Wazazi mmekuwaje?

Mabinti wote niliograduate nao chuo na kuolewa haraka wanaishi maisha duni. Cha ajabu wote walikuwa watumishi na watu wa imani, kasoro gumegume mmoja aliolewa na mzungu kibabu ana miaka kama 65 wako Marekani kwa sasa.

Hao walioolewa hawajapata kazi hadi sasa, na maisha sio mazuri kivile ukizingatia elimu yao hawajaitumia ama kuajiriwa ama kujiajiri. Kuna ambao nina ushahidi wanajutia na mwingine nimemchangia gharama za hospitali.

Mtu kamaliza chuo hajaenda intervie yoyote, hajaajiriwa au kujiajiri. Huyo mbio kafunga ndoa. Hapo ana honeymoon, akitoka analea mume, akitoka anapewa mimba, analea mimba, anajifungua, analea kichanga. Baada ya hapo tiyari hatakiwi kukaa mbali na mtoto, hawezi tena kuwa free kwenda interview siku ya interview mtoto anaamka anaharisha.

Unakuta hamna hamna miaka miwili imekatika wapo tu hamna hatua wamefanya. Familia changa inakula hela balaa, gharama za maisha zimepanda. Mke elimu anayo ila kazi hana.

Nashauri binti ukimaliza chuo focus kwanza kuwa na chochote cha kuingiza kitu. Ajiriwa kwanza, hivi nani atakuajiri private sector ukiwa na mtoto wa miezi 6 kila siku una dharura? Alafu entry level opportunities zina mizunguko mingi huiwezi ukiwa na ndoa changa na watoto wadogo.
Kazi za serikali chache. Unless uhakikishe unayeolewa naye anaweza cover kila kitu, mna nyumba na bima na cashflow ya kueleweka.
 
Umemaliza kila kitu. Hata mimi nina ushuhuda wa mabinti wengi wanaoishi kimaskini kwa kuharakia ndoa.
 
Destine ya mtoto wa kike awe na kazi au hana kazi ni kupata mme! Stability ya binti ni mme! Utake/usitake hata kama wewe baba uko vizuri lakini ukiona binti yako yupo yupo tu ni shida! Tatizo ni kupata mme sahihi vinginevyo akiangukia kwa wavuta bangi ni shida zaidi!
 
Kuna binti nadhani mtakuwa mnalingana nae kamaliza degree miaka 4 iliyopita, alitaka sana kuolewa na milionea ili atukomeshe macuzooo ni wiki iliyopita tu kanipigia anatafuta mume walau mwenye elimu na kazi ya kuzugia,🤣🤣 anataka mbinu za kumnasa mwanaume wa kumpa heshima ya ndoa nyie dunia iko speed, yuko very desperate kwa sasa anahaha hadi huruma nyodo zote zimemuisha

Kama hauko tayari kuolewa baki hivyo hivyo ila huko mbeleni usije sumbua watu km huyo cuzo wangu
 
Hata mtoto wa kiume yuko vizuri kuoa alafu anazingua ni shida! Kijana akiwa na uwezo alafu hana mke kama baba ni shida! Popote uendako! Stability ya kijana/binti ni kuwa na mwenza! Ebu fikiria kijana/binti ana kipato cha kutosha na hana mwenza uwe na uhakika anaishi maisha ya ushetani kusagana, mashangazi/michepuko! Kama wewe mzazi uwezi kulichukulia kwa uzito umeishafail ukiletewa wajukuu wasioeleweka usipige kelele! At least try to do something!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…