika Maporomoko ya Maji ya Mto Rumakali Amesema jitihada za Wataalamu wa Nishati Katika Kutafuta Vyanzo vya Maji Kwa ajili ya Kufua Umeme ni Kubwa na Hivyo Zinapaswa Kuungwa Mkono Kupitia Miradi Hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Makete Juma Sweda Amesema Miradi Mikubwa ya Umeme Nchini Imekuwa Ikitegemea Vyanzo Vya Maji Toka Wilayani Humo Hivyo Wananchi wake Wanatakiwa Kukumbukwa Pia Kwa Kupelekewa Nishati ya Uhakika ya Umeme.

Juma Kyando na Christon Mahenge ni Baadhi ya Wakazi wa Wilaya ya Makete Ambao Wanasema Endapo Mradi wa Umeme wa Rumakali Utatekelezwa Basi Watanufaika Pakubwa Ikiwemo Kupatiwa Umeme wa Uhakika.

Source : NJB TV
 
TOKA MAKTABA:

31 January 2021

Utekelezaji miradi ya umeme mto Rumakali na Ruhudji, umefika patamu waziri wa nishati afika eneo la mradi

,JANUARY 31, 2021

Na Amiri Kilagalila,Njombe
Katika kutekeleza azma ya serikali ya kuhakikisha upatikanaji umeme nchini unakuwa wa uhakika na kuwapunguzia wananchi mzigo wa ghalama za umeme pamoja na kukuza uchumi wa viwanda, serikali imeendelea kutenga fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbali ya kuzalisha umeme.

Miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na mradi wa Rumakali uliopo wilayani makete utakaozalisha megawati 222 pamoja na mradi wa Ruhudji uliopo mjini Njombe utakaozalisha megawati 358 na kufanya onezeko kubwa la nishati ya umeme huku mkoa wa Njombe ukiwa ni wa kimkakati huku ukiwa ni mkoa wa pili kwa uzalishaji mkubwa wa nishati ya umeme.

Waziri wa nishati Dkt. Medard Kalemani amebainisha hayo januari 30, 2021 alipofika mkoani Njombe pamoja na kutembelea eneo la maporomoka yam to Rumakali uliopo kata ya Kipagalo wilayani Makete na kubainisha kuwa mradi huo utakaozalisha 222 MW ,tayari utekelezaji umeanza na serikali imeshatoa shilingi bilioni 899 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi.

Dr. Medard Kalemani amefafanua kuwa msukumo wanaoweke katika utekelezaji wa miradi ya kuzalisha umeme ni kwasababu uzalishaji wake ni wa ghalama nafuu na kupelekea wananchi kupata bila changamoto kubwa ukilinganisha na aina nyingine ya umeme.

“Uzalishaji wa umeme kwa maji ni ghalama nafuu kulinganisha na vyanzo vingine, kuzalisha umeme kwa maji Unit moja inaghalimu kiasi cha sh.36 tu huku vyanzo vingine ni zaidi ya sh.103 na kuendelea.

Mradi wa Mwl. Julius Nyerere utakapokamilika utawapunguzia wananchi mzigo wa bei za umeme na bei zitashuka sana”alisema Kalemani
Aliongeza “Utekelezaji wa mradi wa Rumakali na Ruhudji umekwishaanza,timu ya kutekeleza mradi huu imeshaundwa na kimsingi timu hiyo imenza na shughuli za matayarisho ya kuanza miradi tajwa na kufika Julai 02, 2021 ujenzi rasmi wa miaradi ya Rumakali na Ruhudji utaanza” aliongeza Dr. Medard Kalemani
Mbali na hayo amesema katika mradi wa Rumakali kitajengwa kituo cha kupokea umeme na utasafirishwa hadi Mwakibeta jijini Mbeya umbali wa kilomita 150 na vijiji vyote vitakavyopitiwa na njia ya kusafirisha umeme vitapatiwa nishati hiyo.

