Waziri aanika uozo wa wahisani mbalimbali

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=2]30 MAY 2012[/h]
Na Pamela Mollel, Arusha


IMEELEZWA kuwa bajeti nyingi za nchi za Afrika zimekuwa tegemezi kwa wahisani jambo ambalo linachangia uwepo wa matumizi mabaya ya rasilimali za nchi kwa maslahi ya wahisani husika.

Pia Serikali imetakiwa kutumia utawala bora wa fedha kwa wananchi wake na matumizi sahihi ya mali asili ili ziweze kuwa na tija kwa vizazi vijavyo na kuitumia demokrasia katika kukuza pato la wananchi.

Changamoto hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Elimu Mafunzo ya Amali kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Ally Juma Shamuhuna wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha kwenye mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).

"Tumekuja kujifunza suala zima la demokrasia inavyoweza kukuza uchumi wa nchi yeyote sanjari na utawala bora wa matumizi ya fedha za serikali
na kuwa tunaelekea kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2012-13 ambapo tayari tutakuwa na tumepata uzoefu," alisema Waziri huyo.

Alisema kuwa, Serikali yeyote itakayofuata mambo matatu na kuyajali kwa maslahi ya wananchi wake hususan utawala bora wa fedha, matumizi sahihi ya
demokrasia sanjari na matumizi ya mali asili zitaifanya serikali kutokuwa
tegemezi kwa wahisani.

“Mashirika haya ya fedha ulimwenguni hayatoi fedha bure, lazima watangulize maslahi yao hali inayopelekea nchi zilizofadhiliwa 'kubaka' demokrasia na wananchi wake kuendelea kuwa maskini,” alisema Bw. Shamuhuna.
 
Uozo wa Wahisani, hatuoni Uozo wa Serikali na Mawaziri wake kwa Ulaghai na Ufisadi Mpaka Bajeti haitoshi inabidi

kutegemea huo Uozo wa Wahisani? Jamani serikali ya CCM acheni kukufuru.
tozi+83.jpg
 
Huyo mwana CCM ndio anajua leo? Ndio matatizo ya kuwa tegemezi....siasa ya ujamaa na kujitegemea si tuliiacha wenyewe, tunataka kuishi kwa misaada
 
Kimsingi hakuna jipya hapo, alikuwa anakamilisha mada yake ili alipwe posho sidahni kama alikuwa anamaanisha hayo aliyoyasema. Baada ya mada kabla ya kurudi Zanzibar lazima atapita katika Ofisi za Balozi za Magharibi kuulizia fursa za misaada kwa jimbo lake. So nothing new its just the continuation of the "Poverty Policy of Africa"
 
Back
Top Bottom