Waziri Dr. Mwakyembe huyu ndio mkurugenzi wako

Waziri Dr. Mwakyembe huyu ndio mkurugenzi wako

KAMCHIMBE23

New Member
Joined
Feb 27, 2013
Posts
4
Reaction score
0
Mwanzoni nilikuwa nafikiria wengi wa watumishi katika Mamlaka ya Usafiri wa Anga wanamuonea huyu Mkurugenzi wetu Mkuu Bwana Fadhili Josia Manongi kwa kusema hajui kazi na anaendesha mamlaka kwa majungu. Sasa nimeamini hilo kwa matukio yafuatayo;

1. Amekuwa akifanya kazi kwa majungu ambayo anayasikiliza hasa kutoka kwa Kurugenzi wake wa Huduma na Biashara Bwana Reuben Ruhongole, huyu Ruhongole amekuwa na chuki na uadui mkubwa kwa baadhi ya wafanyakazi kiasi hupeleka majungu kwa Mkuu ambapo wafanyakazi husika hukataliwa kuongezewa mikataba ama kuhamishwa kituo.
Na katika hilo wengi wa wafanyakazi baadhi yao kwa walio na ndugu zao huko juu wamefanikiwa kupanchi uhamisho ama kurudishwa pale walipohamishwa.Ila kuna baadhi ilkula kwao ambapo waliamishwa na wengine kukatiziwa mikataba kwa chuki za Miungu watu hawa

Mfano:IBRAHIMU NATEPE (ACCOUNTANT); alihamishiwa KIA kutoka chuoni lakini kwa kuwa ni mtoto wa laiekuwa mkubwa simu ilitoka juu tuu na uhamisho ukafutwa.

LILIAN MEEELA (MASJALA): Huyu sakata lake lilianzia pale miaka ya nyuma kwa kumkataa Bwana Mapenzi Reuben na hatimae alihamishiwa kituo cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa - JNIA, na pia aliona haitoshi alimuandikia barua ya kukatisha mkataba wake wa kazi japo Mheshiwa Rais alishatoa tamko watumishi wote amabao wana Mikataba wenye umri mdogo waajiriwe isipokuwa wale tuu waliobakisha muda mchache wao waliwaajiri kwa Permanent wale waliowapenda kama SHRO lakini wengine ndio wakanziwa visa vya kuondoka,matokeo yake ilitoka agizo kutoka ngazi za juu na Lilian amepewa ajira ya kudumu;

TALA MTANDALA (DRIVER): Huyu alipunguzwa kazi kwa majungu na kuambiwa mkataba umeisha ila alipokwenda mahakamani wakashindwa kesi wamemrudisha kazini

SASA NAKUJA KATIKA TOPIC KUBWA ILIYONISHANGAZA KWA HUYU MKURUGENZI MKUU Bwana F. Manongi, wao walikaa vikao vyao vya menejiment ambavyo kwa kiasi kikubwa wasemaji ni Ruhongole na Fadhili na waliamua wamuamishe Bwana Philip Komanya (Driver) kwa zile zile chuki za Bwana Mkubwa sana ruhongole kwa watumishi akiwemo Komanya, ambapo kichekesho ni kwamba alipewa barua ya uhamisho na baada ya masaa mawili uhamisho ukafutwa baada ya Komanya kumvaa Mkurugenzi Mkuu na kumueleza alichomueleza mpaka huyo Bwana manongi akatishika na kumuagiza Ruhongole afute uhamisho wa huyo dereva. Derevaaa anakubabaiishaje Mtu Mkubwa kama wewe?Inaonyesha bwana Komanya alikua na ukweli ambao walimgwaya wakijua anaweza kuupeleka mbele ya safari.

Hivi kweli pamoja na madaraka yako ya ukurugenzi Mkuu unatishwaje na mtu wa cheo cha chini kama dereva na wewe kufuta maamuzi mliyoamua katika kikao na Wakuu wenzako?

Hivi kweli pana utawala bora hapo kwa kucheza na maslahi ya watu kuwahamisha hamisha na pindi wanapokwenda kwa wakubwa uha,isho unafutwa?

Hivi kweli Bwana Ruhongole anajua sheria za kazi mpaka dereva uliemfukuza kazi anakushinda kiurahisi mahakamani?

