Wazee wetu walisomeshwa bure wakapata kazi nzuri serikalini, leo wanataka sisi watoto wao tusio na ajira rasmi tulipe madeni yasiyoisha!

Burkinabe

JF-Expert Member
Feb 12, 2023
1,896
3,206
Asalaam Aleykum.
Inasikitisha sana kuzaliwa kwenye nchi ambayo watu wake wamejaa ubinafsi na kila mtu yuko tu kuangalia maslahi yake na ya familia yake!

Yaani nyinyi ma "Baby Boomers" ndo wa kutufanyia hivi kweli?!
Nyinyi mlisoma bure, tena shule nzuri, zenye walimu wazuri, madarasa mazuri, material ya kujisomea ya kutosha, chakula kizuri, tena wengine mpaka nguo mlikuwa mnafuliwa na kutandikiwa vitanda vyenu pasipo kulipia chochote kabisa. Tena hata nauli, tunasimuliwa mlikuwa mnaandikiwa "warrant" na mnasafiri bure kabisa kutoka kwenu hadi shule, na kutoka shule hadi kwenu.

Tunasimuliwa tena kwamba, kabla hata ya kuhitimu, Taasisi nyingi zilikuwa zinawagombania kwa ajili ya kwenda kufanya kazi huko.

Cha kusikitisha, wale waliopata nafasi za kutengeneza mifumo ya elimu, wao wakasahau kabisa kwamba walisoma bure na kuanza kuweka sera kandamizi dhidi ya watoto wao!

Itoshe tu kusema inasikitisha sana kuwa na viongozi wabinafsi wasiojali maslahi ya watu wao..
 
Ungewahi kuzaliwa
 
Back
Top Bottom