Waziri Lukuvi, aongoza bomoabomoa Coco beach Dar es salaam

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,720
55,852
Waziri Lukuvi ameongoza zoezi la bomoabomoa jijini DSM katika maeneo ya Coco Beach.
uploadfromtaptalk1454167830848.jpg

Waziri wa ardhi, nyumba na makazi Mh.William Lukuvi ameongoza zoezi la bomoa bomoa jijini Dar es Salaam katika maeneo ya ufukwe wa Coco pamoja na uzio uliojengwa pembezoni mwa moja ya hoteli za kitalii ambazo zipo karibu na eneo hilo.

Mhe.Lukuvi amesema ameamua kuongoza zoezi hilo baada ya kubaini kuwa ujenzi wake haukufuata taratibu na ameiagiza taasisi za kuzuia na kupambana na rushwa-TAKUKURU kuendesha uchunguzi dhidi ya waliohusika na ujenzi katika maeneo hayo ili waweze kuchukuliwa hatua stahili.

Waziri huyo wa ardhi, nyumba na makazi amesema serikali kamwe haitishiwi na aliowaita wanatumia kiburi cha kuwa na fedha nyingi katika kufanya ujenzi hata maeneo yasiyo stahili na atahakikisha wanadhibitiwa.

Chanzo: ITV
 
Wayakumbuke na maeneo ya wazi yaliyovamiwa na kuuzwa kwa watu. Tibaijuka alikuja na kasi mpya toka HABITAT akaweka na mabango yenye kuonyesha maeneo ya wazi lakini hadi leo mabango yapo na nyumba zipo. Watu walikimbilia mahakamani kuweka zuio mambo yakapoa hadi leo. Nadhani ingukuwa bora jama eneo linajulikana kuwa liko kwenye ramani ya mipangomiji kama eneo la wazi kama kuna jengo libomolewe na mwenye jengo apeleke shauri mahakamani kuthibitisha kwamba kaonewa. Sio akasimamishe ubomoaji!
 
na hizo kodi zote walizokusanya hapo, wawarudishie hao wawekezaji! Wanafiki wakubwa, kodi walikuwa wanakusanya, halafu leo wanasema sio sehemu salama, kwa maana ya kulinda fukwe! fukwe bongo.

Hii nchi nafiki sana, wanashindwa kulinda vyanzo vya maji, wanakuja kulinda miishio ya maji....? Ajab kabisa
 
Pole sana kwa yanayokukuta. Huu ni mwisho wenu WAHUJUMU UCHUMI na mliozoea kutumia kauli Kama "Serikali mmeiweka Mfukoni". Fukwe ulitaka ziwe wapi labda!? Kwenu Mumbai au Bombay!? Inatia hasira kwa Wabantu Kama wewe wenye fikra za kibwanyenye na ugabacholi uliotukuka.
 
Ndg unaandika tokea chooni nn mbna hasrahivyo
 
Pole sana kwa yanayokukuta. Huu ni mwisho wenu WAHUJUMU UCHUMI na mliozoea kutumia kauli Kama "Serikali mmeiweka Mfukoni". Fukwe ulitaka ziwe wapi labda!? Kwenu Mumbai au Bombay!? Inatia hasira kwa Wabantu Kama wewe wenye fikra za kibwanyenye na ugabacholi uliotukuka.
Ubaguzi, ubaguzi, ubaguzi....
 
na hizo kodi zote walizokusanya hapo, wawarudishie hao wawekezaji! Wanafiki wakubwa, kodi walikuwa wanakusanya, halafu leo wanasema sio sehemu salama, kwa maana ya kulinda fukwe! fukwe bongo.

Hii nchi nafiki sana, wanashindwa kulinda vyanzo vya maji, wanakuja kulinda miishio ya maji....? Ajab kabisa
Uwe tayari kulipa fidia za uchafuzi wa mazingira jipu we!
 
Pole sana kwa yanayokukuta. Huu ni mwisho wenu WAHUJUMU UCHUMI na mliozoea kutumia kauli Kama "Serikali mmeiweka Mfukoni". Fukwe ulitaka ziwe wapi labda!? Kwenu Mumbai au Bombay!? Inatia hasira kwa Wabantu Kama wewe wenye fikra za kibwanyenye na ugabacholi uliotukuka.

Mkuu kama kawaida yako. Ulianza kukoment vizuri tu lakini mwisho ukaamua kuonesha sura yako halisi ya kibaguzi.
 
Kawaida yangu ni ipi mkuu!? Maana hata MKE wangu wa ndoa haijui na hajawahi kuijua kawaida yangu!!
 
Ubaguzi, ubaguzi, ubaguzi....
Kama kutetea Maslahi na Kanuni za nchi ni UBAGUZI acha niwe mbaguzi. Ila mlizoea kuifanaya Tanzania Kopo la chooni, unalithamini ukiwa unatumia...ukimalizana nalo unalitupa kwa hasira kwenye ndoo. Mtaiheshimu SERIKALI awamu hii hamna jinsi.
 
HAO Waliouza Na Waliotoa Vibali Vya Ujenzi, Ndio Wanaohitajika Now, Ili Wawe Mf. Na Funzo Kwa Wengine!!!!
 
Back
Top Bottom