Nafaka
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 12,157
- 31,334
Jamaa akiwa katika safari yake ya kuelekea nci ya ahadi (Spain) alikutana na msafiri mwingine anaitwa John. Wote walikuwa wana lengo la kufika Libya kwanza. Unaambiwa kwa mwaka huo 1998, Libya ilikuwa kama Eldorado (Mji wa dhahabu). Ilikuwa ni nchi ya fursa na wasafiri kafiri kama jamaa, pale ndipo lilikuwa eneo la kupata kazi ili akusanye pesa ya kuendelea na safari. Kwa wengine ilikuwa ni sehemu ya kupita ukiwa unaelekea Ulaya.
Kwakuwa hii safari hakuianzia nyumbani kwao, maana kwao aliondoka tu akiwa anakimbia asiuawe na kaka yake, hivyo akakimbilia Gunnea Bissau. Sasa baada ya kukutana na John na kushauriana kwamba waende Libya, ilikuwa haina budi kurudi Cameroon kwanza. Hivyo walirudi mpaka mji wa Younde, Cameroon na kisha kuchukua usafiri wa gari moshi mpaka Kaskazini mwa nchi ya Cameroon. Anasema kwa kipindi kile eneo hilp lilikuwa ni hatari sana, kulikuwa na watu wenye silaha ambao walikuwa wakiua sana wasafiri na kisha kuchukua mali zao. Hivyo safari yao ilikuwa ni ya siku kadhaa na walikuwa wameambatana na wanajeshi waliokuwa wakihakikisha ulinzi mpaka walipofika kwenye mpaka wa Chad na Cameroon. Anakumbuka siku hiyo ilikuwa ni Ijumaa, na ilibidi walale pale mpakani.
Anasema siku iliyofuata, ambayo iliuwa ni Jumamosi, waliamua kuvuka mpaka waende upande wa pili yai waingie nchi ya Chad. Kama ilivyo mpakani, watu wa Cameroon walikuwa wakivuka kuingia Chad na Wachad wakiingia Cameroon kwa wingi, eneo la hapo mpakani linajulikana kama Chad pont Guelli.
Jamaa na John nao wakaungana na watu wengine na kuanza kusonga mbele kuvuka mpaka. Walikuwa wamekaribia kuingia Chad, mara ghafla jamaa anazuiwa na mwanajeshi. Jamaa anahisi labda mwanajeshi hamwiti yeye, lakini mwanajeshi anasisitiza wewe hapo kisha anachomoa bastola na kumsogelea. Alipomfikia anaielekeza kichwani kwake na kumwambia rudi ulikotoka au nikupasue kichwa hapa hapa.
Watu wote walipigwa butwaa, John yeye kuona vile akasonga mbele kama vile hamjui jamaa. Jamaa alikuwa anajua kuwa wanajeshi wa Chad hawana masihara, aligeuka na kuanza kutembea kurudi alikotoka. Moyo wake ulikuwa ukienda kasi lakini alisonga mbele na kurudi upande wa Cameroon.
Mara anatokea mzee raia wa Chad na kumwambia; pole sana kwa alichpkufanyia mwanajeshi wan chi yetu.
Jamaa anamjibu; Siyo muungwana na sijui kwanini kanizuia mimi tu kuingia.
Yule, mzee anamwambia kuwa wao ni ndugu, na kama anataka kuvuka anaweza kumsaidia lakini itamgharimu 10,000 CFa.
Jamaa nampatia kiasi hicho na kisha mzee anaondoka. Jamaa alikuwa anawaza kuwa John atakuwa anamsubiri upande wa pili.
Baasda ya dakika kadhaa alirudi na kumwambia amfuate nyuma. Wanafuatana na anamvusha mpaka upandee wa pili yani Chad. Lakini baada ya kuvuka ajabu anashangaa kutomuona John.
Chad ni sehemu yenye joto kali kwakuwa sehemu kubwa ni jangwa inaweza kufika hadii nyuzi joto 65. Jamaa akawa anajihisi mpweke, rafiki yake hamuoni. Akawa anawaza labda atakuwa kwenye kituo cha mabasi yanayoenda Libya. Jamaa anaenda kituoni lakini hamuoni. Yeye ndiye alikuwa kagharamia safari yote kutoka Guinnea mpaka mpakani na sasa aikuwa kabakiwa na pesa kidogo sana. Huenda jamaa ndiyo maana hakumsubiri.
Jamaa akiwa kabaki peke yake katika safari ya kuvuka Jangwa la Sahara huku akiwa na pesa kidogo. Kijiji cha Faya Largeau kiko Kaskazini mwa Chad, ndicho kijiji cha mwisho kabla ya kufikia kwenye na mpaka wa Chad na Libya. Ili kufika Libya kutoka Chad ni safari ya siku sita mkipita jangwani. Na hapo ni kuomba Mungu kusitokee tatizo lolote. Jamaa analipa pesa kwa ajili ya safari, na kabla ya safari inabidi ujiandae kwa chakula na maji ya kutosha. Wakati akiomba ushauri kwa watu juu ya nini abebe wakati wa safari, walikuwa wakimshauri kama hana jambo la muhimu ahairishe safari wakimwambia kuhusu hatari anayoweza kukabiliana nayo jangwani. Jamaa akaona kwani kama wegine waliweza mimi nashindwaje, liwalo na liwe twende.
