Waziri Kigoda - Bungeni Leo

Waziri Kigoda - Bungeni Leo

SaidAlly

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2011
Posts
2,392
Reaction score
2,360
Nimeangalia kipindi cha bunge jioni hii kinachoendelea tbc1.

Kwa kifupi sana simfagilii Mh. Kigoda kwa historia yake huko nyuma isipokuwa jinsi alivyokua akijibu hoja za wabunge kwa unyenyekevu na pasipo kua na mipasho kama tulivyoona jana kwa huyo dokta wenu wa barabara....

ameonyesha mfano mzuri sana kwa taifa letu. Japo inawezekana baadhi ya majibu hayakujitoshereza lakini kwa jinsi alivyokua anajibu inafungua milango kwa wabunge ambao hawajaridhika wanaweza kumfuata nje ya bunge na kupata ushirikiano mzuri.

Laiti Mawaziri wangekua wakijibu hoja kama viongozi wa Serikali pasipo kua na ushabiki wa vyama naamini nchi yetu ingeendelea vizuri kwa amani na michango ya wabunge hasa upinzani wangesaidia sana kujenga nchi yetu.

Nampongeza Kigoda sana kwa busara aliyotumia na nina imani kama mawaziri wote wangekua wanafanyahivyo...bunge letu lingekua linafanya maamuzi ya maana kuhusu nchi yetu na sio zile staili za mipasho za magufuli na wenzie wapenda sifa za ccm.

Wananchi tunaona na tunaelewa.

Angalizo:
Simaanishi ndio agombee uraisi. Pia samahani wadau siwezi kuandika tukio zima lilivyokua ila wenye kuweza wawekeeni wadau kwa uelewa zaidi.
 
Kwa hiyo wapinzani wamemsifia? Ama vip?

kwa muda nilioangalia nimemsikia Sugu akimpongeza kwa kujibu kama dokta na Waziri wa Serikali kwamba hakupiga mipasho kama alivyofanya Magufuli jana (nukuu yangu si neno kwa neno kama alivyosema sugu isipokua ni jinsi nilivyomuelewa)

Kwa ukweli Kigoda ameonyesha busara sana na amepokea michango hadi ya upinzani kwa roho safi. Nampongeza Sugu pia kwa kuwa mkweli na kusifia panapostahili.
 
Nami pia nimemkubali Dr Kigoda hakuonesha mbwembwe hata kidogo. tunaitaji mawaziri kama hawa ili nchi kusonga mbele.
 
Back
Top Bottom