Aidha amesema bado mikakati ya ukamilishwaji wa kazi ya kupeleka umeme vijijini unaendelea na taratibu zote za kufikisha umeme vilivyosalia nchini zimekamilika ambapo februari 05 mwaka huu 2021 wakandarasi wataanza kuingia kazini ili kukamilisha vijiji vilivyosalia ndani ya miezi 18 kwa kuwa tayari serikali imeshatoa shilingi bilioni 851 kwa ajili ya kazi hiyo huku akiwataka wananchi ambao ambao bado vijiji vyao havijapatiwa huduma kuwa wavumilivu.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa Rumakali, meneja uendelezaji wa vyanzo vya umeme kutoka shirika la umeme Tanzania (TANESCO) mhandisi Toto Zedekia amesema, wamejiridhisha baada ya kufanya utafiti na tathmini ya kina kuwa maporomoko ya mto Rumakali una maji mengi na yakutosha kuzalisha umeme.
“Tumejiridhisha vya kutosha mto huu una maji mengi na kutosha kwa kuwa una mita za ujazo 13 kwa sekunde” na kuongeza kuwa
“Litajengwa bwawa lenye urefu wa mita 870 kutoka kingo moja kwenda nyingine na urefu wa kwenda juu utakuwa ni mita 70 na litakapokamilika litakuwa na uwezo wa kuhifadhi maji ya kutosha”

Awali akitoa taarifa ya hali ya upatikanaji wa umeme mkoani Njombe, kaimu meneja wa kanda ya Nyanda za juu kusini Maghalib Mhandisi Yusuph Salim amesema, hali ya umeme mkoani humo imeimarika zaidi tofauti na miaka ya nyuma na hali hiyo imechangiwa na kukamiilika kwa mradi wa Makambako hadi Songea.

Aidha mhandisi Yusuph amesema upatikanaji wa umeme mijini na vijijini ni wa uhakika na kupitia miradi ya umeme vijijini (REA),takribani vijiji 293 vya mkoa wa Njombe vimefikiwa na huduma ya nishati huku vikisalia 88 ambavyo vyote vimeingizwa katika mradi wa REA awamu ya tatu mzunguko wa pili huku 90% ya miradi ya REA ikiwa imekamilika.

Baadhi ya wananchi wa kata ya kipagalo wamefurahishwa kuona mwanga wa kuanza kwa mradi wa umeme katika mto Rumakali kwa kuwa wamekuwa wakisubiri tangu miaka 40 iliyopita huku wakiamini kupta fursa za kiuchumi mradi huo utakapoanza rasmi.

Katika ziara hiyo waziri wa nishati Dkt. Medard Kalemani ameongozana na maafisa waandamizi kutoka wizara ya nishati na shirika la umeme Tanzania (TANESCO).

Waziri Kalemani akielekea eneo la mradi wa umeme unaozalishwa katika mto Rumakali uliopo wilayani Makete kata ya Kipagalo.

Waziri wa nishati Dkt,Kalemani akizungumza na baadhi ya wataalmu alipopokelewa katika ofisi ya mkoa wa Njombe iliyopo mjini mjini humo alipofika kwa ajili ya kukagua mradi.

Mhandisi Yusuph Salim akitoa taarifa ya upatikanaji umeme kwa mkoa wa Njombe pamoja na utekelezaji wa miradi ya REA mkoani humo.
Source : Utekelezaji miradi ya umeme mto Rumakali na Ruhudji,umefika patamu waziri wa nishati afika eneo la mradi
 

TOKA MAKTABA:​

12 January 2021


Mradi wa Umeme Ruhudji, Maandalizi ya Miundombinu Wezeshi Yaanza​







Maandalizi ya Miundombinu wezeshi kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Ruhudji Mw 358 yameanza rasmi.

Akiwa katika ziara ya kukagua mahitaji ya ujenzi wa miundombinu wezeshi, leo Januari 12, 2021, Kaimu Katibu Mkuu Nishati, Mhandisi Leonard Masanja amesema mradi huo ni muhimu katika kuendeleza sekta ya Nishati ya umeme Nchini.

Ziara hiyo imefuatia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuanza kutekelezwa kwa miradi ya Ruhudji na Rumakali iliyopo Mkoani Njombe.

Mhandisi Masanja amesema, ujenzi wa miradi ya kufua umeme kawaida inaanza na maandalizi ya awali ambayo ni ujenzi wa miundombinu wezeshi.

"Mradi huu ni kati ya miradi muhimu, tumekuja kuanza maandalizi ya mahita ya ujenzi wa miundombinu wezeshi kama maji, umeme, barabara, na kadhalika", amesema Mhandisi Masanja.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka amesema TANESCO imejipanga kutekeleza mradi wa Ruhudji hadi kukamilika kwake.

Kazi ya ujenzi wa mradi wa kufua umeme kwa maji wa Ruhudji inatarajiwa kuanza mwaka huu 2021 baada ya taratibu za manunuzi kukamilika.






Source : Mradi wa Umeme Ruhudji, Maandalizi ya Miundombinu Wezeshi Yaanza
 
Back
Top Bottom