Waziri Maiga shughulikia haraka: Ubalozi wa Ujerumani nchini kubandika ukutani Ramani ya Tanzania inayoonyesha Ziwa Nyasa liko Malawi.

kama wajeruman waliweka mipaka na kuonyesha ziwa liko Malawi na waingereza nao wa
kaonyesha ziwa liko upande wa Tanganyika Basi wenye maamuzi ya kuamua ziwa LA nani ni wajerumani au waingereza, wakae waamue nani mumiliki halali wa ziwa Nyasa/Malawi.
Naubalozi waingereza ubandike ramani yao inayoonyesha ziwa lipo tanganyika inakuwa ngoma droo
 
Ndugu yangu KIDUNDULIMA nimemuelewa vizuri sana mtoa mada, ila inaelekea kuwa hawa wakoloni wawili wamefanikiwa kuteka mawazo yetu waafrika kwa kuaminishwa kuwa mikataba waliyoiweka ndiyo sahihi,na kama ni majadiliano yafuate mipaka iliyoamuliwa na mkutano wa Berlin. Kwa bahati mbaya tangu uhuru hadi siku ya leo si Au au mamlaka yoyote inayotaka tujadili hii mipaka kwa kutumia utaratibu uliokuwepo kabla ya kuja wakoloni na hapa nikimaanisha wajerumani ..1800 kurudi nyuma.

Ikubukwe tu kuwa baada ya wajeremani kuingia afrika mashariki walijitwalia maeneo ya pwani Bagamoyo,badaye Tanga na Moshi. Eneo la Nyika linalohusisha mpaka wa magharibi kwa maana ya mkoa wa Kigoma na ziwa Tanganyika uliingizwa baadaye kwenye himaya na mipaka ya wajerumani, Huku kusini hawakuwahi kuwa na mamlaka kwa sababu akina Chifu Mkwawa na wangoni hawakuwapa mwanya wajeremani wa kujitwalia nchi kirahisi, kwa maana hiyo mpaka kati ya Malawi na eneo la ziwa Nyassa haukuwepo zaidi ya wakazi wa eneo hilo kulitumia ziwa kwa manufaa yao kama ilivyokuwa kwa maziwa mengine.

Mkataba ya Heligoland bado unabaki kuwa mkataba wa kitapeli uliopata kuingiwa na wakoloni bila ridhaa ya waafrika wenyewe na nashangaa sana kuona waamalawi wakiushikia bango kama kielelezo cha umiliki, Ukweli ni kwamba ni waingereza na wajerumani wenye maslahi na agenda ya siri.
 
Hili jambo si la kupuuzwa hata kidogo.Maswala ya mipaka ya nchi yana maslahi mapana kwa watanzania.
Serikali ilisimamie hili jambo kwa haraka na ufasaha.Serikali iwasiliane na wenye mamlaka za kuchora ramani kupata taratibu za kuwa na Ramani inayotundendea haki Watanzania.
Ushauri kwa Mh.Rais,aweke kambi kubwa ya jeshi pande zile karibu na Ziwa nyasa,na activities nyingine kubwa kubwa,ili kujiweka sawa kwa lolote
 
Asante sana kwa uleweshaji mzuri
Thanks again
 
Wawaachie tu, hata maziwa tuliyo nayo hakuna yanacho tusaidia.
Unaweza kuamini kuwa mwanza na bukoba wana mgao wa maji?
Unajua kigoma hakuna maji safi?
Unajua kuwa maji ndani ya mji wa Moro ni kizungumkuti?

Sasa mnagombania ka kipande ka ziwa Malawi ka nini?
 
Wajerumani bro ndo ndo walitutawala mwanzo wanajua mpaka wetu na malawi, Tanzania pamoja na kuwa na Ziwa Tanganyika, Victoria na li bahari lote mnalalamikia hako?? Waacheni wamalawi wajiachie
Sasa hivi Tanzania uzalendo umeshuka sana, wamalawi wakifanikiwa kuchukua ziwa Nyasa Jiandae na Wakenya kubeba Mlima Kilimanjaro..... vivyo hivyo Warwanda na Waganda kugawana Kagera,Bukoba na Kigoma...


