Wawili wafikishwa mahakamani kwa kuisababisha TCRA hasara ya shilingi bilioni 2

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,434
7,067
Wakazi wa Zanzibar, Kalrav Patel(37) na Kamal Ashar (59) wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka saba likiwemo la kusababisha hasara ya Sh 2 bilioni kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa leo amedai kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbroad Mashauri kuwa washtakiwa walitenda makosa hayo 2015 kati ya Mkoa wa Dar es Salaam na Zanzibar.

Washtakiwa hao wanatetewa na Wakili John Mapinduzi wanadaiwa kuwa katika maeneo hayo ya Dar es Salaam na Zanzibar walikula njama ya kutaka kusafirisha vifaa vya mawasiliano bila kibali.

Ilidaiwa kuwa katika kipindi hicho 2015, washtakiwa hao walisafirisha vifaa vya mawasiliano kinyume na sheria za TCRA .

Kishenyi amedai kuwa mbali na mashtaka hayo washtakiwa hao wanakabiliwa na shtaka la kuingiza, kusimika nchini kifaa cha mawasiliano aina ya Voice Over internet protocol (Coop) na kukitumia bila ya kuthibishwa na TCRA.


Chanzo: Mwananchi
 
Hasara ya 2billion?.......TCRA wameanza kufanya biashara gani siku hizi?

Wanaongeza chumvi tu, si rahisi ku-raise revenue kama hizo unapotumia VoIP kwenye mawasiliano actually njia hii ni cheap sana kuitumia kuliko njia nyingine. Hapa wanaichukulia kama kosa la jinai kama kesi ya uhaini!!
 
Back
Top Bottom