Wazanzibar hawautaki muungano, tunawalazimisha tu

Askarimaji

JF-Expert Member
Jan 28, 2016
257
623
Mashahid wawili waliokuwa wanashuhudia utiaji sahihi wa hati ya mungano kati ya nyerere na Karume waliuliwa kwa kutatanisha, baadae Karume mwenyewe nae akajakuuliwa kwa kutatanisha pia, Baada ya hapo hati ya muungano haujulikani ilipo, ukihoji unaozea jera kama shekh Farid na Mselemu Ally na wenzao.

Khasimu Hanga na Othuman Sharifu, hawa ndio walikuwa mashahid wawili pekee upande wa Zanzibar wakati wa kutia sahihi, waliuwawa kwa kutatanisha, iko picha ambayo inawaonyesha hao jamaa wawili wamesimama kwa nyuma.

Yalifanyika mapinduzi ya kuwauwa waarab na kuwafukuza Zanzibar, baada ya waarab kuuliwa ikafata zamu ya wale vijana wanamapinduzi kuuwawa wao, na sehemu iliyofanyika mauaji ya kuwaua hao vijana ni pale mahara wanapaita ngazi mia.

Hivyo bas yali fanyika mapinduzi ya pili ya kuwaua wanamapinduzi,

Baada ya Karume kuona muungano hauna tija kwa wazanzibar alisema neno ili... " Msihofu wazanzibar... Muungano ni kama koti, likikubana unalivua tu". Baada ya hapo karume akawaita viongozi wake wote warudi nyumbani, akawaambia kuna jambo linatokea visiwani. Hii kauli ndio ilikuwa chanzo cha umauti wake masikini, kabla ata ilo jambo alilosema litatokea ghafla yeye anauwawa. Ni wazi inaonyesha karume alitaka kuua muungano, ghafla akauliwa yeye kabla ya kuua muungano.

Baada ya karume kuuwawa akapewa uraisi Aboud Jumbe, ambae ata yeye pia hakuwa na raha na muungano, alikuwa yupo kama limoti, hana mamlaka makubwa kama raisi, koti la muungano likawa linambana, Jumbe akachukua karatas kuandika kero za muungano awasilishe bungeni Dodoma, akiwa anajiandaa kwenda Dodoma wakati anapaki makablasha yake vizuri, anaitafuta ile karatas ya kero za muungano haioni, kaitafuta kila kona haioni, akaona isiwe tabu yapo kichwani nitayaeleza, ile anafika Dodoma tu ile karatasi iko mezani kwa Nyerere. Jumbe anajiuliza nyerere kaipataje ile karatasi, mara ajenda anabadilika bungeni anaanza kujadiliwa yeye pale bungeni, mbaya zaidi anaambiwa toka nje tukujadili, aya mambo yote Jumbe ameyaelezea katika kitabu chake cha The Patnership.

Raisi wa nchi anatoka nje kujadiliwa, alikuja kwa ving'ora sasa anatoka nje kujadiliwa na mwishowe anapigwa chini nafas inashikwa na mtu mwingine Idrisa Abdul wakil,

Abdul wakil akaanza kupata shinikizo kwa vijana wake wakina Seif sharif Hamad juu ya kero za muungano, hatimae kikaitishwa kikao cha CCM Dodoma....mwisho wa kikao wanafukuzwa CCM Seif Sharif Hamad, Hamad Rashid na Shabani Mlowe, Walifukuzwa kwasababu waligusa muungano.

Pia huku kwetu bara kuna mtu mmoja nae alishindwa kuuelewa muungano Anaitwa Njeru Kasaka na genge lake la G55 walipeleka mswaada bungeni kuhoji je serikali ya Tanganyika ilifia wapi? Nae yule bwana yakamkuta makubwa, mpaka leo hajulikani yuko wapi.

Wazanzibar wakaona labda wafikishe kero zao katika huu mchakato wa juzi wa katiba mpya, ila cha kuuzunisha sasa sheria ya mswaada wa mabadiliko ya katiba inasema marufuku kujadili Muungano
Swali linakuja.... Kuna nini katika muungano? Mbona kila anaepagusa hapa linamkuta kubwa? Kuna siri gani?

Uamsho ni wazanzibar, walisikika uamsho wakisema kuwa " sisi wazanzibar hatuja ungana bali tumetawaliwa, dunia nzima hakuna muungano kama huu" uamsho waliibuka kuamsha wazanzibar wote, na wakasikika, Uamsho wana haki na nchi yao na walisimamia haki kitimilifu, Mwisho wa siku mashekh wote wa Uamsho wako ndani mpaka leo sababu ni kuugusa muungano, Uamsho walitaka sheria iruhusu muungano kujadiliwa, pili walitaka iitishwe kura ya maoni kujua wazanzibar wangapi wanautaka muungano, wangapi hawautaki muungano, Uamsho wakina Mselem Ally, Farid hadi, Ostadh Mussa Abdallah, Shekh Azad na wengine kibao mpaka sasa wanaozea jera.