Viongozi wajitahidi kuwapa wananchi huduma stahiki ili wawe wazalendo kwa Taifa lao....

Kwa post hii inaonyesha mtu huoni thamani ya kuwa mtanzania....!
 

Lakini mkuu, mkoloni wetu halisi ni Mjerumani na Tanganyika lilikuwa ndilo koloni lake, na ndiyo maana anayo michoro yote ya koloni lake.

Mwingereza alikuja na kufanya marekebesho ya hapa na pale na alishikilia tu Tanganyika na halikuwa koloni lake.

Nafikiri wajerumani wamepitiwa tu maana hizo ramani wanazo nyingi sana tangu hizo za EAGC.

Maestro balozi Mahiga awakumbushe kwamba hatuko tena Germany East Afrika.

Ila Wajerumani ndo wakoloni wetu halisi.
 
Ni OAU mwaka 1963 iliyoamua kuwa, ili kuleta utulivu na maelewano barani Afrika, inability Nchi zone wanachama kuheshimu mipaka ya kikoloni, licha ya Makonda mengi ya kimipaka yaliyowekwa na Wakoloni. OAU iliona kuwa matatizo ya baadhi ya makabila kuwa ndani ya Nchi zaidi ya moja (Tz - Waganda, Wanyamwanga, Mambwe-Lungu, Wakonde/Nyakyusa, Wajaluo, Wakurya, Wamasai, Wayao na Wamwera), ni madogo sana na rahisi kutatatua kuliko endapo Nchi za kiafrika zitatupilia mbali mipaka ya wakoloni.
Tatizo hilo lilitokana na ukweli kuwa: wakati katika Bara Ulaya na Asia, Mataifa (Nations) ndiyo yaliyounda Dola (a Sovereign state); huku kwetu Afrika, Dola/Nchi (States) ndizo zilizounda Mataifa. So Mataifa ya Kuafrika hayakuundwa na kabila moja moja bali makabila mengi, isikuwa tu Nchi ya Somalia iliyoundwa na Wasomali, pamoja na Nchi za Kiafrika. Huku kwetu Sub Saharan Africa, Nchi kama Nigeria, Cameroon na Sudan zina makabila (mataifa) zaidi ya 200 kwa kila moja. Tanzania tumekuwa na makabila 126.

 
Mtakuja kuuza sisi wengine walahi kwa mawazo yako.
Hivi wewe, urithi wa mashamba ambao mababu zako walimuachia baba yako, wangeamua kuuza eti kwa kuwa hawakuweza kulima mashamba yote, ungepata shamba wewe la kurithi?
Mbona Nchi kubwa kama Urusi inang'ang'ania Visiwa vya Kuril vilivyochukuliwa kwa Wajapan baada ya WW II, licha ya kwamba ina eneo kubwa kuliko Nchi zote duniani, huku eneo la Siberia pekee ambayo ni kubwa kuliko Nchi zote duniani likiwa na km square milioni 13 lakini likiwa na wakazi milioni 36 pekee? Kwa nini wasiwaachie tu Wajapani wenye km square laki 3 pekee lakini watu milioni 130?
 
Ukweli mchungu ni kwamba, kihistoria, kisheria na kimataifa, Ziwa Nyasa ni mali ya Malawi. Hata kama watanzania hatuupendi lakini huo ndio ukweli na utaendelea kubakia hivyo hivyo daima.

Ni makosa ya mkoloni katika kugawana Afrika, na makosa hayo hayo ndio yaliweza kutufaidisha Tanganyika(Tanzania) tukamiliki mlima wote wa Kilimanjaro na pia kumiliki kwa sehemu kubwa eneo la ziwa Victoria.
 
Ccm na mambo mengine mngekuwa mnachunguza hivi watu wasiojulikana wangekuwa washakamatwa.Yaani umezoom ,umetafuta reference weee.asante.Na mambo ya muhimu kwa mustakabali wa nchi muwe mnazoom hivohivo mnachunguza out of the box
Hahahaaa!
 
Same old Arsenal yetu Aaron ramsey anakosa nafasi ya wazi kabisa kufunga gili kwa Arsenal.

Dakika zimekwenda ni 38

Goli 0-0
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…