kwamtoro
JF-Expert Member
- Nov 15, 2010
- 4,922
- 3,236
Nina bahati mbaya sana na huyu mume wa mtu, jirani yangu.
Siku moja mke wake kaniita shemeji naomba uje unipe ushauri, kwa heshima na tahadhima nikaenda, tukawa tumekaa kitako akinieleza masahibu yanayo mkabili (sii ya ndoa) Mara mume wake huyoo.
Siku nyingine tena nikiwa narudi kutoka kazini, nikapanda basi ambalo ni la mwisho kunifikisha sehemu za makazi yangu, mara shemeji kapanda akaja kukaa siti moja na mimi, mara mume wake naye huyoo kapanda.
Siku nyingine tena nikawa nimetoka town nikashuka sehemu ya makazi yangu, shemeji naye akawa ameshuka kwa basi lingine tukaongozana, mara mume wake huyoo katoka dukani akatukuta tunaongozana.
Baada ya matukio hayo matatu juu, mimi na mume wake mahusiano yakashuka kwa kiwango kikubwa. Akawa kama mtu wa kunichunia hivi, mimi sikujali kwa sababu moyoni najijua siwezi fanya ujinga wa namna yeyote kwa mke wake.
Tukio la mwisho shemeji kaniita akaniambia anaomba nimsetie internet kwenye simu yake mara akasikia sauti ya mtoto ndani akilia. Akakimbilia ndani kwa mtoto, mara mume wake huyo kanikuta nimeshikilia simu ya mke wake. Nikamsalimia mume wake kauchuna mazima, nikamsubiri mke wake nikampa simu yake mimi nikasepa.
Sisi ni majirani, pia mimi nina mke na mtoto.
Binadamu tusiwe na mawazo mabaya, tutauwana bureee.