barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Wakuu,
Mimi nimepata majaribu kidogo,nina binti wa kazi niliyekaa nae huu mwaka wa 12 sasa.Nilimchukua kwao akiwa bado binti mdogo sana wakati huo nikiwa na mke wangu na ndoa mbichichi.
Pendekezo la kumchukua binti huyu lilitoka kwa mke wangu ili wawe wanasaidiana kazi za hapa na pale,ukizingatia wakati huo my waifu alikuwa mjamzito na pia anaenda ofisini,sababu mimi sikuwa na uzoefu sana wa wadada wa kazi nilimwachia hiyo kazi yeye ya kumtafuta huyo dada wa kazi.
Tumeishi na huyo dada wa kazi kwa zaidi ya miaka kumi,na kwa kweli hata ukija nyumbani kwangu huwezi kudhania kuwa huyu ni dada wa kazi sababu alishakuwa kama sehemu ya familia kabisa na ilifikia hata mimi "kujisahau" na kuona kuwa huyu ni mtoto wangu na si dada wa kazi.
Alikuja akiwa binti mdogo sana,baadae niligundua kuwa ana uwezo sana wa kusoma na kujieleza,tukampeleka English course kwa muda kadhaa,baadae tukakubaliana ajiunge na darasa la "Qualifying Test" wao huita "QT" ili akifaulu basi apate nafasi ya kujiunga na mtihani wa kidato cha nne.
Alifanya mtihani wa "QT" kwa miaka miwili bila mafanikio,lakini mwaka wa tatu akapata "Pass" na hatimaye kupata sifa za kufanya mtihani wa kidato cha nne kama "Private Candidate",Mungu si Athumani alifaulu na kupata credit.Tulimpigania akajiunga na masomo ya kidato cha tano na cha sita na hatimaye alifanya vizuri na kupata nafasi ya kujiunga chuo kikuu.Huko tuliamuacha huru achague kile anachopenda kukisomea.
Muda wote pale mtaani watu walikuwa wanajuaa huyu ni mwanangu au basi kama si mwanangu basi ni ndugu yangu.Hata watoto wamekuwa na wanamuita dada,na kwa nilivyowasoma hata watoto wangu huwa wanajuwa kuwa yule ni dada yao wa kwanza kuzaliwa.Maana kuna mambo huwa wanaongelea wakiashiria kuwa yule ni dada yao mkubwa na ni mtoto wangu.Tulikubaliana na waifu kuwa ipo siku tutawaweka watoto tuwape ukweli juu ya huyu "dada" yao.
Baada ya maisha yake ya chuo hatimaye binti amepata kazi na mchumba,wakati wote alipokuwa kwangu wazazi wake tulikuwa tukiwatembelea na kuwajulia hali,na tulikubaliana na binti kuwa sababu yeye pale amefikia anaishi kama nyumbani tu basi hela yake ya mshahara tuwe tunawapa wazazi wake moja kwa moja.Tumekuwa tunafanya hivyo kwa miaka mingi sasa.
Kifupi aligeuka toka kuwa mfanyakazi mpaka kuwa "mtoto wa familia",na hakika amenisaidia sana mimi na mke wangu katika kuwakuza watoto wetu vizuri sana kwa kadiri ya mapenzi ya Mungu.Watoto wangu wanampenda sana,wakati mwingine mpaka naogopa,ilifikia kuna mtoto mmoja tukiwa tumelala nae usiku akiamka anataja jina la house girl,mpaka tunaamka na kumpeleka chumba cha haosue girl ndio analala.
House girl wangu amekuwa,amesoma,ana kazi na sasa amepata mchumba ambaye kwanza alinitambulisha mimi kabla ya wazazi wake,na baadae tulifanya taratibu za jamaa kuwajuwa wazazi wake wa kweli maana na huyo jamaa alikuwa anajua mimi ndio mzazi halisi wa binti.Na kwa kweli sikuwahi kumwambia kuwa huyu binti alikuwa house girl wangu,japo jamaa anajiuliza undugu wetu na binti unakujaje maana hata makabila ya mke wangu na yangu wala hayafanani na binti.Hilo tumeliweka kapuni.
Kikubwa kinachonitatiza kwa sasa ni kuwa baba na mama wa binti hawataki kabisa kupokea mahari ya mtoto wao.Kama baba yake ndio kakataa katakata kuwa hataki kabisa kupokea hiyo hela sababu huyo mtoto aliniachia mimi toka akiwa mdogo.Mama ndio anasema yeye aitwe tu siku ya harusi basi,mambo ya mahali na mengine tumalize mimi na familia yangu sababu wao walishanipa huyo mtoto toka akiwa mdogo na hajawahi hata kurudi kwao na kusema kashindwa kuishi kwetu.
Mtihani huu umekuwa mgumu sana kwangu sababu kwanza wale ndio "biological Parents" wa huyu binti,tena bado ni wazima na wana afya tu japo ni wazee.Lakini nawaza hii ya kupokea mahali kwa mtoto sio wako ina uhalali kweli?Naweza kutumia mbinu gani kuwashawishi hawa wazee wapokee mahali ya mtoto wao ambayo ni stahili yao?Na je huyu jamaa muowaji hakuwahi kujua mahusiano yangu na huyu binti kuwa ni hosue girl wangu wa zamani na hudhani ni mwanangu au ndugu yangu,je swala hili la wazazi kukataa kupokea mahali haliwezi kutapakaa na kumfikia jamaa na hivyo kuona kama kuna jambo alifichwa?
Nimejaribu kutumia wazee kijijini kwa huyu dada lakini bado wamegonga mwamba,mimi nawiwa vigumu sana kupokea mahali hii,najiona sistahili kwa lolote ingali wazazi wake wapo hai.Nipo njia panda.