Albert Msando
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 1,019
- 171
Zidumu fikra za Mwenyekiti.
Nimeona ni vyema nikaanza na salamu hiyo kwa sababu kuu moja, fikra za Mwenyekiti, Marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere zimedumu kwa muda mrefu hatimaye tumefika mahali sasa hali si hali na wote tunajidai kushangaa yanayotokea.
Ni kwa bahati mbaya sana fikra zake zimeendelea kutuongoza mpaka leo. Huko alipo ameendelea kutuangalia jinsi ambavyo tumezivaa fikra zake kama NIRA na naamini amekuwa akitushangaa kwa nini tumeshindwa kuendeleza pale alipoachia yeye.
Binafsi nampongeza Mwenyekiti kwa jambo kubwa moja, kuweza kufikiri na kutekeleza kile alichofikiri. Pia aliweza kuaminisha umma kwamba alichofikiri ni bora kwa ustawi wa umma. Kwa sasa hivi sina wa kumpongeza kwa kufikiri na kutekeleza anachofikiri.
Lakini, fikra zake na utekelezaji wake una mambo mengi tu. Mabaya na Mazuri. Kwa wale ambao bado wanamuamini hata katika kifo mabaya ni hakuna. Kama yapo hayakuwa yake.
Ila, nina machache ya kuweka hapa jamvini.
Kuna mama mmoja ameshitaki viongozi wa kijiji fulani. Viongozi hawa walikuwa ni wajumbe wa kamati ya ugawaji ardhi miaka ya 1970 wakati wa Operation Vijiji. ardhi yake iligawanywa kwa wanakijiji wengine. Baada ya miaka zaidi ya 15 akafungua kesi. Anadai ardhi yake. Kwenye ardhi hiyo leo kuna shule mbili, makanisa mawili, kaya zaidi ya 500, barabara ya umma, dispensary. Mama huyo alishinda kesi!!! Dalali akaenda kukamata mali wananchi wakaja juu.......Operesheni Vijiji/Ujamaa na Kujitegemea.
Mpaka leo hii bado Katiba yetu inasema;
KWA HIYO, BASI, KATIBA HII IMETUNGWA NA BUNGE MAALUM LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, kwa niaba ya Wananchi, kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo, na pia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania
inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia na ujamaa.
SURA YA KWANZA
JAMHURI YA MUUNGANO, VYAMA VYA SIASA,WATU NA SIASA YA UJAMAA NA
KUJITEGEMEA
Lengo la Katiba hii ni kuwezesha ujenzi wa Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar au wa
chochote kati ya vyombo vyake na udugu na amani kutokana na kufuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, ambayo inasisitiza
utekelezaji wa misingi ya kijamaa kwa kuzingatia mazingira yaliyomo katika Jamhuri ya Muungano. Kwa hiyo, Mamlaka ya
Nchi na vyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha-
Fikra za Mwenyekiti zimeendelea kudumu mpaka leo. Hakuna anayethubutu kuzigusa. Eti bado ni 'nchi' ya kijamaa. Sawa.
Haya, hilo tuache. Kuna hili la Zanzibar na Tanganyika. Alifanya kazi kubwa kuziunganisha nchi mbili ili ziwe nchi moja. Wote tukaamini amefanikiwa na sisi ni wamoja. Tuliamini fikra zake. Hakuna aliyehoji kwa sauti.
Kwa miaka yote Katiba yetu inasema;
1. Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano.
Kwenye utangulizi tukatamka kwa sauti;
KWA KUWA SISI Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki, udugu na amani:
Hapa sisi ni Watanganyika na Wazanzibari! Tuliamini hivyo.
Lakini, Wazanzibari wakaendelea na maisha yao. Wakiamini kwamba wanaonewa na kudharauliwa. Hii si kweli. Wanaonewa na nani?? Wameijenga 'nchi' katika misingi ya uhuru, haki, udugu na amani?
Hilo si la msingi kwa sasa. Tunagalie walichokuwa wanafikiria na kutekeleza.
Katiba ya Zanzibar inasema;
(9)(i) Zanzibar itakuwa ni NCHI ya kidemokrasia na haki za kijamii.
(9)(2)(a) Mamlaka ya kuendesha NCHI ni ya wananchi wenyewe …
(10) Kwa madhumuni ya kuendeleza umoja na maendeleo ya watu na ustawi wa jamii katika NCHI itakuwa ni wajibu wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar:
(10)(3) Itadhibiti uchumi wa NCHI kufuatana na misingi na madhumuni yaliyoelezwa na katiba hii.
(12)(3) Haki za raia, wajibu na maslahi ya kila mtu yatalindwa na kuamuliwa na mahkama pamoja na vyombo vya NCHI na vinginevyo vilivyowekwa na sheria.
(21)(i) Kila Mzanzibari anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa NCHI…
(23)(2) Kila mtu ana wajibu wa kulinda maliasili ya Zanzibar, mali ya NCHI pamoja na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi…
Kwa hiyo basi, Tanzania sio nchi moja kama tulivyokuwa tunaamini. Ni dhahiri hatukuungana kama nchi moja. Zanzibar ilibaki kuwa nchi. Wazanzibari waliendelea kuishi kama nchi muda wote mpaka leo.
Je, sisi wengine nchi yetu ni ipi? Tanganyika iko wapi? Zanzibar ina bendera, raisi, baraza la wawakilishi, vikosi vyake vya ulinzi nk. Sisi?
Kama wao wana maisha yao na nchi yao iweje wanatuchagulia Raisi? Je inawezekanaje raia wa nchi nyingine achague Raisi wa 'nchi' nyingine? Sawa sheria zinaruhusu hilo, je sheria hizo ziko sawa? Na sheria kuu iko sawa?
Sheria Kuu (KATIBA) inatamka kwamba Tanzania ni nchi moja. Katiba ya Zanzibar amabyo nayo ni Sheria Kuu inatamka Zanzibar ni nchi. Sasa hapa ipi ni nchi na ipi si nchi? Hii yote ilianzia kwa Mwenyekiti......MUUNGANO!
Imani yetu imetuponza au imetuponya?
Basi nimalizie na swali, Je Wazanzibari wanashiriki kwenye mchakato wa Katiba Mpya kama raia/wananchi wa nchi gani?? Tanzania au Zanzibar? Sifa ya kushiriki utungaji wa Katiba ni lazima uwe raia wa nchi. Nchi haipo, raia hawapo!
ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI. KISIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.