Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,411
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amemsimamisha kazi Afisa Mipango Miji wa Lindi, Castory Manase Nkuli baada ya kunyang`anya ardhi ya vijiji vya Ruvu na Mchinga hekari 4000 na kumilikisha kampuni ya Azimio Housing Estate kinyume cha sheria.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimsimamisha kazi Ndugu Castory Manase Nkuli Afisa Mipango Miji kwa tuhuma za kumilikisha ardhi kinyume cha sheria
Waziri Lukuvi aligundua hayo baada ya kuona utaratibu wa umilikishaji wa ardhi haukufuatwa na badala yake kuonekana kuwa na mianya ya rushwa kwa kuwa ardhi hiyo imehamishwa kutoka ardhi ya kijiji hadi kumilikishwa kwa kampuni ya Azimio ambapo kisheria ilitakiwa hati ya eneo hilo itoke kwa idhini ya Rais.
Afisa Mipango Miji huyo aligundulika kuwa na kosa la kughushi kwa kujifanya ni Afisa ardhi baada ya kuandika barua na kuisaini kwa niaba ya Afisa ardhi wakati yeye ni Afisa Mipango Miji ili kuimilikisha kampuni ya Azimio Housing Estate ambalo pia ni kosa kisheria.
“Kama nyie hamna uwezo wa kumfukuza kazi basi mie namsimamisha kazi kuanzia leo hafai kuwa mtumishi wa serkali” alisema Lukuvi huku akiagiza eneo hilo lirudi na kuwa mali ya serikali. Sasa hiyo ardhi lazima irudi itakua mali ya serikali kuanzia leo”.
Akithibitisha makosa hayo Kaimu Mkurugenzi Mipango Miji na Vijiji kutoka Wizara ya Ardhi Bi Immaculate Senje amesema kwamba utaratibu wa umilikishaji wa ardhi hiyo haukufuatwa ambapo kisheria ilitakiwa hati ya eneo hilo itoke kwa idhini ya Rais na baada ya Tangazo la Serikali na kuridhiwa na wana kijiji.
Chanzo: Bongo 5