Wazanzibar wanabwekea vivuli vyao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazanzibar wanabwekea vivuli vyao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kavulata, Aug 14, 2012.

 1. kavulata

  kavulata JF-Expert Member

  #1
  Aug 14, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 3,181
  Likes Received: 1,536
  Trophy Points: 280
  Mbwa huwa wanatabia ya kubweka. Mwenye mbwa anafurahi akisikia mbwa wake anabweka sana sana nyakati za usiku akiwa amelela kwakua anapata ishara ya watu, vicheche na vitu vingine vinavyoikaribia nyumba yake. Mwenye mbwa huwa hadharau mbweko wa mbwa wake hasa usiku, mara nyingi atataka kujua kwanini mbwa anabweka. Atatoka nje ama atachungulia dirishani ili kuona sababu ya mbwa kubweka. Bahati mbaya wako mbwa waoga ambao wanabwekea hata vivuli vyao wenyewe na vile vya miti, hivyo kusababisha mashaka yasiyo ya lazima kwa watu waliolala na kufurahia usingizi wao.

  Miaka 46 ya muungano wetu imesababisha mambo mengi na makubwa, miongoni mambo haya ni pamoja na
  1. Watu wa pande mbili za muungano kuoana na kuzaa watoto
  2. Wanzanzibar wengi wamehamia Bara na kufanya biashara, kujenga, kusoma na kufanya kazi hata kwenye taasisi zisizo za muungano bila masharti.
  3. Wazanzibari wanatoa mahitaji mbalimbali toka bara kwenda visiwani bila usumbufu wowote
  4. Wazanzibar wako 1 mil lakini kwenye bunge la muungano wanawakilishwa na wabunge wasiopungua 40 na kushiriki katika kupitisha sheria na bajeti za taasisi ambazo sio za muungano wakati kwao hakuna mbara hata mmoja kwenye baraza lao la wawakilishi.
  5. ....... endelea kutaja! ha, ha,

  Pamoja na mafanikio haya mazuri kwa wazanzibari juu ya muungano wako wazanzibari wanaobweka eti muungano uvunjwe. Binafsi watu wanaotaka muungano uvunjwe ninawafananisha na mbwa wanaobwekea vivuli vyao, hawako serious na makini wa wanachobwekea, wanatupigia kelele tu za kubweka. Kama kweli wako serious wanataka muungano huu ufe basi yafuatayo yatimizwe kwanza:

  1. waanze kwa kuwarudisha visiwani wazanzibari wao wote walioko bara (shaurimoyo, msasani, chumbageni, maofisini, mashuleni, vyuoni, hospitalini, n.k) kwa shughuli mbalimbali kuonyesha msisitizo
  2. Viongozi na wastaafu wao wote wahame bara wakaishi visiwani (kwao), waache kulala bara
  3. Wasuse kuchukua umeme, nyama, mazao toka bara
  4. Wawashawishi wabunge na mawaziri wao walioko bara wajiuzulu mara moja
  5. .... endelea kutaja mi nakohoa na kupiga chafya kwanza, teh

  Kusema tu tufunje muungano bila ya kuanza na mambo haya Maalim Seif na wenzake (Uamsho) wanabwekea vivuli vyao tu, waache kuwasumbua watu waliolala, hiyo ni danganya toto na wala tusipoteze muda wetu kuwasikiliza. Hiyo ni danganya toto. Tunajua hawawezi kuvunja muungano asilani, wajaribu tuone. Wao ndio wanaobunya matunda ya muungano bwana! Wasitutishie ngongoti wala wasitingishe kiberiti chenye njiti kibao
   
 2. i

  iseesa JF-Expert Member

  #2
  Aug 14, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hata bila Muungano WAZENJ wataweza kufanya yote uliyoyataja hapo juu. Hujaona watu walioa wazungu na kuzaa nao watoto? Wazungu hawafanyi biashara hapa Bongo? Kwani wanafanya haya yote kwwa sababu tuna Muungano nao?
   
 3. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #3
  Aug 14, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Yaani unawafananisha Wazanzibari na mbwa. Subiri.......... Kwanza hoja zako hazina mashiko, kajipange upya.
   
 4. kavulata

  kavulata JF-Expert Member

  #4
  Aug 14, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 3,181
  Likes Received: 1,536
  Trophy Points: 280
  Globu Mnatukosesha raha, mara mnataka katiba, wimbo wenu, bendera yenu, FIFA, kiti UN, nk. huku ni kubwekea vivuli vyenu, ondokeni na watu wenu wote kutoka bara ili waunguja na wapemba mkajuane hukohuko. Tunajua wako watu wanaotamani waarabu warudi ZNZ waje na tende na halua za bure
   
 5. peri

  peri JF-Expert Member

  #5
  Aug 14, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  muungano una faida na mapungufu yake kwa pande zote.
  Kikubwa ni kujadili namna ya kuuboresha sio kukimbilia kuuvunja.
  Huko ni kukurupuka.
   
 6. Mabagala

  Mabagala JF-Expert Member

  #6
  Aug 14, 2012
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,465
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  itafika siku tu wataondoka. wape muda wanajipanga
   
 7. Ufunuo

  Ufunuo JF-Expert Member

  #7
  Aug 14, 2012
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  waende wapi? Wtu wenyewe wanazaliana kama nguruwe wataenea huko visiwani? Wataenda kuuana hawa.
   
Loading...