Wazalisha watumishi hewa kikaangoni

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka Makatibu Tawala wa Mikoa nchini kuchukua hatua kali kwa wote waliosababisha kuwepo kwa watumishi hewa. Amesema suala hilo la watumishi hewa limeisababishia serikali hasara kubwa hivyo ni lazima watu wote waliohusika katika mchakato huo wabainishwe na wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria za utumishi.

Waziri Mkuu, Majaliwa alisema hayo jana alipokuwa akipokea taarifa ya maendeleo ya Mkoa wa Lindi iliyowasilishwa na Mkuu wa Mkoa huo, Godfrey Zambi katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi wilayani Ruangwa .

Waziri Mkuu alisema kazi ya kubaini watumishi hewa inalenga kuokoa fedha za serikali ambazo zilikuwa zinalipwa watumishi waliokufa, kustaafu wengine ni wale ambao wahusika walijiwekea majina na kisha fedha kuingia mifukoni mwa wajanja.

“Makatibu tawala wa mikoa ndio wakuu wa watumishi katika mikoa, hivyo ni lazima tusikie wamechukua hatua gani kwa wote waliosababisha kuwepo kwa watumishi hewa na si kukaa kungoja maagizo ya Rais,” alisema.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zambi katika taarifa yake kwa Waziri Mkuu alisema mkoa huo una jumla ya wafanyakazi watoro 57 na hewa saba ambao ni marehemu, wastaafu waliokuwa wanalipwa mishahara na kuisababishia serikali hasara ya Sh milioni 36 kwa mwezi mmoja.

Alisema kazi hiyo ya kubaini watumishi hewa na watoro itakuwa endelevu. Alisema wameanzisha timu kwa ajili ya kufanya uchunguzi kubaini sababu zilizosababisha watumishi waliokufa au kustaafu kuendelea kulipwa.

Rais John Magufuli wakati akiwaapisha wakuu wapya wa mikoa Machi 15 mwaka huu, aliwapa siku 15 kuhakikisha wanabaini watumishi hewa wote katika mikoa yao na kuwaondoa katika mfumo wa malipo.

Baada ya kufanyika, jumla ya watumishi hewa 7,795 walibainika ambao wameisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 7.5. Fedha zarejeshwa Fedha za mishahara ya baadhi ya watumishi hewa zilizokuwa zikilipwa kwenye halmashauri nchini zimeanza kurudishwa.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Sulemani Jafo alisema hayo juzi wakati akifunga mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa Tanzania (ALAT). Katika mkutano huo, Jafo alisema anazo taarifa za halmashauri moja ambayo imerejesha Sh milioni tano.

Ameagiza fedha zote zinazorudishwa, zikatiwe risiti. Katika mkutano huo, Naibu Waziri alihoji kama zipo halmashauri zilizoanza kurejesha fedha hizo, wakurugenzi wapatao watano walisimama kuthibitisha kufanya hivyo kwenye halmashauri zao.

Hata hivyo, waliposimama kwa sekunde chache, hawakutaja halmashauri zao wakaketi na mkutano ukaendelea. Naibu Waziri alisisitiza wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha watumishi wote hewa wanarudisha fedha walizokuwa wakilipwa.

Alisema hilo ni agizo la Rais John Magufuli na kwa dhamana waliyopewa wakurugenzi, wanapaswa kusimamia kuhakikisha hakuna watumishi hewa kwenye maeneo yao. “Kikubwa zaidi ni kuondokana na suala la watumishi hewa kwani linaipunguzia serikali uwezo katika jukumu lake la kuhudumia wananchi,” alisema.

Kufikishwa mahakamani Wakati Naibu Waziri akihimiza wakurugenzi watendaji kufuatilia fedha hizo za watumishi hewa, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Steven Kebwe, ametaka wafikishwe mahakamani na wakati huo huo fedha hizo zilizolipwa kila mwezi, zirejeshwe.

Mbali na kuwafikisha mahakamani watumishi hao, Mkuu wa Mkoa ameagiza uchunguzi wa kina ufanyike kwa watumishi wengine hewa ambao wanaoneshwa kuwa walistaafu, wagonjwa, waliokufa, kuacha kazi; kutaka taarifa zao ziwasilishwe ofisini kwake kwa hatua zaidi.

Dk Kebwe alitoa agizo hilo hivi karibuni wakati akizungumza na watumishi wa idara mbalimbali za serikali wa halmashauri ya Wilaya ya Kilosa ikiwa ni ziara yake ya kwanza wilayani humo tangu ateuliwe kushika wadhifa huyo.

Alisema katika uhakiki wa watumishi hewa katika halmashauri za mkoa wa Morogoro, waliobainika ni 122 na kwamba ufuatiliaji zaidi unaendelea . “Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa mna watumishi hewa 29 , kati ya hao 17 ni watoro ...nakutaka Mkuu wa Wilaya na ODC, hawa watoro watafuteni wapelekeni mahakamani na warejeshe fedha za serikali zikatiwe ritisi na hawa ni wezi, “ alisema Kebwe.

Alimtaka Mkuu wa Wilaya pamoja na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo kwa kushirikisha vyombo vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa kina kuhusu watumishi ambao wameoneshwa wamefariki, kustaafu , ugonjwa na kuacha kazi ili kubaini ukweli wa jambo hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, John Henjewele, alisema hivi sasa wako makini kuhakikisha hakuna mtumishi hewa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa na ofisi yake kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama vinafuatilia mtandao uliokuwa umezalisha watumishi hewa na eneo mojawapo ni la Idara ya Utumishi.

