Wazazi tuungane kuipinga Bodi ya Mikopo

Wazazi tuungane kuipinga Bodi ya Mikopo

Stream line

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2015
Posts
393
Reaction score
243
Ndugu zangu wazazi wa tanzania. Sote tu walipa kodi kwanini bodi inaanza kutubagua. Kama mtanzania anaomba mkopo ambao atarudisha. Basi ni kwa nini aanze kuchambuliwa? Tuungane kulipinga hili. Wanetu tuliwasomesha shule za binafsi walipokuwa ma festiboni. Sasa tunao wengine nyuma na tunahitaji kujenga mabanda kwani tunazeeka.

USHAURI: ili pesa ipatikane kwa wingi bodi (naamini walimu mmo) ielekezeni TRA njia nyepesi ya kutoa elimu kwa mlipa kodi. Mf. Bidhaa inayouzwa kwa sh. 30,000/= kodi yake ni sh.5,400/= usipodai risiti sh. 5400 inaibiwa/umemwongezea muuzaji.

Asanteni
 
Serikali zote huwa hazina pesa kwani hazifanyi biashara. Wenye pesa ni wananchi wake. Ndo maana utaona kuna makundi ya nayoitwa WAASI. kila siku wako vitani japo hawazalishi. Pesa yao hutokana na wananchi wao. Walioko Ndani na nje ya nchi
 
Anzisha uone cha moto, mwenyewe ashajisemea hajaribiwi~ acha tuisome namba na atatunyoosha kweli kweli
 
Serikali zote huwa hazina pesa kwani hazifanyi biashara. Wenye pesa ni wananchi wake. Ndo maana utaona kuna makundi ya nayoitwa WAASI. kila siku wako vitani japo hawazalishi. Pesa yao hutokana na wananchi wao. Walioko Ndani na nje ya nchi
Kama Serikali ya Tanzania haifanyi biashara, pale kigamboni na madarajani zile tozo ni za nini?

Hospitalini unatibiwa bure wewe?
 
Tunaipingaje???
Nadhani tuna wawakilishi wa kutusemea, tuwatumie hao
 
1.Namna pekee ni kudai risiti. Kelele zote za ukata zitaisha.
2. Hata hivi kutoa maoni itasaidia.
3. Kuipinga si kuandamana. Waikumbuke kauli ya rais kuusu mikopo wakati wa uchaguzi.
 
Waziri kasema fedha zilizopo zinatosha kusomesha watoto 110,000. Watoto waliodahiliwa ni 66,000. Waliopata mikopo ni 25,000: wanapowanyima watoto fedha wanataka kuziwekeza wapi?
 
Pesa ipo. Si pesa yote inayokusanywa inatangazwa. Vyanzo vingine ni siri. Ila miscelloneus money ndiyo inayotangazwa. Ndo maana tunalipia deni for75% na bado tunafanya mengi tu. Amka,!,,!!!!
 
Bodi hii ukiiangalia inapingana na ahadi za rais. Mwomba mkopo si mzazi vile vile mlipaji. Ila ni mtanzania ambaye ni mjenga nchi wa kesho. Wanabodi wamenitia wasiwasi sana hasa kitaaluma. Hasa pale waliposema ETI WAKOPESHWAJI WANANUNUA TV, MUSIC SYTEAMS, NK. Mkopaji wanafunzi hata akinunua nyumba ni haki yake. Kazi ya bodi ni kutoa pesa.
 
Back
Top Bottom