Kwakuwa hakuwa na pesa, alikuwa amenuia lazima afike walau Faya Largeau. Kutokana na hamu ya kuingia Libya jamaa alikuwa hatafakari tena. Siku ya kusafiri ilikuwa imefika na watu mbalimbali walikuwa wakikusanyika. Usafiri ulikuwa ni pick up na aligundua kuwa kati ya wasafiri wakikuwepo Wacamerron wengine. Alifurahi sana kukutana na Wacameroon wenzake ambao aliwaona kama ndugu zake na kujihisi hayuko peke yake safarini.
Safari ilianza usiku na walianza kuzama ndani zaidi ya janwa. Kama lilivyo jangwa usku baridi sana , na siu ya kwanza nay a pili ya safairi haikuwa mbaya sana. Siku ya tatu wakaanza kushuudia mambo ya kutisha janwani. Anadai upepo wa janwa unakuwa kama unazungumza na mchanga kuruka kamandee angani. Anasema safar ilikuwa inachosha sana na kila kona kumetapakaa mifupa ya wanyama.
Siku ya nne kuna mahali ilikuwa inabidi wateremke kusukuma gari likikwama kwenye mchanga. Hivyo iliwalazimu kutembea sana. Anadai wakati wakitembea huku wakisukuma gari mmoja wao alianguka akazimia. wakadhani labda kachoka wakajaribu kumpa huduma ya kwanza ila kumbe ndo alikuwa kafa hivyo. Jamaa anasema alianza kuona hatari na kuanza kuhisi watakufa mmoja baada ya mwingine.
Jamaa anasema Biblia inasema Jehanamu ni sehemu ya kutisha ambapo binadamu wenye dhambi wanaadhibiwa bila kikomo, ila anadai kwa upande wake Jehanamu inaweza kuwa sehemu yoyote duniani na kwa wakati huo alihisi yuko jehanamu. Wakichimba kaburi na kumfukia kisha wakaendelea na safari.
Walifika Kijiji cha Faya kilichopoKaskazini mwa Chad, Ni sehemu iliyo na watu wachache sana. Jamaa hakuwa na pesa ya kuendelea na safari mpaka Libya, hivyo walimuacha pale. Kabla ya kuachawa alijaribu kuwaomba wale wa Cameroon wawili wamlipie nauli wakagoma. Kuna msafiri mmoja raia wa Chad, akawambia kwamba kama mkimuacha mwenzenu hapa mjue atakufa lakini hawakujali.
Aliachwa hapo Faya Largeau, sehemu iliyopo katikati ya jangwa. Hakuna maji na hakuna shughli yoyote ya kilimo. Watu wa pale wanategemea kuishi kwa kunywa maziwa, hakuna shule wala hospitali, ispokuwa maduka machache. Hakukuwa na shughuli yoyote ya kufanya eneo hil na pia hakuwa na sehemu ya kwenda kujihifadhi. Akiwa anazungukazunguka, aliwaona mbuzi wakila karatasi kwa kukosa majani.
Jamaa alikuwa akilala nje ya duka kila siku. Siku moja akiwa kalala, ng’e alimng’ata. Jamaa alikuwa nagumia maumivu ya sumu amekata tamaa, ndipo bibi kizee alikuja kumsaidia. Alimshikilia na kufyonza sumu tokakweye jeraha. Jasho lilikuwa likimtoka na kapoteza nguvu na macho yakiwa yamepoteza nuru.
Akawa anasikia watu wakiiba na kwa mbali akiona sura zao zikimtazama huku zikiwa na tabasamu. Kisha akapoteza fahamu. Kesho yake aliamkaakijiskia afahdali. Aliendeleakukaa pale kwa bibi kwa siku kadhaa. Lakini alikuwa na mawazo na kila siku mwili ulipoteza uzito.
Siku moja akiwa kalala anakuja jamaa anamwambia, amka unifuate. Jamaa ananyanyuka anamfuata bila kuhoji. Jamaa anamfuata Yuma nyuma wanapita gizani na hakujua wanaelekea wapi. Usiku jangwa kinakua kimya lakini ni rahisi kusikia sauti na alikuwa akisikia sauti za magari y
akijongea.
Mara anaona magari yanasimama mbali kidogo na wao. Yule jamaa anageuka anampadumu la maji na kumwambia chukua haya maji ndicho ninachoweza kukupa. Utasafari na hao watakupelekaLibya. Nimewalipa, sisi wafugaji tunaamini katikakusaidia watu bila kujali imani zao, wakuwa sote ni wasafari katika hii dunia. Tafadhali safari salama na Mungu akulinde. Kabla ya kufungua kinywa alikuwa keshapotea.