figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
Serikali imekiagiza kitengo cha huduma kwa wateja cha Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kufanya kazi hadi usiku.
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya MakaziMheshimiwa WILLIAM LUKUVI amekiagiza kitengo cha huduma kwa wateja cha wizara hiyo kifanye kazi hadi usiku ili kuwahudumia kikamilifu wananchi wanaohitaji huduma za kitengo hicho.
Mheshimiwa LUKUVI ametoa agizo hili wakati wa ziara ya kushtukiza katika kitengo hicho akifuatana na maofisa wa wizara hiyo kuzungumza na waanchi waliokwenda kutafuta huduma ikiwa ni pamoja na kutafuta hati zao walizokuwa wakizidai tangu mwaka 2006.
Akielezea jinsi kitengo hicho kinavyofanya kazi, Kamishina Mkuu wa Ardhi ambaye pia ni Kaimu Katibu Mkuu Dakta MOSES KUSILIKWA amesema watumishi wa kitengo wanafanya kazi kwa uangalifu na uadilifu hata kuweza kuwabaini watu wanaokwenda kutafuta hati ambao ni matapeli .
Katika hatua nyingine zoezi la kuweka alama ya "X" katika nyumba zilizopo katika bonde la Mkwajuni jijini Dar es salaam limeanza rasmi na wananchi wote wanapaswa kuondoka wenyewe kabla ya nyumba zao hazijabomolewa ifikapo Januari Tano mwakani.
Chanzo: ITV