Pia huyu Bwana ruhongole ni mtu ambae anakwamisha mambo mengi lakini Bodi ya TCAA inayajua na kuyafumbia macho, mfano akiwa Mkurugenzi mwenye dhamana ya ajira alishawahi kutoa majibu ya Interview kwa watu wake ila Mama Munyagi alikua mjanja akagundua baada ya wale watu kufanyishwa tena Interview bila kuwepo Ruhongole na walikosa majibu ya kujibu.

Akiwa mkurugenzi mwenye dhamana ya Huduma na Biashara ameshindwa kukusanya mapato kiasi imekuwa ni kawaida kwa Mamlaka kukosa pesa na unapoenda Bank na cheki unarudishwa eti hakuna pesa, sasa kama hakuna pesa kwa nini muandike cheki? Pesa zinaenda wapi ilkiwa ndege zimeongezeka?Wanashindwa kuwadai baadhi ya wateja toka mwaka jana kama Tanzanite JET ambae inaonyesha pesa za wananchi zinaingia mifukoni mwao.

Huyu Bwana Ruhongole amewachagua jamaa zake ambao hawajua walichokifanya kuja kufanya mchakato wa mshahara mpya na hakuna cha maana kilichofanyika ila kazi kubwa imefanywa na wataalamu wa ndani.

NAWASHAURI MPUNGUZE IDADI YA MAADU MMEBAKISHA MUDA MCHACHE KUACHIA NGAZI, MTAKUTANA NA WATU BARABARANI MTAONA AIBU
 
Ruhongole ni smart bwana.sema hapendi longolongo lazima umchukie
 
acha majungu kwanin kama madai ya kwel usifate taratibu.acha majungu bwana.kaz haziend ivyo.
 
Jamani you could solve this in your meetings. Hatuhitaji kujua mambo yenu.
 
Acha majungu na fanya kazi; majungu hayajengi yanabomoa!! Inaelekea hupendi wenzio waliofukuzwa kazi warudi kazini kwanini hasa? Bahati yako, mimi ndio ningekuwa Manongi saa hizi unakaa na mkeo nyumbani mnatazamana!!
 
Ukiona ofisi majungu mengi ujue:
1. Ofisi chovu haina hela kutwa kukalia majungu
2. Ofisi hakuna kazi ndo maana wanakalia majungu
3. Elimu mgogoro?
4. Viongozi hawajiamini wala kujitambua ndo maana wamekalia majungu??
 
Acha majungu na fanya kazi; majungu hayajengi yanabomoa!! Inaelekea hupendi wenzio waliofukuzwa kazi warudi kazini kwanini hasa? Bahati yako, mimi ndio ningekuwa Manongi saa hizi unakaa na mkeo nyumbani mnatazamana!!

Kwa wengine majungu, kwa wengine lete nondo!! Double standard. Acheni watu wapumue waanike na kama kuna mtu anaona ameguswa aingie uwanjani na kusema anachojua si kuwazuia wengine kusema. Hapo TCAA kuna ujinga mwingi sana na uongozi unaachwa tu uharibu.
 
Majungu kila sehemu, popote pale ridhiki inapopatikana huwezi kukwepa majungu!.zinatofautiana tu levels..watu dizaini hii lazima wawepo!
 
Mwakyembe is eating from too many plates!!! Aliwapa ATCL miezi mitatu ama sivyo angewatimua; hiyo miezi mitatu bado haijaisha? He aught to be consisitent with his ultimatums otherwise he will not be taken seriously.
 
wewe ndo una majungu na muoga ndiyo maana unaleta magazeti kwenye JF. Nyie ndo wanafiki na waoga mnaopenda kuandika vipeperushi na kuvirusha usiku kama wale wenzenu wa KEC kule kibaha, if you are serious why not sitting in the meeting and speak out! acheni uoga, mpaka mtu kuwa mkurugenzi ameshapita kwenye huo ujinga wako unaosema na amechunguzwa vya kutosha> you are just rumer monger. acha unafiki
 
Kweli tuache kuwa na double standard, vingine vinashabikiwa na vingine vinafanana watu wanasema ni majungu! Kama ni majungu yaacheni tu yatapita kwa nini yapigiwe kelele?
 
