Waziri Lugola kuvunja mabaraza ya usalama barabani si hatua sahihi, hali za barabara ziboreshwe, madereva wadhibitiwe.

Waziri Lugola kuvunja mabaraza ya usalama barabani si hatua sahihi, hali za barabara ziboreshwe, madereva wadhibitiwe.

Richard

Platinum Member
Joined
Oct 23, 2006
Posts
16,630
Reaction score
25,586
Ajali za kila mara zimekuwa ndiyo habari kubwa nchini kwa sasa.

Kule eneo la Mparanga wilayani Mkuranga, kulitokea ajali kubwa na watu 24 wakafariki na wengine 10 kujeruhiwa vibaya.

Juzi kule Mbalizi mkoani Mbeya ajali ingine ikatokea na watu 20 wamefariki na wengine 45 kujeruhiwa vibaya.

Pamoja na kwamba vyanzo vya ajali zote hizi mbili ni mwendo wa kasi na uendeshaji magari usofuata sheria za barabarani, bado uchunguzi unatakiwa ufanyike ili kubaini vyanzo vingine zaidi ambavyo vinasababisha kutokea kwa ajali kama hizi.

Leo hii waziri wa mambo ya ndani mheshimiwa Lugola amevunja mabaraza ya usalama barabarani nchini kote, sidhani kama mheshimiwa waziri ameshauriwa vyema juu ya hili.

Kinachotakiwa kufanyika ni kuangalia muundo wa mabaraza haya kama kunahitajika marekebisho, utendaji wake, bajeti yake ni kiasi gani, ufanisi wa kampeni zake na ni watu wa aina gani wanaunda mabaraza haya.

Akifanya hivyo atabaini kwamba pengine anayahitaji sana mabaraza haya kuliko kuyavunja na kubakia na idara za usalama barabarani ambazo nazo hazijafikia kiwango cha kimataifa.

Ni vizuri mheshimiwa waziri Lugola akafikira tena juu ya hatua yake hii alochukua ambayo hata kama ni kusoma kwa ndani ya masaa 48 yalopita basi atakuwa alikuwa tayari ametoa maamuzi kabla ya kuapishwa.

Kuna haja ya waziri Lugola akaangalia suala la madereva wa magari makubwa na mabasi madogo na kuangalia namna ya kuwasaidia hawa madereva ambao hizo kazi za udereva ndizo ajira zao na wana familia zinazowategemea.

Kama si hivyo, basi madereva hawa huwa wanaacha magari hayo yaendeshwe na wahuni ambayo wakiishakolea bangi vichwani huamua kuendesha watakavyo.

Madereva kutoiva kisawasawa kwa kufahamu sheria za usalama barabarani.

Madereva wanapaswa kufanyiwa mitihani na kupimwa uwezo wao wa kuendesha magari makubwa na mabasi madogo.

Mitihani hii yaani "driver's competency test" inaangalia uwezo wa dereva kukumbuka sheria za usalama barabani na uzingatiaji wa sheria hizo.

Wanapofaulu mitihani hii basi wanapatiwa cheti maalum cha DCT na kinadumu kwa miaka mitano tu na kila baada ya miaka mitano wanafanya mtihani mwingine.

Pia madereva wapimwe hali zao kiafya pamoja na macho baada ya miaka mitatu ili kubaini hali yoyote ya utata kiafya na kama macho yao yana nguvu kuona umbali fulani.

Chuo cha usafirishaji kichunguzwe namna kinavyotoa vyeti vya udereva.

Kwa kuwa chuo hiki ndicho chuo kinachotambulika rasmi na serikali basi kinapaswa kufanyiwa uhakiki wa wasimamizi wake wa mitihani kama kuna dalili za rushwa kutolewa kwa watahiniwa.

Hii itaondoa mashaka makubwa juu ya taasisi hiyo na hata kule VETA na vyuo vingine vya udereva ambavyo pengine havijakidhi hadhi ya kufundisha udereva.

Iundwe taasisi ya udhibiti wa madereva na magari yote.

Ni vizuri serikali ikaunda taasisi maalum mfano wa NIDA ambayo itakusanya taarifa zote za madereva na magari yote.

Kazi ya taasisi hii itakuwa rahisi mno kwa kuwa tayari taarifa nyingi za madereva zitakuwa zipo NIDA kwa wale watanzania lakini madereva wageni watakuwa na kanzi-data yao.

