Wazazi wenzangu nishaurini

Ungetulia kwanza upunguze jazba then uandike thread mkuu!!!
 
AU unaishi kwa wazazi wako pamoja na dada zako AMA unaishi kwako lakini umelelewa kwa kutawaliwa kiakili na kiamaamuzi.
Jikomboe kaka.
 

Ushauri wangu ni mfupi tu ndugu,

Uza hiyo simu unayotumia kuwepo hapa jf kisha kanunue kiwanja na utaanza kujenga nyumba taratiiiibu uepuke adha ya kukaa chumba kimoja huku una watoto wa miaka mitano na dada zako wanakuzonga,

Unaishi chumba kimoja na familia ya watoto wa wili huku unamiliki simu ya milioni moja na nusu???
 
Prov 13:24: "He that spareth his rod hateth his son: but he that loveth him chasteneth him betimes (diligently)."

"...spare the rod, spoil the child..."
 
Acha ujinga. Hebu tafuta vyumba viwili ukae na wanao. Kwa binti madenge hata kwa 50,000/- unapata vyumba viwili. Na uhame hapo unapokaa karibu na mama yako na wanao! Nna maneno yako kama laki tano hapa! Ina maana mwanao wa kiume chakula cha usiku hali home, na anaondoka mwenyewe kwenda kulala? Akilawitiwa njiani utasemaje? Ungekuwa kakangu na mie ningekudunda!
 
mmh
dada wa aina gani hao wanaotaka kumpiga kaka yao mwenye mke na watoto wawili?

we ni kichwa cha familia..act like one
 
Nimehangaika kweli kusoma hii mada. Dah! Sasa sijajua unacholalamika ni nini wakati we ndo hutekelezi majukumu yako kama mzazi. Iweje we ulale wakati hujahakikisha wanao wamelala? Mtoto wa miaka 5 anaenda kwenye vibanda vya kuangalizia pilau we habari huna halafu dada akikuhabarisha na kukukemea unakasirika? mtoto wa miaka 5 hakukosea kwenda kuangalia video saa 3 usiku bali wewe ndiye uliyekosea kwa kutomfundisha mwenendo toka mapema. Labda ulikuwa hujui, ulivyojua hukutakiwa kumuangushia kipigo bali kumkanya kwa maneno na kumfuatilia.

Mtoto wa miaka 5 anatakiwa kuwa chekechea na mara nyingi kutokana na uchovu wa mchana si rahisi kumkuta macho saa 3. Huyo inaelekea hata shule haendi, mitaa ndo shule yake. Lakini pia unawapa mzigo watu walioko kwa mama yako wakiwemo dada zako mzigo wa kulea mtoto wako wakati hawako tayari. Tukiwaambia watu humu wasioe mpaka watakapokuwa tayari ikiwa ni pamoja na uwezo wa kifedha wanatuona tumepinda. Sasa wewe tafuta hela kwa bidii panga nyumba ya kukutosha wewe na familia yako, hakikisha unaishi mazingira ambayo ni salama kwa watoto, halafu wewe na mke wako mtambue kuwa jukumu la kulea ni kubwa na linahitaji uzito wa pekee.
 
mmmh mkuu nunua basi tv hapo home sio vizuri mtoto wa miaka mitano anaenda kuangalia tv kwa jirani tena usiku...ila mi naona yote ni uzembe wako tu.....
halafu hebu hama hapo ukapange mbali na nyumbani kwenu ili uwe huru (mwisho dada zako wataanza kuchunguza kama unamfikisha mkeo kileleni shaulilo.)
 
Mi sijamuelewa, unaishi karibu na kwenu? Mara mtoto analala kwa bibi mara miembe mara mashetani .Rudia kuandika upya, usije ukapewa matibabu yasokuhusu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…