Ndiyo Watanzania hawa tena wasomi.Utashangaa lugha za mitaani mpaka sekta nyeti za utendaji Serikalini.Tutapata wapi muda wa kujifunza mabadiliko ya maendeleo ya kitekinolojia yanayotokea Duniani?.
 
Ningependa kumjibu ndugu kamchimbe 23 kama ifuatavyo: Kwanza nasikitika ndugu huyu alivyojitahidi kuuficha ukweli ili uongozi wa sasa TCAA uonekane haufai sijui ni kwa maslahi ya nani. Kwanza ikumbukwe wazi mambo mengi yamefanyika katika kipindi cha mkurugenzi alieondoka na hatukusikia kelele zinazotolewa leo,mfano wakati wa mama munyagi kiliundwa kitengo katika idara cha mtu mmoja na kikawa kinatengewa mamilioni ya fedha hakuna alieuliza au kuandika tuhuma yoyote ,baadae mtu huyo alipofanyiwa kampeni ya kupata kazi Africa Mashariki kitengo kilifutwa.Nasema kampeni kwa sababu katika usaili wapo waliofanya vizuri kuliko yeye lakini alibebwa.Pamaoja na kusomeshwa kwa garama kubwa kuliko mfanyakazi yoyote. Pili ni jambo la kawaida wakati huo kwa watu Fulani kupewa upendeleo wa kila kitu hata ilipokuwa yanafanyika mabadiliko ya wakuu wa viwanja kuna watu walikuwa hawaguswi yote hayo tunaelewa. Pia kwa chuki tu kuna watu walifanya usaili na kufaulu vizuri lakini hawakupewa nafasi kuitumikia idara ,leo hii wamepata fursa hiyo na wameonyesha ni wachapakazi hodari katika mamlaka. Tatu:Ujenzi wa aviation house uliasisiwa na utawala uliopita na viongozi wa sasa walikuta basi limeshaanza safari na matokeo yake wote tunajua. Nne:wafanyakazi kupunguzwa kazi na baadae kurudishwa kazini na mahakama haikuanza leo ,tunamkumbuka engineer Ngiloi aliondolewa kazini na alipofungua kesi alishinda na kuigarim mamlaka mamilioni ya pesa na mpaka leo anadai mamlaka . Tano:Kuhusu uhamisho ni kitu cha kawaida sio mara ya kwanza wafanyakazi kufanyiwa uhamisho kwa mfano Natepe alishawahi kupelekwa Zanzibar kwa uhamisho wa muda wakati wa mama munyagi,yusuf mwadini alipelekwa arusha kwa muda,kuswai na beatrice wameletwa dar na chilala amepelekwa mwanza mpaka leo yupo huko na wahasibu wengi walibadilishiwa vitengo ili kupata uzoefu na sio kukomoana ,hoja hiyo pia haina msingi wowote. Kwa hiyo kinachoonekana hapa ni chuki kwa uongozi huu mpya na wala sio utendaji kwani katika kipindi kifupi cha mkurugenzi manongi wale waliozoea kuiba na kufuja idara hawana nafasi na wanataka mkurugenzi mkuu amuondoe luhongole kwa sababu anaonekana kikwazo cha genge la ufisadi,nani asiejua alivyoondolewa mvunjapori kwa sababu ya kutetea wanyonge. Tuwache majungu waacheni viongozi wachape kazi.
 
