Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,842
- 24,614
Nilikuwa posta ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani kumejaa sana kutokana na wingi wa waandishi na washika dau mbalimbali ambao wameamua kufatilia suala la aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani mwetu ndugu Kitwanga ambaye alisitishiwa nafasi yake hiyo isiendelee kutokana na kilichoelezwa kuwa ni "Ulevi"
Waandishi wengi ni dhahiri walipenda wasikie ni nini atakachosema Mwathirika huyo wa Kwanza wa Uwaziri katika Serikali ya Mh Dr J.P.Magufuli. waandishi wengine walionekana wakiteta kwa kumwonea huruma na huku wengine wakipongeza kitendo cha yeye kundolewa kwenye nafasi hiyo nyeti kwa fedheha. nikajikuta nami kama mdau nikiwaza hivi hakukuwa na namna nyingine ya kumwondoa kutokana na skata lile au hilo la Lugumi isipokuwa kutumia kigezo kama hiki? anyway wakuu wenyewe ndo wanajua lakini hili li jambo zito kusema kuwa alikuwa amelewa. sijajua kilitumika kigezo gani kugundua hilo. lakini kama alilewa kiukweli alikosea sana kufanya masikhara kwenye mambo nyeti ya mustakabali wa Taifa hili.
Ningekuwa ni mshauri wake ningemshauri aachane kabisa na mambo hayo ,huu ni wakati wake wa kumrudia Mungu akitubu na dhambi zake nyingine zote kama anazo. sana sana namtia moyo asife moyo sisi Watanzania hatujamchukia.
akabidhi ofisi kwa Naibu au Katibu Mkuu kwa sasa mpaka tutakapopata waziri mwingine. yu never know, naweza kuwa mimi.