Wazanzibari Mti na Macho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazanzibari Mti na Macho

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Makaimati, May 11, 2011.

 1. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi sasa, vyombo vya habari takriban vyote vimeshupalia taarifa za kuchomwa moto kwa vibanda vya wafanyabiashara wa kutoka bara, huko Pwani Mchangani, Mkoa wa Kaskazini, Unguja. Jambo hili hivi sasa liko Mahkamani ingawa tayari kuna ambao wameshalitolea hukumu ambayo imeelekea kisiasa siasa. Wako ambao wanainasibisha kadhia hii na huu Muungano wetu na wengine kuhusu kuvunjika kwa maadili ya Kizanzibari jambo ambalo hao wafanyabiasharaha wanahusishwa nalo kama anavyoeleza huyu mzee wa kijiji hicho:

  "Akizungumza kwa njia ya simu mzee wa miaka 70 wa kijiji cha Pwani Mchangani Ame Haji Ame ameilaumu serikali ya wilaya ya kutokana na kupuuza madai ya wananchi ya muda mrefu ambapo wanalalamikia suala zima la kuwepo vitendo viovu vinavyofanywa na wafanyabiashara hizo alizoziita za kikahaba ambapo alisema vitendo hivyo vimekuwa vikishamiri kila kukicha.
  Alisema mbali ya vitendo hivyo kumekuwepo na uhalifu mkubwa na uharibifu wa mazingira yanayofanywa katika maeneo hayo na fukwe kwa wafanyabiashara hao kufanya vitendo vya biashara ya ngono waziwazi jambo ambalo limekuwa likiathiri jamii ya wananchi wa kijiji hicho ikiwa pamoja na mipira ya kondom kuzagaa na kuchezewa na watoto wadogo ambapo serikali ilishauriwa kukomesha vitendo hivyo lakini imekuwa ikisitasita kuchukua hatua. “Ndio wananchi wamekasirika kwa sababu kumekuwa kukifanyika vitendo viovu vya biashara ya ngono na hili tumelitamka muda mrefu kuiomba serikali yetu ya wilaya kuichukua hatua lakini serikali imeshindwa kuchukua hatua madhubuti kukomesha vitendo hivi, sasa huwezi kuwalaumu wananchi kwa sababu ndio wanaothirika na madhila haya na jamii inaendelea kuharibika” alisema Mzee huyo.


  Mimi sitaki kuzungumzia hili kwani kama nilivyotangulia kusema, hili jambo liko Mahkamani.
  Mimi napenda kuwatahadharisha Wazanzibari kuwa wasishabikie hili jambo kwani linaweza kuwa ni bomu la kutega kwa upande wao. Ukitizama wakati lilipokuja, unaweza kuona limechipuka wakati mjadala wa “Muungano” wetu uliposhamiri.
  Vyombo vya habari vya Tanzania vinaweza kutumika ili tuendelee kujadili hili na kuacha lengo letu kuu.

  Kuna kitu gani kibaya kwa Zanzibar kama kuchomwa Qur-an? Ni gazeti gani la Tanganyika lililolivalia njuga kutupa taarifa ya kesi ilivyokwenda? Kuna habari zisiothibitishwa mtendaji wa hayo hayupo hata huko gerezani.

  Mbona hatujasikia Makamo wa Pili wa Rais wala Waziri wa Mambo ya Ndani wala maelezo baada ya habari kugusa uchomwaji wa QUR-AN?


  Ni karibuni tu tuliyaona yaliyotokea Jang'ombe. Mke wa Askari Jeshi kutoka Bara kaibiwa kipochi, shilingi elfu tano na simu ya mkononi, ikapigwa Jang'ombe nzima. Leo Mabanda ya wamachinga yameungua moto limekua suala kubwa kupita kiasi na kubatizwaUbara/Muungano.

  Leo kwanini kuungua vibanda vya wauza ulevi iwe issue kubwa hivi na kuelezwa kuwa ni katika jitihada za kuvunja Muungano?


  Wazanzibari wametiwa majaribuni kwa muda mrefu lakini sasa wameanza kuguswa kwa kuingiliwa mno tamaduni zao.

  Kukurupuka kwa vyombo vya habari kuandika kwamba Wafanyabiashara wa Bara wamechomewa biashara zao ni aina moja ya kupalilia hili suala kiugomvi ili na wao wapate sababu ya kulipiza kisasi.

  Nachelea kusema kwamba kuna kila dalili mbaya dhidi ya Zanzibar huko mbeleni na Zanzibar imesakamwa sana.  Wazanzibari mti na macho, tusije tukafanywa uwanja wa vita
   
Loading...