Wazee wa 'HIGHWAY ' tukutane hapa

samuel faraj

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
1,326
1,265
Hii ni special kwetu wazee wa barabarani share chochote kuhusu barabara kuu e.g. Kipande kipi cha HIGHWAY kizuri, kibovu, chenye watekaji wengi, wazee wa torch wengi ,sehemu yenye sharp corners nyingi,barabara yenye vurugu nyingi(umakini wa hali ya juu unahitajika hapa) etc

Experience yangu katika kua highway
1. Kipande kilichonyooka unamaliza hata darsh board (Lamadi-bunda-sirari, bukoba _kyanga, hedaru-same)

2.Barabara inayohitaji concentration kubwa(Tanzam HIGHWAY) hii ina gari nyingi sana na wazee wa malori usiku wasumbufu sana mwendo wa full light tu

3.Barabara yenye wazee wa kazi(watekaji), Tanzam highway( maeneo ya doma) , biharamulo-kigoma, wami darajani

4.Kipande chenye wazee wengi,Iringa-mbeya, dar-tanga- moshi

5.barabara zenye sharp corners (namtumbo-tunduru,dodoma-iringa road, njombe-madaba, kitonga)

Tiririka na wewe experience yako HIGHWAY

 
Dah!! umenichekesha sana kwenye hiyo namba 4 hapo umetusingizia wakali wa TANZAM ila hili jambo nlikutana nalo mwaka flan nlikua na route za dar-tanga na dar-lushoto aisee sio siri nilishangaa sana kukuta yaani wazee wa makamo kabisa yaani wale waliokua wanapaswa kukaa nyumbani na kupumzika lakini bado wako road wanang'oa mihogo halafu gari zenyewe canter au fuso ambazo ni unfriendly kabisa kwa umri wao. Hadi wengine hata kutembea vizuri hawawezi lakini wapo mzigoni. Hapo kwenye namba 3 naomba uongezee mkoa wa Singida kwa ujumla wake.
Hapo namba 2 trucks zipo nyingi lakini wengi wao sio wakorofi sana, ila ukitaka uipate fresh iwe ni jumanne usiku na jumatano hapo unakutana na IT zimefunguliwa mzee na hivi utafkiri wote ni watoto waliolelewa na mama mmoja, akitoa mmoja wote sita wanatoa unaweza kushuka na panga kwenye gari ukachinja mtu....
Big up umenikumbusha enzi nikiwa dere
 
hahaha wazee wa IT wakorofi sana nao wanatembea rough sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…