Wazazi wa Binti wagoma kupokea Mahari

Wazazi wa Binti wagoma kupokea Mahari

sir kiduku

Senior Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
101
Reaction score
262
Nitangulize samahani zangu kwa wakubwa nitakao wakwaza lakini uzi huu ni kutaka ushauri tu hvyo naomba mawazo yenu

Iko hivi niko kwenye mahusiano na binti mmoja kwa muda wa miaka mi 3 sasa,
Tulianza mahusiano tukiwa mkoa mmoja (X), then yeye alipata kazi mkoa mwingine (y) ila ni mikoa karibu nauli n 8-10k tu

Mkoa huu (X) ndipo familiya yake ilipo (ambao ni ndugu zake anapo binti, yeye mzazi wake mmoja ameshatangulia mbele za haki hivyo yuko na baba tu aishie mkoa (Z)

Hivyo kwa muda wote huo wa mahusiano tuliweka mipango mbali mbali na tulikuwa tunaweza kutana hata kabla yeye ya kuwa na likizo alikuwa akija huu mkoa (X)ambapo pia ndugu zake wapo tunakutana maana mimi pia nilikuwa naish mkoa huo huo

Sasa shida imekuja tokea pale nilipo taka kuanza taratbu za kupeleka mahari kwa mzazi wake mkoa(Z)
Ndipo ndugu yake mwngne(binti hakai kwa huyu ndugu) amabye naye anishi mkoa (X) akaanza kupeleka taarifa kwa ndugu zake wengne na mzee wake kuwa nilishawahi kukutana na huyo binti kimwili na alishawahi kulala kwangu, taarifa hizo alizipata kwa msismamizi wa binti alipokuwa anafanyia kazi mkoa (y)

Ila hawakuwa wanauhakka kuwa ni kweli au laa ndio maana sisi hatukuwa na woga wa kuendelea na ratiba nyngne za mahari

Aliwaambia wasipokee mahari yangu na mambo mengne yasieendelee kwasababu mimi sifai kuwa na binti yao ni kama simuheshimu binti yao (NB:binti sijamkuta kigori na pia mahali walikuwa wamenipangia 3M, lakini baada ya presha hiyo kuwa kubwa wamekataa nisiipeleke hawatopokea)

Ila nilikuwa nimeshatoa posa kwa ndugu anapoish binti masna hayo ndiyo yalikuwa maelekezo ya mzee wake aishie mko (Z)

Tulitarajia baada ya kutoa Posa ndo tuende kwa Mzee wa binti na washenga wangu tukatoe mahari, ila ndugu yake akaamua kuanzisha hayo mengine

Msimamo wa binti ni kutaka kuwa na mimi ila ndugu zake ndio hawataki kusikia hilo
Naombeni mawazo yenu wakuu
 
Ukikataliwa ukweni tulia usilazimishe, kaa mbali na huyo Binti. Inawezekena vipi baba mzazi aulize kama umeshawahi kumlomba Binti yake? Hapo hakuna familia mkuu.
Baba mzazi hajaulizia, ila ndugu yake ambaye ni shangazi yake tuliye naye huu mkoa mimi nilipo ndo ameamua kufikisha hizo taarifa kwa baba wa binti, hivyo mzee akaona nisiendelee na binti yake
 
Kaza moyo achana na hiyo familia Mkuu, kama Shangazi na baba wa binti wameungana kukukataa hiyo siyo red flag bali ni red flag pro max, angekua mama tungesema ana maslahi na binti yake uingie kibishi ila kwenda kushindana na upande wa mzee wa binti wanaweza wasije hata kwenye ndoa yako, matukio makubwa yote kwenye ndoa au situations nyingine huwa yanaanza na series of events sasa wewe umeanza na tukio bado show utaipata ukikaza kichwa
 
Back
Top Bottom