Malungwana
Senior Member
- Sep 14, 2013
- 187
- 99
Kama uliwahi kutembelea Zanzibar au kukaa kwa kipindi fulani, basi utayaona haya:-
1. Wazanzibari halisi (wanavyojiita wenyewe) kwa dhati kabisa hawana mapenzi ndani ya mioyo yao na watu wenye asili ya bara.
2.Wanaamini ndani ya mioyo yao mtu yeyote mwenye asili ya bara, basi hata awe kasoma vipi elimu ya dini ya kiisalam basi hana uwelewa kama ambavyo wao wanataka, na wanasema kua wabara wote ni wa kristo na wengi wao hujibadilisha dini na majina mara tu wakishuka boti pale bandarini Zanzibar!. na ndio maana ukiwa na asili ya bara hata kama ukisalimia Asalaam aleikum.......basi mara wasikujibu au wasiitikie ipasavyo.
3. Wabara hawana haki ya kumiliki ardhi Zanzibar, kwa kua sio kwao.
Hayo na mengi yanaonyesha ni kwa nini watu wenye asili ya bara hawathaminiki Zanzibar, mtu ambae anaonekana kana kwamba hajastaaarabika basi Zanzibar huitwa "mnyamwezi nini" na kuna baadhi ya wabara ambao walishaishi Zanbzibar kwa miaka mingi na wakabadilisha na dini, basi hata kabila zao za asili hua hawazipendi, na hawataki kuonekana ni watu wenye asili ya bara!!! hili ni tatizo lao.
Nilishawahi kumshuhudia mwendesha mashtaka mmoja mahakama ya Mfenesini, alitoa tamko kwa hakimu kua "Mweshimiwa naomba mtuhumiwa asipewe dhamana kwa kua ni mtu wa bara!" dah! nilishangaa sana!.
Kwenye nyumba za kupanga (hasa zinazomilikiwa na wa Pemba) hua hawataki kupangisha wabara (wabongo) kama wanavyoitwa huko Zanzibar, na kama ukipangishwa na ukiwa si muisilamu basi kupiga kwaya ni MARUFUKU!.
Tembelea maduka yote ya mjini Darajani, Stone town, nk, hutakuta duka hata moja anamiliki mtu wa bara, na huthubutu kupewa mlango wa kufungua duka, pale darajani utawakuta wa machinga tu wa kibara wameshika CD mkononi, ila sio maduka makubwa.
Madukani, hasa maduka ya nguo na vifaaa vya electronics, kule Zanzibar kuna bei aina tatu:-
1.Bei ya kwanza ni bei ya wenyewe kwa wenyewe, nina maana kama duka ni la mu Unguja basi ana bei ya mu unguja kwa mu unguja, kama ni la mpemba basi kuna bei ya mpemba kwa mpemba! hii ni bei nafuu sana ni ya wao kwa wao
2.Bei ya pili ni ya kuuziwa mbongo, hii bei utauziwa kwa muonekano tu kua wewe ni mbongo, kwa lafudhi ya kiswahili chako na kwa mavazi yako na jinsi ulivyochomekea shati lako na kuvaa buti ( maana wazanzibari si sana kuchomekea na mara nyingi huvaa sandals!)
3. Bei ya tatu ni yaa kuuziwa wazungu, hii ndi bei kubwa kuliko zote hapo juu.
Wana JF naomba michango yenu katika hili, huu kweli ni uungwana, je na wao wanaoishi huku bara wanatengwa na kufanyiwa kama haya?