Matukio ya tindikali zanzibar na mauaji yanatuchafua pia watanganyika maana kimataifa inalipotiwa kama Tanzania ambayo 90% mataifa yanaitambua kuwa ni Tanganyika.
Wazanzibar mbadilike bwana.
Usiwe mbinafsi kiasi hicho kwa kujifanya kujisahaulisha yanayotokea Tanganyika haya yafuatayo yalitokea zanzibar?
1. Kumwagiwa Tindikali kubenea
2. Kuwekewa sumu Mwakyembe
3. Kuuawa kwa Mwangosi
4. Mlipuko wa Bomu kanisani Olasit Arusha
5. Mlipuko wa Bomu Mkutano wa CDM Soweto Arusha
6.Kumwagiwa Tindikali Shehk Arusha
7. Kumwagiwa tindikali mzee wa Home Shooping center
8. kumwagiwa tindikali Musa Tesha
9. Mauaji ya kinyama ya Mwenyekiti wa CDM kule useriver
10. Kuuawa kwa kada wa CCm kule Ndago
11. Kuuawa kwa kada wa CDM kule Igunga
12. Kushambuliwa wabunge wa CDM kule Mwanza
13. kushambuliwa kwa Mbunge Nassar kule Monduli
14. Kuwepo na wauza madawa ya kulevya wanaotambulika lakini hawachukuliwi hatua ingawa rais ana majina yao.
Ukilinganisha matukio ya Zanzibar na kwetu Tanganyika ya kwetu ni mengi sana kwa hiyo kama ni uchafuzi wa Tanzania watanganyika tunaongoza kuichafua Tanzania.