Zero Hours
JF-Expert Member
- Apr 1, 2011
- 12,944
- 18,653
Weekend iliyopita niliamua kufanya Utalii wa ndani katika Kisiwa cha Sanane kilichopo Mkoani Mwanza. Niliamua kupeleka Familia yangu ambao kwao ingekuwa ni mara ya kwanza kufika mbuga ya Sanane.
Binafsi nilitembelea hiki kisiwa mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2013.
Hata ivyo sikufurahia sana kulinganisha miaka kama 20 iliyopita.
Nakumbuka hiki kisiwa kilikuwa na vivutio na burudani nyingi sana tofauti na wanyama wachache waliopo hivi sasa kama swala, Mamba, Punda na ngedere .
Nakumbuka sana apo zamani kulikuwa na SOKWE aliyekuwa kivutio kikubwa sana kipindi icho bila Kusahau Simba, mbwa mwitu, Tembo, Tausi na wanyama wengine wengi. Nilikuwa mdogo sana nikiwa na umri wa miaka kati ya 7 hadi 12.
Nakumbuka miaka iyo siku za weekend, mamia ya watu ( asilimia kubwa wakiwa Watanzania) walikuwa wakijazani katika kisiwa hiki wakiburudika na vivutio vingi vya kitalii vilivyokuwa vimesheheni katika mbuga ya saanane.
Sina uhakika kama leo hii hivi vivutio vilirudishwa tena tokea mara ya mwisho kutembelea mbuga hii maana hata wekend iliyopita sikufanikiwa kufika katika mbuga hii. Changamoto kubwa ilikuwa ni Usafiri wa majini kufika katika mbuga hii.
Nilifika ofisini na kuuliza utaratibu ukoje na wakanifahamisha utaratibu mpya uliopo sasa. Na huu utaratibu mpya ndyo ulionifanya nishindwe kufika uko.
Utaratibu hivi sasa ni; unatakiwa kukodi boti private kwa cost ya 59,000 pamoja na 5,900 kama kingilio cha kila kichwa. Huu utaratibu sio kama ule wa zamani ambao kulikuwa na masaa maalumu ambayo boti ilikuwa inaondoka endapo kuna watu au watalii wanaotaka kwenda katika hii mbuga.
Binafsi hii cost ilinikatisha tamaa kabisa. Nikawaambia wanafamilia yanguu hii ni karibia 70,000 si bora tukanunue mbuzi mzima tukamchome tule tufrahie tu maana hata uko tunakoenda kuona sana sana tungeona swala na mamba tu.
Ukilinganisha na cost za zamani hii ni pesa ndefu sana na inadiscourage utalii wa ndani. Mwananchi wa kawaida kama mimi hatuwezi kabisa hizi gharama. Nakumbuka mara ya mwisho 2013 nilienda sanane kwa gharama ya elf 4000 tu.
Kwa hali niliyoona leo katika zile office za mbuga ya Sanane ni kuwa tunapoteza mapato mengi sana amabayo tungepata kutokana na utalii wa ndani katika hiki kisiwa. Yani hakuna watalii na pamedolola tu. Ni kama wale wahudumu wa maliasili ( TANAPA) wanakula tu mshahara wa bure
Kwa muda niliokuwepo pale zaidi ya saa zima, sikuona mtu wala mtalii hata mmoja anayekuja kuuliza kwenda kule. Nilishangaa sana wakati miaka ya zamani, siku za weekend watu waalikuwa wakijazana kuelekea Mbugani. Boti 2 zilikuwa zinapishana yani zinaenda na kurudi zikipeleka na kurudisha watu ( watalii). Serikali ilikuwa ikukusanya pesa nyingi sana wakati ule.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dr. Kingwangalla Pamoja na Serikali ya Awamu Ya 5 tunawaomba muangalie jinsi ya kufufua utalii katika kisiwa hiki. Hatuwezi kutangaza utalii wakati sisi wananchi wenyewe tunashindwa kutembelea mbuga zetu za Wanyama.
Hatuhitaji kusubiri Wazungu ndyo waje kutalii mbuga zetu. Hata sisi tunaweza ingiza pato la taifa kupitia utalii wa ndani na kutangaza vivutio vyetu vya utalii.
Ushauri wangu ni, vile vivutio vilivyokuwepo zamani pamoja na huduma na burudani zirudishwe bila kusahau kupunguza gharama ili kuvutia wananchi kutembelea Mbuga ya sanane ili kutangaza kimataifa vivutio vyetu vya utalii.
Ikishindikana apewe mwekezaji binafsi afufue hii mbuga ya Wanyama. Hata mimi mnaweza nibinafsishia hii mbuga muone maajabu.