Hata wazee wastaafu ambao wanapata pension nao wanapewa posho au ni wale ambao hali sio nzuri kimaisha?
Na ni vema wawajali hao ambao hawajiwezi maana wakiweka sera kuwa wote wenye miaka 70 nakuendelea ina maana hata wenye nacho watapewa, waaangalie sana hao wasionacho inshallahHilo sijui Mkuu kwani taarifa ya BBC haijafafanua zaidi. Mimi nilichoshuhudia ni wazee wa kawaida sana mtaani wakiwa vituoni wakivuta mikwanja.
Something is better than nothing Mkuu. Hapo kuna kilo 3 za sukari (4,500); 5 za mchele (7,500); 3 za maharage (6,000); na salio linabaki kwa ajili ya chumvi. Mwezi haujasogea hapo? Tushukuru hata kwa kidogo tunachopewa.Mbona kasenti kenyewe kadogo hivyo $9
Ni afadhali kupata kidogo kuliko kukosa kabisa. Hicho ndicho kiasi kinachowezekana kwa sasa. Hali ya uchumi ikiwa nzuri zaidi kiwango kitaongezeka. Hongera CCM kwa kuja na mpango huu.Mbona kasenti kenyewe kadogo hivyo $9
kitita cha dola 9 nyuso za bashasha wakitia madole gumba haya kila la kheri
Something is better than nothing. Milioni inaanza na 1.Siwezi kusifia kumpa mzee $9 kwa mwezi hata kidogo. Mleta mada ameshindwa kugeuza hiyo $9 kwenye hela yetu kwa sababu anajua ni kiasi duni sana.
Haya ngoja tuingie kazini tuone kiasi wanachopata.
$9 kwa tsh ni 19800 kwa mwezi.
Kwa siku ni 19800/30 ambayo ni tsh 660.
Sasa mzee wa watu hana kipato chochote unampa tsh 660 kwa siku. Hii ni kwa ajili ya fegiii au?
Lakini nimegundua kitu kimoja....katika hiyo 660 mzee anaweza nunua karanga 6 na akabakiza shilingi 60 kwa ajili ya ugoro. Tena hapa nina wasiwasi ugoro wenyewe unaweza kuwa ni tsh 65. Dah masikini wazee wengine wasiokuwa na uwezo wa kujiliza ili wapunguziwe kale ka dala (tsh 5) wanaweza wakaukosa.
Kwa hiyo mlo wa asubuhi karanga mbili, mchana karanga mbili, usiku anamalizia zile mbili zingine na ananusa ugoro siku inaisha. Unajua siyo mbaya sana hata hivyo kwa sababu wazee wetu siyo walaji sana.
Kwa wazee wenye akili wanaweza kuwa wananunua karanga zao 198 mapema kabisa kwa ajili ya matumizi ya mwezi.
Something is better than nothing. Milioni inaanza na 1.
Bahati mbaya au makusudi😕!Nafikiri hii habari itaandikwa nchini Zanzibar, jaribu kufuatilia magazeti yao waweza Iona,
Na ni vema wawajali hao ambao hawajiwezi maana wakiweka sera kuwa wote wenye miaka 70 nakuendelea ina maana hata wenye nacho watapewa, waaangalie sana hao wasionacho inshallah