Wazayuni wamevamia zaidi ya mara 100 katika mwezi mmoja maeneo matakatifu ya Palestina

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,487
4bk6e21a3ef01e8bvy_800C450.jpg


Waziri wa masuala ya kidini na waqfu wa Palestina amesema, Wazayuni wameuvamia mara chungu nzima msikiti mtukufu wa al-Aqsa na Haram ya Nabii Ibrahim (as) huko Alkhalil katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita.

Yusuf Ad'is, ameashiria mashambulio na uvamizi wa mtawalia wa utawala wa Kizayuni dhidi ya msikiti wa Al-Aqsa na kuwazuia waumini wanaotaka kusali kutoingia kwenye haram ya Nabii Ibrahim huko Alkhalil na kueleza kwamba, wazayuni wameyavamia maeneo hayo matakatifu zaidi ya mara 100 katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita.

Waziri wa masuala ya kidini na waqfu wa Palestina amesema uvamizi wa kila leo unaofanywa na wazayuni dhidi ya msikiti wa al-Aqsa ni miongoni mwa jinai za dhahiri dhidi ya haki za wananchi wa Palestina na kuongeza kwamba mbali na msikiti huo uliobarikiwa pamoja na haram ya Nabii Ibrahim (as), walowezi wa Kizayuni wamevamia pia mara kadhaa haram ya Nabii Yusuf (as) na maeneo mengine matakatifu ya haram za Mitume wa Mwenyezi Mungu huko Ariha na Salfit.

Utawala wa Kizayuni umezuia mara kadhaa kusomwa adhana katika haram ya Nabii Ibrahim kwa kisingizio kwamba inawakera na kuwaudhi Mayahudi.

Ikumbukwe kuwa tangu mwanzoni mwa mwezi Oktoba mwaka uliopita wa 2015 hadi sasa maeneo mbalimbali ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu yamekuwa yakishuhudia wimbi la malalamiko ya upinzani dhidi ya siasa za kichokozi za utawala wa Kizayuni na njama za utawala huo za kupotosha utambulisho wa Baitul Muqaddas pamoja na mpango wake wa kuugawa kiwakati na kimahali msikiti mtukufu wa Al-Aqsa.../

Chanzo: Home - Pars Today
 
Chunguza kwa makini sana hicho chanzo chako cha habari,kwani huo msikiti uko wapi?????
 
Back
Top Bottom