Waungwana naomba mnishtue usingizini, mapenzi haya

Geniustin

JF-Expert Member
Mar 15, 2013
4,379
2,829
Wakuu,

Habarini za mapumziko na heka heka za kila siku.

Kuna kitu kinanitatiza mjumbe wenu;

Hivi mwanamke anajisikiaje kuwa anapigiwa simu hapokei, anatumiwa meseji hajibu. Na usipomtafuta, ndo basi hamuwasiliani (yaani hadi umuanze wewe)

Na muda mwingine kwenye What's App meseji zinaonekana zimesomwa kabisa, lakini hajibu ukimlalamikia sana, baadae sana anakwambia neno "pole GENIUSTIN"

Hii tabia inamaanisha nini? Au siku hizi nimeanza kuwa mvulana? Maana hii tabia inaniumiza sana. Wanaume wenzangu na wanawake.

Naombeni mnifafanulie, ili nishtuke usingizini, kikombe hiki nikiepuke.

Nawasilisha.
 
Shtuka mkuu..
Ukiona manyoyaaaa
Penzi ni la wawili sio mmoja aumie
Raha ya penzi mshirikiane mshirikishane lol
But.....ongea nae kwanza may be yuko busy na majukumu yake atakueleza tu.
Paragraph ya kwanza imeniingia akilini.
Sasa hiyo ya pili, Ina maana uBusy hadi kushindwa kumjulia hali Partner wake?!!
 
Paragraph ya kwanza imeniingia akilini.
Sasa hiyo ya pili, Ina maana uBusy hadi kushindwa kumjulia hali Partner wake?!!
Wahi mapema kujitafutia anaekufaa huyo si wako....
Wanasemaga jiongezeeeee
Hakunaga ubusy kwa unaempenda na kumjali na kama upo lazima utamtaarifu in advance ili asiumie......
Huyo ako na mwingine anaempea attention not you.
Usikawie kufanya maamuzi utaumia maradufu....
 
Nashukuru kwa Ushauri wako.

Ingawa moyo unauma.
 
Back
Top Bottom