Magari yanapofanyiwa ukaguzi basi taarifa zote badala ya kuwekwa kwenye makaratasi, zoezi zima la ukaguzi linafanywa kupitia mtandaoni na taarifa zinaingizwa moja kwa moja kwenye mfumo wa computer.

Hii itasaidia kubaini magari na madereva wazembe au waso madereva pale wanapopita katika vituo vya ukaguzi.

Dereva anapofika kwenye kituo anaingiza kadi ya DCT na anaingizwa kwenye mfumo ambao itamuangalia atakapokuwa akisafiri na gari hadi anapofika mwisho wa safari.

Hivyo basi pamoja na gari kuwa na kifaa cha kudhibiti mwendo (sifahamu vimeishia wapi) bado anakuwa anafahamu kwamba anaangaliwa namna anavyoendesha gari.

Hali hii itaenda sambamba na udhibiti wa magari kuona ubora wa injini, ubora wa matairi na kama yanafaa kuendelea kutumika baada ya muda fulani.

Kwa mfano taasisi hii itaangalia aina ya matairi yote yanayoingizwa nchini na kwa kuwa bado kiwanda chetu cha general Tyre bado hakijaanza kazi rasmi ya uzalishaji matairi, basi matairi yote kutoka nje yanapaswa kuangaliwa ubira wake na kuthibitka kuwa ni bora kabla ya kutumika kwenye barabara zetu.

Uboreshaji barabara alama za barabani na ufungaji kamera maalum

Hali ya barabara zetu bado si ya kuridhisha na ukiangalia barabara ya Mbalizi ambayo ina mteremko inahitaji kingo maalum, alama za kutosha kuonya madereva kuhusu mteremko huo na kamera maalum kuchukua picha za magari yanayozidisha mwendo.

Alama za barabani bado ni muhimu sana kwa nchi kama ya kwetu na wala alama hizi hazigharimu fedha nyingi kuzitengeneza.

Serikali kupitia kila mkoa ingepanga bajeti maalum kwa kila idara ya usalama barabani kuhakikisha kila mkoa una alama za kutosha za barabani na kamera maalum "speed camera".

Kamera hizi maalum zitaondoa mianya ya rushwa kwa askari wa usalama barabarani ambao huruhusu magari yaendelee na safari ilhali yana matairi mabovu au ubovu mwingine.

Pia kanera hizi zitakuwa zimeunganishwa na mtandao maalum wa internet na picha maalum zikipigwa na gari kuzidisha mwendo, basi taarifa zinakwenda moja kwa moja kituo cha usalama barabani cha mkoa ambao watamshugulikia huyo dereva mkosefu.

Madereva ambao wanapatikana na makossa ya kuzidisha mwendo hupewa faini maalum ambayo watatakiwa kuifuata kwenye kituo cha idara ya usalama barabani na kisha kuipeleka TRA ambako watalipa faini hiyo na kuongeza trilioni zetu za kila mwezi kama mapato ya taifa.

Ifanyike kampeni ya AJALI SASA BASI nchi nzima.

Kwa kuwa wananchi ndiyo waathirika wakuu wa ajali hizi ambazo zinasababisha umauti na watu kupoteza ndugu zao na pia kusababisha ulemavu wa kudumu na matatizo mengine, basi serikali iwashirikishe wananchi kwenye kampeni ya nchi nzima.

Kufanyike kampeni na wananchi wapewe namba maalum ya kuripoti gari yoyote ile inayozidisha mwendo katika barabara yoyote ile na dereva ashitakiwe kwa uzembe au kusababisha ajali.

Narudia kutoa ushauri, Mheshimiwa waziri afikirie tena uamuzi wake wa kuvunja mabaraza ya usalama barabarani.
 
Ushauri wako ni mzuri. Siku hizi kuna tabia ya magari ya jeshi la wananchi na pia jeshi la polisi wanapita njia zisizo ruhusiwa wakati kuna foleni. Wakijifanya wana haraka. Kisa hiki ndicho kilisababisha ajali na kuua wanachuo wa mlimani kwani dereva akiwa na ambulance, anapita kulia ambapo anakutana na magari yanayokuwa kwenye maeneo yake.