Raisi wa Zanzibar akija huku bara anakuwa kama mjumbe wa baraza la mawaziri,
Raisi wa Zanzibar hawezi kuingia mikataba yoyote ya nchi, lazima aje huku amshauri bwanamkubwa. Wazanzibar wamelijua hili na linawakera sana, hawautaki muungano tunawalazimisha tu.

Note: Usijihusishe na mijadala wala harakati kuhusu Muungano, Utakwenda na maji.
 
umeandika ujinga mwingi kwani unafikiri hata sisi wabara tunautaka huo muungano hao mashahidi unaowataja waliuawa na wazanzibar wenyewe na huyoKarume aliuawa na wazanzibar wenyewe kwa sababu wanazojua wao wenyewe msituletee chuki zenu huku ziishie hukohuko
 
Kama wazanzibar wanataka kuvunja muungano kitu cha kwanza wanachotakiwa kufanya ni kutafuta strong candidate agombee urais wa Jamhuri ya muungano. Wakishaikamata dola, kupitia huyo raisi wanaweza kufanya mchakato wa kuvunja muungano. Vinginevyo rais wa Jamhuri siku zote atakuwa kikwazo katika kusikiliza matakwa yao, ikumbukwe rais wa Jamhuri amepewa madaraka makubwa sana kulinganisha na rais wa Zanzibar.
 
Muungano hauna tija kwa pande zote mbili, sasa sijui nn kilichonyuma ya pazia. Maana inaonekana viongoz tu ndo wanajua wanachovuna kwenye muungano. Pia ndoto za kua wazenj, wataweza chagua rais wao sahau kwan kila atayeingia razima awe pandikiz
 
Mahzib Ndio hawaitaki ila wapo wachache mno
Wazanzibar kwa umoja wao hawautaki ukoloni ukiondoa wazanzibara waliopo visiwani kama Muungano huu ulikataliwa na mwanakindakindaki wa ASP Shujaa ABOUD JUMBE MWINYI mpk mkamuweka kifungoni kidole cha kuwaoneshea mahizb umekitoa wali Watanganyika silaha yenu ya kutugawa tushaishtukia wazanzibar tymesimamama pamoja
 
umeandika ujinga mwingi kwani unafikiri hata sisi wabara tunautaka huo muungano hao mashahidi unaowataja waliuawa na wazanzibar wenyewe na huyoKarume aliuawa na wazanzibar wenyewe kwa sababu wanazojua wao wenyewe msituletee chuki zenu huku ziishie hukohuko
Wazanzibar wengi wameuliwa na watanganyika plus hao waaasisi wa muungano wenyewe
 
Kama wazanzibar wanataka kuvunja muungano kitu cha kwanza wanachotakiwa kufanya ni kutafuta strong candidate agombee urais wa Jamhuri ya muungano. Wakishaikamata dola, kupitia huyo raisi wanaweza kufanya mchakato wa kuvunja muungano. Vinginevyo rais wa Jamhuri siku zote atakuwa kikwazo katika kusikiliza matakwa yao, ikumbukwe rais wa Jamhuri amepewa madaraka makubwa sana kulinganisha na rais wa Zanzibar.
Huko ni kuzunguka akitokea rais wa Zanzibar aliekua strong tuu muungano huu unaenda na maji
 
Muungano huu unawanufaisha wengi japo hata hawa wadogo waliowekeza huku bara.

Sidhani uwekezaji walioufanya huku watapenda upotee hivi hivi kisa watu fulani hawataki muungano..!!.

Hata jirani yangu mzanzibari amevuka mikoa kibao mpaka kuja kujenga huku Kaskazini sidhani kama atakubali kuondoka muungano.

Ni wachache tena wanaotumwa ndiyo hawautaki, nahisi wanatumiwa na familia flani za walio arabuni.
 
Umesema usijuhusishe kuuzungumzia au kuulizia utapotea sasa mbon wewe ueuzunguzia huogopi kupotezwa
Mashahid wawili waliokuwa wanashuhudia utiaji sahihi wa hati ya mungano kati ya nyerere na Karume waliuliwa kwa kutatanisha, baadae Karume mwenyewe nae akajakuuliwa kwa kutatanisha pia, Baada ya hapo hati ya muungano haujulikani ilipo, ukihoji unaozea jera kama shekh Farid na Mselemu Ally na wenzao.

Khasimu Hanga na Othuman Sharifu, hawa ndio walikuwa mashahid wawili pekee upande wa Zanzibar wakati wa kutia sahihi, waliuwawa kwa kutatanisha, iko picha ambayo inawaonyesha hao jamaa wawili wamesimama kwa nyuma.

Yalifanyika mapinduzi ya kuwauwa waarab na kuwafukuza Zanzibar, baada ya waarab kuuliwa ikafata zamu ya wale vijana wanamapinduzi kuuwawa wao, na sehemu iliyofanyika mauaji ya kuwaua hao vijana ni pale mahara wanapaita ngazi mia.

