boyskillz
Senior Member
- Apr 29, 2013
- 109
- 104
Kuna watu wamenihoji mtazamo Wangu kuhusu ile bomoa bomoa inayoendelea maeneo mbali mbali hapa jijini Dar es Salaam.
Ndugu zangu si jambo zuri au la kawaida kuona nyumba yako au yenu ikiangushwa chini na wakati huo hauna sehemu ya kujishikiza kwa hiyo itakulazimu ulale nje.
Sipingi wala sizuii serikali kufanya ilichokusudia lakini NAPINGA kwa namna moja au nyingine njia wanazo tumia katika kuziondosha nyumba hizo na wakazi hao.
My take
Kama serikali inaamua kuwaamisha wananchi eneo fulani basi sio kuwalipa pesa na viwanja Bali ni serikali yenyewe iingie jukumu la kwenda kuwajengeja wananchi nyumba kwanza eneo wanaloona linastahili iwakabidhi kisha ndo ikabomoe maeneo yasiyotakiwa kuwapo makazi.
Kwasababu serikali si wanaamini kwamba fidia ile wanayolipwa wakazi inatosha basi serikali yenyewe ikajenge kwanza nyumba hizo kwa hio fidia wanayoiamini ni stahiki kisha wakawagawie wananchi nyumba na sio kiwanja ama pesa kwa sababu nyumba haikamiliki siku moja ukahamia
Ingekuwa ni vyema hatua hizo pia zingechukuliwa hapa Dar kwanza ndo wazibomoe nyumba hizo wanazosema zipo kwenye vyanzo vya maji.
Wanatuambia maeneo hayo hayafai kuwapo na mkazi yoyote! Naomba tujiulize kama wanafahamu hayafai mbona katika kampeni walienda huko huko pasipofaa kubembeleza wakazi wa maeneo hayo ambao Leo wameonekana wadhambi katika macho ya mkuu wa mkoa na waziri wake.
Kwanini serikali ilipeleka umeme maeneo hayo yasiyofaa? kwanini walipeleka huduma zingine za kijamii na wanajua hayafai? Kwanini waliweka hata ofisi za Mtendaji? Kwanini walitoa vibali wananchi wajenge hko? Na mbona ule mradi wao wa mabasi yaendayo kasi bado umepita huko? Kwanini walienda kufanya kampeni maeneo yasiyofaa? Mkuu wa mkoa atujibu maswali haya machache tu.
Kinacholiliwa sasa hivi na wananchi hawa sio nyumba hizo Bali ni mstakabali wa maisha yao, kuna watoto wadogo kabisa hata wengine hawajaanza kutambaa,kuna vikongwe wasiojiweza, kuna wanafunzi hko kuna watu wengine wamepoteza vyeti vyao vya elimu kwa sababu bomoa bomoa ilipokumba maeneo hayo wao walikua makazini.
Naamini serikali ni sikivu iliangalie upya swala hili wajenge kwanza nyumba maeneo yanayostahili wawape wananchi.
Mwisho, Nampongeza Mh. Mbunge aliyeenda kutetea wananchi wake mahakamani na akatuonesha kwa kuna UTAWALA wa sheria nchini kwetu tuachane na Mambo ya KUKURUPUKA.
Namuombea ashinde kesi hio japo ime base maeneo machache.
Eng Enock Ally