INABIDI WAANZIE HAPO. KUDHIBITI MAGARI YA JESHI KUPITA NJIA ZISIZO SAHIHI KWA KUJIFANYA WANA HARAKA.
Utakuta Dakitari anaenda muhimbili yuko kwenye follen lkn Gari la Jeshi linapita kulia likijifanya lina haraka. Hivi Jeshini kuna haraka ya nini mpaka kuvunja sheria za barabarani huku matrafiki wakiwaangalia tu bila kuchukua hatua?.
Najiuliza maswali mengi kuwa hata Tyson kule marekani na maguvu yake, aingie dukani na kuchukua vitu bila kulipa kwasababu ana nguvu za kupindukia?
 
Suala la faini liangaliwe upya. Faini itozwe kwa lengo la kumrekebisha dereva na siyo tu kama chanzo cha mapato.Hii inatokana na madereva wengi kuzoea adhabu hiyo na pia ni chanzo cha rushwa. Inafaa kuwe na adhabu za uwajibikaji pale inapothibitika kuwa gari lililopo njiani siyo salama kwa matumizi na hivyo kuhatarisha maisha ya wananchi. Adhabu hiyo ianzie kwa mmiliki na dereva ili kisiwepo kisingizio chochote. Tukikimbizana na faini tutafurahia mapato mengi huku tukigharimu maisha ya watu. Jeshi la polisi wasikimbilie kutoza faini ili hali utapokea hiyo faini na mwishowe watu watakufa.
 
Traffic wakikusanya mapato mengi....
ni wazi kwamba bado hakuna elimu ya kutosha kwa madereva...
kwa hivyo bado wana kazi kubwa ya kutoa elimu ya kutosha
ili mapato yapungue.....
 
Suala la faini liangaliwe upya. Faini itozwe kwa lengo la kumrekebisha dereva na siyo tu kama chanzo cha mapato.Hii inatokana na madereva wengi kuzoea adhabu hiyo na pia ni chanzo cha rushwa. Inafaa kuwe na adhabu za uwajibikaji pale inapothibitika kuwa gari lililopo njiani siyo salama kwa matumizi na hivyo kuhatarisha maisha ya wananchi. Adhabu hiyo ianzie kwa mmiliki na dereva ili kisiwepo kisingizio chochote. Tukikimbizana na faini tutafurahia mapato mengi huku tukigharimu maisha ya watu. Jeshi la polisi wasikimbilie kutoza faini ili hali utapokea hiyo faini na mwishowe watu watakufa.

Adhabu kwa mmiliki wa gari itakuwa baada ya uchunguzi maana kwa mfano inawezekana mmiliki amenunua matairi mapya lakini dereva anaenda kuyauza mahala kisha afunga tairi mbovu ambazo zitasababisha ajali.

Au mmiliki amenunua kifaa cha kudhibiti mwendo na dereva anakifungua anapofika huko njiani hapo mmiliki anapaswa kila mara kufanya ukaguzi kugundua kasoro yoyote kwenye kifaa hicho.

Hapo huwezi kumlaumu mmliki bali kumbana dereva wa hilo gari.

Ndiyo maana suluhisho la uhakika ambalo halina wa kumlaumu ni kuweka Speed Camera barabarani ambayo itapiga picha pale mwendo unapozidishwa.

Kwa hiyo speed Camera zitaondoa rushwa na mrija kwa jeshi la polisi kujipatia mapato yaso yao.

Faini inatakiwa ilipwe na dereva mkosaji Mahakamani ambako mapato yataingia serikalini moja kwa moja.

Speed Camera zilizofungwa pembezoni mwa barabara na faini zitapungua na madereva watazingatia sheria za barabarani na hakutahitajika askari wa usalama barabarani kuvizia madereva wavunja sheria.

Halafu, hizi speed camera si lazima zimilikiwe na usalama barabani kampuni binafsi zinaweza kufanya kazi hiyo kwa leseni maalum na kwa kushirikiana na idara ya usalama barabarani.

Pia faini hiyohiyo inaweza kutumika kutoka elimu kwa dereva mkosaji ambapo kampuni au taasisi itakayotoa mafunzo endelevu itakuwa ikilipwa sehemu ya faini hizo.

Hapo unaondoa kabisa uwezekano wa faini hiyo kuonekana kama ni mrija kwa jeshi la polisi kujipatia mapato ya ziada.
 
Back
Top Bottom