Hivyo bas yali fanyika mapinduzi ya pili ya kuwaua wanamapinduzi,

Baada ya Karume kuona muungano hauna tija kwa wazanzibar alisema neno ili... " Msihofu wazanzibar... Muungano ni kama koti, likikubana unalivua tu". Baada ya hapo karume akawaita viongozi wake wote warudi nyumbani, akawaambia kuna jambo linatokea visiwani. Hii kauli ndio ilikuwa chanzo cha umauti wake masikini, kabla ata ilo jambo alilosema litatokea ghafla yeye anauwawa. Ni wazi inaonyesha karume alitaka kuua muungano, ghafla akauliwa yeye kabla ya kuua muungano.

Baada ya karume kuuwawa akapewa uraisi Aboud Jumbe, ambae ata yeye pia hakuwa na raha na muungano, alikuwa yupo kama limoti, hana mamlaka makubwa kama raisi, koti la muungano likawa linambana, Jumbe akachukua karatas kuandika kero za muungano awasilishe bungeni Dodoma, akiwa anajiandaa kwenda Dodoma wakati anapaki makablasha yake vizuri, anaitafuta ile karatas ya kero za muungano haioni, kaitafuta kila kona haioni, akaona isiwe tabu yapo kichwani nitayaeleza, ile anafika Dodoma tu ile karatasi iko mezani kwa Nyerere. Jumbe anajiuliza nyerere kaipataje ile karatasi, mara ajenda anabadilika bungeni anaanza kujadiliwa yeye pale bungeni, mbaya zaidi anaambiwa toka nje tukujadili, aya mambo yote Jumbe ameyaelezea katika kitabu chake cha The Patnership.

Raisi wa nchi anatoka nje kujadiliwa, alikuja kwa ving'ora sasa anatoka nje kujadiliwa na mwishowe anapigwa chini nafas inashikwa na mtu mwingine Idrisa Abdul wakil,

Abdul wakil akaanza kupata shinikizo kwa vijana wake wakina Seif sharif Hamad juu ya kero za muungano, hatimae kikaitishwa kikao cha CCM Dodoma....mwisho wa kikao wanafukuzwa CCM Seif Sharif Hamad, Hamad Rashid na Shabani Mlowe, Walifukuzwa kwasababu waligusa muungano.

Pia huku kwetu bara kuna mtu mmoja nae alishindwa kuuelewa muungano Anaitwa Njeru Kasaka na genge lake la G55 walipeleka mswaada bungeni kuhoji je serikali ya Tanganyika ilifia wapi? Nae yule bwana yakamkuta makubwa, mpaka leo hajulikani yuko wapi.

Wazanzibar wakaona labda wafikishe kero zao katika huu mchakato wa juzi wa katiba mpya, ila cha kuuzunisha sasa sheria ya mswaada wa mabadiliko ya katiba inasema marufuku kujadili Muungano
Swali linakuja.... Kuna nini katika muungano? Mbona kila anaepagusa hapa linamkuta kubwa? Kuna siri gani?

Uamsho ni wazanzibar, walisikika uamsho wakisema kuwa " sisi wazanzibar hatuja ungana bali tumetawaliwa, dunia nzima hakuna muungano kama huu" uamsho waliibuka kuamsha wazanzibar wote, na wakasikika, Uamsho wana haki na nchi yao na walisimamia haki kitimilifu, Mwisho wa siku mashekh wote wa Uamsho wako ndani mpaka leo sababu ni kuugusa muungano, Uamsho walitaka sheria iruhusu muungano kujadiliwa, pili walitaka iitishwe kura ya maoni kujua wazanzibar wangapi wanautaka muungano, wangapi hawautaki muungano, Uamsho wakina Mselem Ally, Farid hadi, Ostadh Mussa Abdallah, Shekh Azad na wengine kibao mpaka sasa wanaozea jera.

Raisi wa Zanzibar akija huku bara anakuwa kama mjumbe wa baraza la mawaziri,
Raisi wa Zanzibar hawezi kuingia mikataba yoyote ya nchi, lazima aje huku amshauri bwanamkubwa. Wazanzibar wamelijua hili na linawakera sana, hawautaki muungano tunawalazimisha tu.

Note: Usijihusishe na mijadala wala harakati kuhusu Muungano, Utakwenda na maji.
 
Muungano huu unawanufaisha wengi japo hata hawa wadogo waliowekeza huku bara.

Sidhani uwekezaji walioufanya huku watapenda upotee hivi hivi kisa watu fulani hawataki muungano..!!.

Hata jirani yangu mzanzibari amevuka mikoa kibao mpaka kuja kujenga huku Kaskazini sidhani kama atakubali kuondoka muungano.

Ni wachache tena wanaotumwa ndiyo hawautaki, nahisi wanatumiwa na familia flani za walio arabuni.
Wazanzibar wameekeza Kenya Uganda wapo Ulaya na Amerika hivyo itabidi tuungane na wote hao kwa mujibu wa comment yako
 
Siyo kwa mujibu wa comment yangu sema HUJAELEWA KITU, hapa tunazungumzia muungano kijana wangu, hebu jiongeza "kuwekeza ukiwa raia wa nchi husika na kuwekeza ukiwa uhamishoni.."

Back
Top Bottom