.
KWAKO NDUGU MPITIMBI, NADHANI WEWE NDIO UNAJALIBU KUUFICHA UKWELI KWA KUJALIBU KUTURUDISHA ENZI ZA MAMA MUNYAGI NA MIMI NITAKUJIBU KAMA IFUATVYO 1. KWAKUWA WAKATI HUO SIKUWEPO SIWEZI KUZUNGUMZIA HUYO MTU ALIEUNDIWA KITENGO NA KISHA KUTAFUTIWA KAZI EAST AFRIKA 2. KAMA KULIKUWA NA WATU WANAPEWA UPENDEREO KATIKA INTERVIEW ALIEKUWA AKIWAPA NI LUHONGOLE KWANI YEYE NDIO ALIKUA MUHUSIKA MKUU PIA ALIKUWA AKIWAPA BAADHI YA WATU MAJIBU NA USHAHIDI UPO 3. UONGOZI ULIOPO WALIKUTA AVIATION HOUSE IMESHASIMAMA ILA KULIKUA NA MAREKEBISHO MADOGO MADOGO, MBOA WALISHINDWA KUSHUHULIKIA UMEME KWA MWAKA MZIMA TUKITUMIA GENERATOR HAPA JENGONI, NANAI ATALIPA HARAMA ZILE 4.KAMA HAPO MWANZO WALIPUNGUZWA NA NDIO HAO WAKUBWA ZAKO NAO WAIGE TEMBO, SASA MBONA KILA KESI INAWASHINDA, AU MTU NA MAELIMU YAKO DEREVA ANAKUSHINDAJE KWA HOJA MAHAKAMANI UONI KAMA PANA MAPUNGUFU 5. KAMA NI UHAMISHO WA NATEPE UMESEMA ULIKUA WA MUDA KWENDA ZANZIBAR TENA KULE NI KWAO MBONA HUO WA KIA ULIGONGA MWAMBA, KUHUSU MVUNJAPOLI PIA SIKUWEPO WAKATI HUO IVYO SIWEZI KUSEMEA HADITH ZILIZOPITA 6. UNAPOSEMA LUHONGOLE ANADHIBITI UBADHILIFU NA GENGE LA MAFISADI SIKUELEWI KABISA, WATU WANAFUJA PESA MPAKA MAMALAKA INAKOSA PESA BENKI NI CHEKI NGAPI ZA WATEJA ZIMEZUIWA HAPO ACCOUNTS KWENU MAELEZO HAKUNA HELA KWA BANK WAKATI MAPATO YANAONGEZEKA. HIVI KUWALIPA WATU MIL 40 KWA KAZI YA KUPATA USHAURI WA AVIATION HOUSE SIO UFISADI, KWANINI WASINGEWATUMIA WATAALAAM WA NDANI AMBAO WALIKUA WAMEJAZANA PALE KASWELA,MUSA NA KALEKWA, NA KATIKA HILI MTU KAMA MUSA , MTEULE NA LUHONGOLE NDIO WANGEBANWA VIZURI HASA SABABU WALIKUWEPO KABLA YA PM NA KIPINDI HICHO BWANA KALEKWA ALIKUA MGENI YEYE NA PM WANGESIMAMIA KUSHAURI TUU MUSA NA TIMU YAKE WANGETOA MAELEZO MUHIMU,SASA MATOKEO YA RIPOTI YA MIL40. AU KATIKA VIKAO VYA UJENZI WALIFATA POSHO TUU.

KAZI YA KUANGALIA MISHAHARA MIPYA, NANI ASIEJUA KAMA KAMPUNI ILIKUA YA LUHONGOLE? HAKUNA KILICHOFANYIKA PALE NI LONGOLONGO TUU, UNALINGANISHA KAZI ZA MAANA NA KAZI AMABZO KALIAKOO ZIMEJAA HIYO AKILI AU MATOPE, HIVI PROCUREMENT, WAHASIBU, HR SI WAMEJAA TELE MITAANI? LEO KATAFUTE CONTROLLER, AIS AU ENGINERES KAMA UTAWAPATA KIRAHII, MATOKEO YAKE MMECHUKUA VIZEE VYA WATU KUJA KUWASAIDIA, MFANO MDOGO MUSA MMEMUONDOA HQ AMBAPO ALIONEKANA MUHIMU MBONA SASA KAZI ZINAKWENDA KAMA KAWAIDA NA HAMJAONGEZA MTU.

HALAFU WE MPITIMBI USIMFANANISHE MAMA MUNYAGI NA MANONGI ALIESHINDWA SHEREHE ZA AVIATION, MAMLAKA HAINA HELA NI JAMBO LA KAWIDA, MTANDAO UNA KIZUNGUZUNGU MWEZI SASA HAKUNA JITIHADA ZOZOTE, UNIFOM HATUNA TUNASHINDWA NA VIWANJA VYA NDEGE, CALENDA UNATOA MWEZI WA 3 HALAFU MBOFUMBOFU, DAYARI HAKUNA, ANAYUMBISHWA HATA NA WATU WACHINI, HANA MSIMAMO NA MAAMUZI YAKE, MIKATABA MINGI MIBOVUBOVU NA TUNAONA,BADO UNAMSIFIA TUU SEMA JINGINE WE KIBARAKA
 
Back
Top Bottom