Maneno Meier
JF-Expert Member
- May 12, 2013
- 2,469
- 1,697
Waziri Jaffo sisi watanzania tuna kupenda sana kwa vile unaonyesha kuwa kweli wewe moyo wa uzalendo na nchi yako kama wa Rais wetu mpendwa Magufuli anao, unao pia na zaidi ya hayo usimazi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya taifa kulingana na matakwa ya Rais wetu una yafanya kwa ufanisi mkubwa sana. Endelea hivyo hivyo waziri wetu.
Waziri Jaffo naomba nikuambie kitu, wewe umekuwa Role model wa vijana wetu Tanzania kwa hivi sasa. Wengi wao wanataka wawe kama wewe, kwa kweli ni kitendo cha kufurahisha sana. Utendaji wako wa kazi una wapa watanzania wengi faraja kubwa sana kiasi kwamba wanakuona wewe ni mfano wa kuigwa kama hujui.
Lakini hata hivyo Waziri Jaffo pamoja na sifa zote hizo tunazo kupa kuna tatizo moja kubwa ambalo bado unalo, wewe una huruma sana na watanzania wazembe wasio penda kujituma. Nakusihii Waziri wetu tafadhali, acha mara moja huo mtindo wa kuwaonea huruma hao wazembe na wakwamishaji wa maendeleo yetu. Hawata badikika tena. Wamesha zoea hivyo. Utapigizana nao kelele mpaka utachoka, hawata kuelewa kamwe na matokeo yake naye Rais akiona mambo hayaendi vizuri kama anavyotaka atakutumbua wewe mwenyewe. Kitu ambacho sisi wafuasi wako hatutapenda.
Nakuomba hao watendaji wako wa serikali waki mess tu watoe wote, asibaki mtu hata mmoja. Na kama madaraka hayo huna basi mshauri Rais au Waziri mkuu ambao wana madaraka makubwa wafanye hivyo. Nina uhakika Rais huyu anaye penda maendeleo ya watanzania, atakuunga mkono tu kwa vyovyote vile.
Tanazania haina uhaba wa Ma-engineer. Ma-engineer tunao kibao ambao hawana kazi za kufananya na hata wengine kudiriki kuhama nchi na kwenda kutafuta riziki zao nje. Unawabembeleza wa nini mazombi hao wasio kwenda na wakati?
Mijitu iliyo zoea kuto tumia ubongo wao kuelewa kwa nini wamepewa wadhifa wa kutekeleza sera za chama na malengo ya serikali kwa maendeleo yao wenyewe, watoto, familia zao, unafikiri ita kuwa rahisi kutambua wajibu wao na kuwa na mwamko wa kujituma kwa ajili ya maendeleo ya watanzania wengine kwa ujumla? Achana nao. Watakufanya uonekane mpiga domo tu kwa Rais na hatimaye akaondoa uaminifu kwako. Watakufanya uugue ugonjwa wa moyo bure waziri wetu. Tunakuhitaji bado!
Wazembe wa namna hii Waziri Jaffo tunaomba wasipewe tena nafasi ya kupewa miradi nyeti ya maendeleo nchini Tanzania. Inasikitisha sana kuona jinsi wanavyo tokwa na mishipa kujaribu kudanganya. Kudanganya kwenyewe hawawezi bali ni uwenda wazimu na visa tu.
Wao wanafikiri watanzania wote wana akili kama zao. Kama hizo nafasi walikuwa wakipeana kiundugu au kiurafiki huko nyuma, watambue kuwa wakati muafaka umefika sasa wa watanzania kuchukua maamuzi yao wenyewe ya maendeleo ya nchi yetu. Hatutaweza mvumilia mtu mzembe na mkwamishaji wa maendeleo ya nchi yetu tena. Na wewe waziri Jaffo ndiyo uwe mfano wa kuwapiga na kuwa bwaga chini kama gunia la mahindi. Kuwa na "ZERO TOLERANCE" na mazombi hayo yasio taka kubadilika na kwenda na wakati!