Waziri Kabudi aomba Bunge kupitisha Bajeti ya TSh 519.66 Bilioni kwa mwaka 2025/2026

Waziri Kabudi aomba Bunge kupitisha Bajeti ya TSh 519.66 Bilioni kwa mwaka 2025/2026

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975
Bunge la 12 Mkutano wa 19 Kikao cha 19 Mei 7, 2025

Orodha ya shughuli za leo;

  • Hati za kuwasilisha mezani
  • Maswali
  • Hoja za serikali


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Palamagamba Kabudi amesema Rais Samia ameweka mazingira wezeshi kwa Wasanii nchini kwa kuwapa mitaji ya kuboresha kazi zao ambapo katika uongozi wake amefufua mfuko wa Utamaduni na Sanaa uliokuwa umekufa kwa zaidi ya miaka 10 na kipindi kifupi jumla ya miradi 359 ya Utamaduni na Sanaa imepatiwa mikopo yenye jumla ya thamani ya TSh. Bilioni 5.250.

Waziri Kabudi amewasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2025/2026, ambapo ameliomba bunge lipitishe bajeti ya jumla ya TSh 519.66 bilioni.

Serikali kuanzisha Chombo maalum kusimamia Miundombinu ya Michezo


"Serikali imeanza mchakato wa kuanzisha chombo maalumu cha usimamizi wa miundombinu ya michezo katika kukabiliana na changamoto za uendeshaji wa miundombinu ya michezo nchini,"

"Chombo hicho kitapewa mamlaka ya kusimamia uendeshaji, ukarabati na matunzo ya miundombinu yote ya michezo nchini."

"Hivyo, ni matumaini yetu kwamba kuwapo kwa chombo hiki kutapunguza changamoto za usimamizi wa miundombinu na kutaongeza thamani ya miundombinu ya michezo nchini,"

Maandalizi ya AFCON 2027

Kuhusu maandalizi ya fainali za soka za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 ambazo Tanzania itaandaa kwa kushirikiana na Kenya na Uganda, Profesa Kabudi amesema wizara inaendelea na ukarabati mkubwa wa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

"Ukarabati huu umejumuisha maeneo ya vyumba vya wachezaji (dressing rooms) na maeneo ya waandishi wa habari (media tribune and press conference),".

Ameongeza kuwa "maeneo mengine ni kufunga viti vipya na kuondoa vya zamani ambapo hadi kufika Aprili 2025 jumla ya viti 40,000 vimewasili na vinaendelea kufungwa. Kukarabati eneo la mchezo wa riadha kwa kuondoa na kuweka taa mpya."

Ametaja pia kuwa mifumo ya viyoyozi, mtandao wa intaneti, majitaka (ikiwamo vyoo), pamoja na uchoraji wa rangi sehemu mbalimbali nayo inakarabatiwa, huku "jumla ya taa 352 zikiwa zimefungwa."

Mengine ni "kuondoa na kufunga milango mipya, kukarabati jukwaa la viongozi na kuondoa na kupanda nyasi mpya sehemu ya kuchezea."

Kwa ujumla, Profesa Kabudi amesema "ukarabati wa uwanja huu umefikia asilimia 80."

Kuhusu Uwanja wa Uhuru, amesema kuwa "ukarabati mkubwa wa uwanja huo umefikia asilimia saba."
 
Back
Top Bottom