Akaunti za watumishi hewa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, Idd Mshili, alimwomba Mkuu wa Mkoa kuwezesha kupata zuio mahakamani akaunti za watumishi hewa ziweze kufungwa.

Mshili alisema, katika uhakiki wa watumishi hewa, halmashauri ilibaini kuwa na watumishi hewa wapatao 29 , kati yao, watano ni waliostaafu, sita ni marehemu, mmoja aliacha kazi na watumishi 17 ni watoro.

Alisema halmashauri hiyo ina jumla ya watumishi 3,860 wa kada mbalimbali huku kukiwa na upungufu wa watumishi 1,982 , sawa na asilimia 34 ya mahitaji ya watumishi wote 5,842.

“Pamoja na jitihada za Serikali za kukabiliana na tatizo hili, bado upungufu huu umejitokeza zaidi kwenye sekta za elimu, afya , kilimo na mifugo,” alisema Mshili.


Chanzo: Habari leo
 
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka Makatibu Tawala wa Mikoa nchini kuchukua hatua kali kwa wote waliosababisha kuwepo kwa watumishi hewa. Amesema suala hilo la watumishi hewa limeisababishia serikali hasara kubwa hivyo ni lazima watu wote waliohusika katika mchakato huo wabainishwe na wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria za utumishi

Makatibu Tawala si ni miongoni mwa wazembe ambao hawakulishughulikia hilo mapema? mimi nilidhani vyombo vya usalama serikali kuu ndivyo viwashughulikie hao watu
 
Mh.Raisi ninayo heshima ya pekee kwako kuutambua uthubutu wako wa kizalendo katika kuwatumikia watanzania.Kwakua lengo sio kukupongeza ngoja niende mojakwa moja kwenye lengo mahususi la mada yangu.Pamoja nakwamba umeshapatiwa idadi ya watumishi hewalakini bado hujawaweza hao wajanja wachache wanaoifaidi hii nchi na kuishi kama malaika.Ninaamini kwamba bado wapo watumishi wengine hewa kwa sababu "WALIO BUNI,KUANDAA NA KUTENGENEZA MAZINGIRA YA WATUMISHI HEWA NDIO WALIOPEWA KAZI YA KUBAINI HAO WATUMISHI HEWA"Hiyo ni ajabu,hatari na niudhaifu mkubwa katika mkakati huo mahususi lakiini ushindi kwa wapiga dili hao. USHAURI WANGU MAJINA YOTE YA WATUMISHI HEWA YAWEKWE HADHARANI ILI KWAMBA TUKUSAIDIE MH.RAISIKUPIGANA HII VITA KWANI NI KALI NA WEZI HAWA WANAZOMBINU WATAENDELEA KUHUJUMU NCHI YETU.Nimeshauri hivyo kwasababu miongoni mwetu wapo wanaojua majina ya watumishi hao hewa bali haieleweki kwamba wapo wamebainika ama la kwakua imetajwa idadi na sio majina
 
nasikia dar wanahakiki kichwa kwa kichwa pua kwa pua jicho kwa jicho halafu wanachukua na finger print sasa wale wa afisa utumishi waliowaficha jamaa zao ili waendelee kupiga mtonyo sasa wanahaha kwa kuficha huo ujinga na kwa sasa hawachomoki lazima wanase
 
Naunga mkono asili mia mia moja hoja yako.Ingekuwa vizuri mno kama kila mkoa itoe hadharani majina yote hewa na vyeo vyao hewa walivyokuwa wanatumikia.Utashangaa unaweza kukuta jina la mtumishi hewa ameajiriwa mikoa kadhaa aliwaowahi kufanyia kazi.Mimi nimewahi kufanyia kazi mikoa mitano siajabu ukakuta nimekuwa nikiliwa kila mkia.
 
mpaka sasa idadi ya watumishi hewa imefikia 7700. unashauri ni hatua gani zichukuliwe kwa wahusika, tena wengine ni watumishi wa halmashauri wakiwemo wakurugenzi wa halmashauri na maofisa wa ngazi mbalimbali ndani ya halmashauri.
tunamshauri nini Rais wetu kuhusu hatua za kuchukua.
 
Kuna ajira za kutosha japo kupunguza tatizo la ajira nchini, tatizo ni ulafi na ubinafsi wa wenye mamlaka tu.
 
Mishahara ya wafanyakazi walio kazini zililiwa kifisadi Chuo cha Ufundi Arusha. Je wafanyakazi ambao hawapo kwa kustaafu, kuachakazi nk zitabaki salama?
 
Wapelekwe mahakamani yafunguliwe charge ya uhujumu uchumi, yakikutwa na hati yafungwe na kufilisiwa
 
Inauma sana mijitu inachukua mishahara hewa ilhali huku kitaa kuna madogo wamemaliza vyuo mbali mbali wana nguvu,ujuzi na ari ya kujenga taifa ila hawana ajira na mikopo ya bodi wanatakiwa walipe!

Yaani hao wote ningekamata weka ndani kesi zao wangekua wanazisikiliza wakitokea korokoroni and in the meantime wangekua wanalima vizuri sana kuzalisha chakula kwa ajili ya watanzania waliowaibia miaka tele!
 
Back
Top Bottom